SEKESEKE: Wapangaji Majengo ya CDA Dodoma wanatimuliwa muda huu

SEKESEKE: Wapangaji Majengo ya CDA Dodoma wanatimuliwa muda huu

Ni tukio la aina yake, Wapangaji wa Nyumba za CDA maarufu kama "Maghorofani" wanatimuliwa muda huu, hii inatokana na lile Tangazo la hivi karibuni lililodai CDA wanataka kufanya ukarabati

Polisi wamejaa, ni taharuki tupu, hata kama mpangaji haupo wanavunja mlango vitu vinatolewa.

View attachment 373292View attachment 373293View attachment 373294View attachment 373290
View attachment 373288
Duuh hapo issue ni kodi tu, manake naona kuni tu ndio zimeanikwa nje,hamna furniture hapo,hata bi mkubwa wangu kisamvuchole hana furniture hizo.
 
kuna rafiki yangu alikuwa anaishi pale kwenye hayo maghorofa,tangu zamani sana wana mgogoro na CDA wanaambiwa wahame hawataki,CDA wanaita vikao hawahudhurii.jamaa aliniambia CDA wamesema wanataka kuyarepair hayo majengo maana yamechakaa sana so wakatakiwa wahame.hii kesi ina miaka so sioni kama kuna mtu kaonewa hapo.tatzo kupenda dezo maana kodi bei rahisi nyumba vyumba cjui vtatu sebule choo bafu kila familia/mpangaji mmoja,pale hata watu waliojenga hawakuachia vyumba,wengine wakitaka kuondoka wanampangisha mtu kwa chajuu.ukitaka kujua mtu kaonewa au laah,ielewe kwanza situation nzima.naona hapa watu wanalalamika tuu.
Naelewa watu wanaotumia hiyo mijengo wanakaa kama bure tu..na hata huwa hawataki kuiachia!
 
Hakuna alieonewa ...watu hawalipi kodi,kuna baadhi wanadaiwa hadi 1.6m...kodi ya mwezi Tsh 23,000/=....maisha hayo hayapo kwa sasa,majengo yamechaakaa notice ya kwanza ilitolewa 2004..hawatoki kila kukicha kukimbilia mahakamani..wapishe ukarabati
 
Wapishe ukarabati,hakuna alieonewa hapo mgogoro wa wao kutoka humu ni wa muda mrefu hata hivyo CDA waliwavumilia mnoo. Nyumba zikarabatiwe wengine tupange
 
Maghorofa yalizidi uchafu watu walikuwa wanapikia kuni wanafuga mabata ghorofani acha tu watupishe siye wastaarabu wa dasalamu tuhamie tutafuga kasuku tu
 
Kwenye mabadiriko yoyote ni lazima watu waumie..
Mkuu kweli wapo watakaoumia na wapo wanaopeta,lakini ikibidi tutangulize utu kwanza.Watu elfu mmoja wakiwemo watoto na akina mama inabidi tuvumilie japo miezi mitatu.
 
Aisee... Hii namba imesomeka in CAPS LOCK.
 
Na bado.Kila mtu lazima aonje shubiri awamu hii!
 
KODI ZAO WANAWARUDISHIA AMA?
Nyie mnachojua ni kuchangia kila jambo hata kama hamlifahamu ili mradi kupinga tuu.
Kwa taarifa yenu hao wipewa notice ya siku 90 na wakaongezewa siku 7 bado waligoma kutoka na waliambiwa wapishe ukarabati na pia asilimia 90 walikuwa wana dai kodi wana miaka zaidi ya 15 hawajalipa wana kwepa tuu.

Hebu jifunzeni kufatilia mambo kabla ya kuchangia.
hawa si ndo walimpa JPM kura 100% kazi mnayo wakoma....

Rais wetu anafanana na rais wa uturuki

Acha wanyooshswe hakuna vimbelembele Kama watu wa dom huwa wanajifanyaga Damu Yao ya kijani!

Ova
 
Back
Top Bottom