SEKESEKE: Wapangaji Majengo ya CDA Dodoma wanatimuliwa muda huu

SEKESEKE: Wapangaji Majengo ya CDA Dodoma wanatimuliwa muda huu

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
559
Reaction score
808
UPDATE

Zaidi ya wakazi 1100 waliokuwa wakiishi mtaa wa Maghorofa mengi manispaa ya Dodoma wameondolewa kwenye makazi yao kwa nguvu na mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA chini ya usimamizi wa jeshi la Polisi ambapo zoezi hilo limeacha simanzi na vilio kwa kaya 174.

Zoezi la kuwatoa wakazi hao kwenye nyumba hizo zilizoko kata ya Kikuyu Kusini lilianza mapema asubuhi likitekelezwa na kampuni ya udalali ya Mvina General Supply Limited kwa usimamizi wa Jeshi la Polisi.

Hata hivyo zoezi hilo almanusura liingie dosari baada ya baadhi ya vijana waliokuwa wakifanya vibarua kubainika kujihusisha na vitendo vya wizi lakini hata hivyo jeshi la Polisi lilikuwa macho na kufanikiwa kuzima majaribio yote ikiwemo la vijana wawili walioshirikiana kuiba fedha taslimu shilingi Milioni mbili na laki tisa ambao kamera ya ITV ilibahatika kuwanasa.

Zoezi hilo liliendelea ambapo wapo baadhi ya wapangaji waliondoa vitu vyao kwa hiyari huku wengine nguvu ikitumika ambapo kaimu katibu wa CDA Saidi Kamsumbile akisema limefuata taratibu za kisheria huku Mkurugenzi Mvina Ibrahim Kivike akidai awali kabla ya zoezi hilo walipewa notsi kuondoka ndani ya siku tisini na kisha kuwaongezea siku saba lakini hata hivyo walikaidi.

Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya wahanga wakiongozwa na Diwani wa eneo hilo wamelalamikia utaratibu uliotumika kwani umewasababishia hasara kubwa huku wakidai baadhi ya vitu vyao kupotea huku pia wakiua Mtaa ambao ulikuwa ukitambulika kisheria.

=============================
Ni tukio la aina yake, Wapangaji wa Nyumba za CDA maarufu kama "Maghorofani" wanatimuliwa muda huu, hii inatokana na lile Tangazo la hivi karibuni lililodai CDA wanataka kufanya ukarabati

Polisi wamejaa, ni taharuki tupu, hata kama mpangaji haupo wanavunja mlango vitu vinatolewa.

1469864303415.jpg
1469864326476.jpg
1469864267472.jpg
 

Attachments

  • 1469864348216.jpg
    1469864348216.jpg
    78.5 KB · Views: 167
Uchaguzi umeshapita ngoja Waisome namba sasa
Nilimuona Mh. Godless Lema jana akisimama na wananchi waliowekewa 'X' kwenye nyumba zao jimboni mwake, vipi nasikia hapo Dodoma kura zilikuwa nyingi ...mbunge wao yuko nao!?
Vipi hizo ndizo zitakuwa nyumba za mawaziri badala ya zile za Mikocheni au ni kwa ajili ya makatibu wakuu na wakurugenzi!? Tujuzeni wenye kujua.
 
hapa kwa mahesabu yangu ya haraka haraka nahs kuna wageni kutoka dar au wizara flan inayohamia dodoma wafanyakaz wanaandaliwa makazi
Hawa jamaa walishapewa notisi muda mrefu wakaenda mahakamani lakini mwenye nyumba (CDA) aling'ang'ania kuwatoa kwenye hizo nyumba. Ila sababu ya kuwatoa haifahamimiki ni ipi.
 
Back
Top Bottom