Sehemu salama zaidi kwenye ndege...

Sehemu salama zaidi kwenye ndege...

Sawa jirani. Naufanyia kazi ushauri. Naanza kuweka akiba kwa kibubu. Tupande hizi za ndani. Samahani. Naruhusiwa kupanda ndege nikiwa na mihogo mibichi na Karanga? Au Mahindi ya kuchoma?
Jirani
Unaongea na mie au Rrondo???!!
 
Inasaidia kujua wapi salama zaidi kukaa in case mnapambana na crash landing.
Dah...sasa wewe binafsi utakuwa kwenye kundi la 69 au 31? Uhai wa mtu binafsi kwa kibinafsi haupimwi kwa pasenti (%) zaidi ya 0% au 100%....yaani unapona au unakufa.... Watu wa bima ndiyo wanatumia takwimu hizo ili wajue watawalipa watu wangapi....au jeshini wajue wanabaki na nguvukazi kiasi gani....Kwa kifupi unaweza kukaa sehemu yenye usalama wa kupona 1% ikatokea ajali na wewe ndiyo ukapona....au ukakaa kwenye usalama wa kupona 99% ikatokea na wewe ndiyo uka RIP.....umenisoma?[emoji4]
 
Ndege ni usafiri salama zaidi duniani. Lakini ajali yake kupona ni kazi sana.
Kwa utafiti wa wataalam sehemu utakayokaa kwenye ndege ina nafasi kubwa sana kuamua uhai wako.

Igawe ndege mara tatu, kipande cha mbele,kati na nyuma.

1. Ukikaa mbele nafasi ya kupona ni 49%

2.Ukikaa kati nafasi ya kupona ni 56%

3.Ukikaa nyuma nafasi ya kupona ni 69%

Vile vile siti ya koridoni ni salama zaidi kuliko dirishani.
Jitahidi usikae zaidi ya mistari mitano kutoka mlango wa dharura.

Wanasema ndege ikianguka sehemu ya nyuma inameguka mara nyingi inabaki salama, sehemu ya kati kwa sababu ndio kuna tank la mafuta ndio huwa inaungua sana, sehemu ya mbele ndio ya kwanza kukutana na impact mfano kwenye crash landing.
Source:NatGe Air Crash Investigation
Mkuu uko makini, leo NatGeo ndio walikuwa wanaonesha hii kitu..nilidhani naangalia peke yangu[emoji15]
 
Mkuu uko makini, leo NatGeo ndio walikuwa wanaonesha hii kitu..nilidhani naangalia peke yangu[emoji15]
Jumapili huwa sikosi hizo episedes...
 
Dah...tafiti kama hizi hazimsaidii chochote msafiri kwa ubinafsi wake...labda watu kama wa bima[emoji13] [emoji13] [emoji87]
Unaambiwa ndege inapojipiga chini inakatika katikati kipande cha mbele linashika moto mara moja kwa kuwa kuna mafuta...nyie wanyuma mnabaki salamaaaaa..[emoji51] wewe endelea tu kukaa mbele.
 
Dah...sasa wewe binafsi utakuwa kwenye kundi la 69 au 31? Uhai wa mtu binafsi kwa kibinafsi haupimwi kwa pasenti (%) zaidi ya 0% au 100%....yaani unapona au unakufa.... Watu wa bima ndiyo wanatumia takwimu hizo ili wajue watawalipa watu wangapi....au jeshini wajue wanabaki na nguvukazi kiasi gani....Kwa kifupi unaweza kukaa sehemu yenye usalama wa kupona 1% ikatokea ajali na wewe ndiyo ukapona....au ukakaa kwenye usalama wa kupona 99% ikatokea na wewe ndiyo uka RIP.....umenisoma?[emoji4]
Kwahio wewe leo tukikwamvia ukishika waya wa umeme utakuwa na nafasi ya 99% kufa na 1% kupona utashika kwasababu unaweza kuwa wewe ni hio 1%? Jibu lako ndio litakuambia kama nimekusoma au sijakusoma
 
Unaambiwa ndege inapojipiga chini inakatika katikati kipande cha mbele linashika moto mara moja kwa kuwa kuna mafuta...nyie wanyuma mnabaki salamaaaaa..[emoji51] wewe endelea tu kukaa mbele.
Ukiandika thread lazima atakuja mtu au watu ku -challenge. Bahati mbaya hawasomi vizuri, huu ni utafiti wa watu waliofanya air crash investigation mbsli mbali duniani! Ni kichrkesho mtu anakuja na unproven ideas zake kupinga.
 
utaratibu wa ukataji tkt ukoje ktk ndege.au unapea chat ka ya mabasi uchague sits
Swali zuri sana.Unapangiwa seat.Lakini.ukifanya booking mwenyewe online au moja kwa moja kwa agent au airline unaweza kuchagua seat.Hii inaweza kuhitaji ongezeko la.fedha.Seat zingine zinahitaji ongezeko la gharama.Kwa ufupi mlango was ndege ukishafungwa ni kuomba kwa mungu!

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
Nilipanda ndege halafu nikakaa siti ya dirishani, ,sikua na amani kabisa. Kila nikitizama nje chini mbali mpaka nadata ikabidi nishushe shade. Mara nasikia kama ndege imeyumba, inapepea kama karatasi basi nafumba macho, nashika siti kwa nguvu ili nisionekane natetemeka. Naomba watuletee meli tu za masafa marefu kwenda ulaya, marekani, china uarabuni.
 
Treni je!? Imechangia vifo vingapi katika hyo 2975 iliyobaki!?
tran mzuri kama dar to tabora.ila tabora to dar unaweza lia maana linakua linashuka.balaa lipo ukitoka station ya (kidete) mnaitafuta kilosa ndio utajua chuma kinavyo kumya corners za ajabu mpaka aja kubwa unaisi kutoka
 
Aisee juzi nimepanda ndege ikafika sehemu ikapata turbulence moja mbaya sana.

Nilihisi ndo basi tena.

Nilikuwa nimeshika juisi mkononi ikamwagika...ndani ya ndege nikasikia sauti za vilio tu.

Kwa kweli huwa sipendi kusafiri kwa ndege.
Safari ni safari, sio ndege tu.

Siku nipo kwenye boti ikaanza kunepa, kina Mama na Watoto kama kawa wakaanza mayowe....kulikuwa na Ustaadhi mmoja akawa anatamka maneno ya Kiarabu kila Boti likiinuka, yeye ndiye aliongeza hofu kabisaa.
 
Kuna siku ET kutoka Guangzhou ile imepanda tu, si ikaanza tikisika........ Wanigeria nilikia tu Ooh My God.....
Ilitikisika kama dakika 3 hivi afu ikatulia....
Mie nikaanza hisi leo tunapiga chini Kama ile Fly Dubai kule Urusi.....
Nilijikaza kisabuni na kuomba Sala nyngi tu

Ukitaka jua watu wanapenda ishi na wanampenda Mungu ni pale dude likitkisika
 
Kwahio wewe leo tukikwamvia ukishika waya wa umeme utakuwa na nafasi ya 99% kufa na 1% kupona utashika kwasababu unaweza kuwa wewe ni hio 1%? Jibu lako ndio litakuambia kama nimekusoma au sijakusoma
Dah.... Kwahiyo kupona kuna anzia asilimia ngapi chief.,,0.001%..au.51% au 99.999%?[emoji41]
 
Unatulisha matango pori. Mleta mada Nitafutie ndege 5 tu zilizo crush na watu wakapona kwa hiyo percentage uliyotupatia!!!
 
Unatulisha matango pori. Mleta mada Nitafutie ndege 5 tu zilizo crush na watu wakapona kwa hiyo percentage uliyotupatia!!!
Acha uvivu. Tumia bundle lako kutafuta data. Hivi shule mnasomea ujinga? Nimeweka wazi utafiti huu umeelezewa leo kwenye NatGeo Air Crash Investigation channel itafute ujifunze.
 
Back
Top Bottom