Sehemu salama zaidi kwenye ndege...

Sehemu salama zaidi kwenye ndege...

Sasa bro si unatuharibia biashara?

Wateja wote watataka siti hizo tutashindwa kufanya booking kwasababu aina ya siti kama hizo zitajaa fasta.
Huwezi kuahirisha safari kisa siti ya nyuma au koridoni hamna. Huyo atakuwa sio msafiri.
 
Muda ukifika wa kufa hata kama upo bafuni unakufa tu hakuna namna, marubani waendesha mpaka wanastaafu bila tatizo na kila siku wapo mbele.
 
Ha ha ha haizoeleki hii...ndege raha yake ukishashuka uko lounge unabarizi...
Yaani nioipofika Ugiriki transit hadi nilitamani kuwe na meli ya kurudi Bongo. Ila ndege wanazopeleka Ulaya nzuri sana. Nilikata bia hadi wakati nashuka bongo nusu nidondoke kwenye ngazi, maana nilikaa nyuma karibu na mikabati ya bia.
 
Muda ukifika wa kufa hata kama upo bafuni unakufa tu hakuna namna, marubani waendesha mpaka wanastaafu bila tatizo na kila siku wapo mbele.
Totally missed the point.
 
usafiri wa anga sijawahi kuuzoea na sitokaa niuzoee, roho mkononi muda wote
 
usafiri wangu salama naouamini ni miguu yangu tuu
Kwa taarifa yako una nafasi kubwa ya kugongwa na baiskeli,bodaboda,gari kuliko kupata ajali ya ndege. Kwahio hio miguu sio salama kiviiile.
 
Hahahahaa kwenye kenopi ni salama. Na mie naiga hii
Siku yako ikifika imefika tuu, lakini tahadhari ni muhimu pia!!!!

Ngoja nikariri siku nikibahatika kuipanda nikae koridoni!!!
 
Aisee juzi nimepanda ndege ikafika sehemu ikapata turbulence moja mbaya sana.

Nilihisi ndo basi tena.

Nilikuwa nimeshika juisi mkononi ikamwagika...ndani ya ndege nikasikia sauti za vilio tu.

Kwa kweli huwa sipendi kusafiri kwa ndege.
Na wewe ni wa kabila la kanda ile?
 
Ndege ni usafiri salama zaidi duniani. Lakini ajali yake kupona ni kazi sana.
Kwa utafiti wa wataalam sehemu utakayokaa kwenye ndege ina nafasi kubwa sana kuamua uhai wako.

Igawe ndege mara tatu, kipande cha mbele,kati na nyuma.

1. Ukikaa mbele nafasi ya kupona ni 49%

2.Ukikaa kati nafasi ya kupona ni 56%

3.Ukikaa nyuma nafasi ya kupona ni 69%

Vile vile siti ya koridoni ni salama zaidi kuliko dirishani.
Jitahidi usikae zaidi ya mistari mitano kutoka mlango wa dharura.

Wanasema ndege ikianguka sehemu ya nyuma inameguka mara nyingi inabaki salama, sehemu ya kati kwa sababu ndio kuna tank la mafuta ndio huwa inaungua sana, sehemu ya mbele ndio ya kwanza kukutana na impact mfano kwenye crash landing.
Source:NatGe Air Crash Investigation
utaratibu wa ukataji tkt ukoje ktk ndege.au unapea chat ka ya mabasi uchague sits
 
Back
Top Bottom