Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 27,549
- 34,877
Wivu utakuua.Leo tuangazie wasongo.
Unaweza kuwa kumefaulu vizuri na unaweza kuwa ni bora masomoni. Lakini unapokuja mtaani watu hawataki kuona vyeti bali wanataka wasikie kitu tofauti ulichonacho ukifananisha na pengine wanavyovijua au vya wenzako ambao mupo pamoja kwenye interview (usahili)
Wengine ushangaa kuna wale ambao darasani walikuwa midiocre (vilaza) lakini kila interview wakienda upata kazi, ili sio suala la kupendelewa au sijui ana ndugu bali ni kitazamo wa fikra.
Kuna watu wanaajiriwa pasipo kuulizwa vyeti, yaani professional resume (wasifu wako wa kitaaluma) pekee unatosha kukupa kazi.
Phrase ya SO WHAT? Ni namna unavyotakiwa kueleza mafanikio yako ya kishule unayashabihiaha vipi na kitu watu wanafanya au wanataka.
Yaani umefaulu Computer science na first class sasa tuambie kwenye mfumo huu wa biashara ama kwa biashara yetu ama kwa wateja wetu taaluma uliyonayo utakuja na njia gani mbadala ya kuwezesha ubora wa biashara.
Namna yote utakavyo jinasibu inabidi isharabu kwa nafasi au majukumu unayotarajia kuyaganya kwenye fursa iliyoko mbele yako.
Kwa hivyo basi tumia muda mwingi kujigenga kwenye business environment yaani namna gani biashara inafanywa, mapungufu yalipo kisha buni jinsi utakavyoweza kutatua changamoto zilizopo au zitakazo kuja.
Kwa kujenga fikra za namna hii basi Muhitimu au mtafuta fursa utakuwa katika nafasi nzuri ya kupata nafasi.
TUZIDI KUTAFAKARI ZAIDI