Zitto acha kupotosha. Ni hivi, makusanyo ya Awamu ya Nne ni sawa na makusanyo ya mwaka mmoja tu katika Awamu ya Tano

Leslie Mbena

Verified Member
Nov 24, 2019
69
150
ZITTO ACHA KUPOTOSHA. NI HIVI, MAKUSANYO YA AWAMU YA NNE NI SAWA NA MAKUSANYO YA MWAKA MMOJA TU KATIKA AWAMU YA TANO.

Leo 10:15am,13/04/2020

Kulinganisha makusanyo ya miaka mitatu ya mwisho ya awamu ya nne na makusanyo ya miaka mitatu ya muhula wa kwanza katika awamu ya tano ni kutaka kupotosha au kutokuwa na ufahamu sahihi ama chuki binafsi maana awamu ya nne ni kichuguu na awamu ya tano ni mlima, nilisema kijana Zitto ni mdini, mfitinishaji na msaliti kwa Taifa la Tanzania.

Zitto kataja kutofikiwa lengo la makusanyo katika miaka mitatu ya mwisho ya muhula wa kwanza wa Rais John Magufuli huku akisema miaka hiyo mitatu imepitwa na takwimu za miaka mitatu ya mwisho ya awamu ya nne lakini kaacha kutaja kiasi halisi kilichokusanywa awamu ya tano yaani 2017/18,2018/19,2019/20 huku ni kupotosha Umma, pengine gentleman yake aliyoipata katika digrii yake ya uchumi ndio inaendelea kumsumbua.

Ni hivi makusanyo ya mwisho ya awamu ya nne 2012/13,2013/14,2014/15 kwa pamoja yalikuwa sawa na tzs 28 trilioni ambayo ni sawa na makusanyo ya mwaka mmoja tu ya muhula wa kwanza katika awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ambapo 2017/18 Serikali ya Rais John Magufuli ilikusanya tzs 27.7 trilioni.Sasa lazima Kijana Zitto akemewe maana ulongo ulongo wake na husda vikiachwa vitaonekana ni kweli.

Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba, makusanyo ya miaka ya 2012/13 (TZS.8Trilion), 2013/14( TZS.9.28Trilion.), na Mwaka 2014/15 ( TZS.10.77Trilion) sawa na jumla ya (TZS.28Trilioni) ambayo ni sawa na makusanyo ya kodi ya mwaka mmoja tu (2017/18) chini ya JPM.

Kifupi makusanyo ya awamu ya nne kwa mwezi yalikuwa wastani wa TZS. 850bn, kiasi ambacho hakikutosha hata kumudu malipo ya deni la Taifa kwa mwezi na mshahara. Malipo ya deni kwa mwezi yalikuwa wastani wa 650bn, na Mshahara kwa mwezi ilikuwa wastani 550bn sawa na 1100bn. Hivyo ilibidi kukopa kuweza kumudu kulipa mshahara.

Pengine haya ndio yalikuwa msingi wa kejeli za Rais Uhuru Kenyatta miaka hiyo kwamba ilikuwa Kenya peke yake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoweza kumudu kulipa mshahara watumishi wake bila kukopa watu wanasahau sana,huu ni wakati wa kumsifu sana Rais John Magufuli maana si Kenya wala Rwanda anaeweza kutufanyia kejeli tena.

Wastani wa makusanyo ya sasa ya kodi tu kwa mwezi yanatosha kumudu deni na mshahara na hivyo Serikali haikopi tena kulipa mshahara watumishi wake,Shukrani Mh David Kafulila kwa data malidhawa ulizotupati kumjibu Kijana Zitto,huyu bwana hasipojibiwa ataongea uongo na kuwaaminisha watu kama alivyowaaminisha hapo mwanzo eti 1.5 imeibiwa!?

-Kijana Zitto aandika barua nyingine IMF kuikagua Benki Kuu.

Mwaka 2017, kwa mara ya kwanza katika historia,Tanzania ilifanyiwa uhakiki kuhusu uthabiti wa kiuchumi kuweza kukopesheka (Credit rating), kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Moody's ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa duniani katika kazi hizi (inamiliki asilimia 45% ya soko), ilitoa matokeo yake mwezi Machi2017, kuonesha kwamba Tanzania ina daraja la B1 juu ya Kenya, Uganda ambazo zilikuwa na B2. Ripoti hii ilizua mjadala mkali sana Kenya (Business Daily, 4th, March2017).

Mwaka 2018, Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu( Inclusive Economy) , na ya tatu kwa bara zima ikitanguliwa na Algeria na Tunisia(World Economic Forum 2018). Sikatai kwamba kuna mengi ya kufanyia kazi zaidi, lakini rekodi hizi ni kubwa na fahari kwetu kama Taifa kwamba tunakwenda vizuri katika maeneo mengi kuhusu ujenzi wa uchumi

Mwaka 2017, IMF, iliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa manne ya Afrika yanayoelekea safari ya Vietnam katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nchi zingine ni Nigeria, Kenya na Ethiopia. Rejea mahojiano ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF), Bi Christine Lagarde, alipohojiwa na Jarida la Quartz akiwa Addis nchini Ethiopia alipotembelea Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika( UN- Economic Commission for Africa).

Mwaka 2019,Serikali ya Tanzania ilitangazwa kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa fedha za Umma (World Economic forum, Economic Opinion Survey 2019).Kwa mujibu wa Ripoti hiyo nchi za Kenya ilishika nafasi ya 70,Uganda 100,Ethiopia 48,Malawi 106,Msumbiji 118,Ghana 61,Zambia 68 na Botswana 37.

-Kijana Zitto,kama masikio yako hayasikii basi macho yako yanaona miradi mikubwa inayomaliziwa katika Awamu hii ya tano.

Mapinduzi makubwa Sekta ya miundombinu na rasilimali watu yanaonekana bayana kwa kila mtanzania. Naamini kasi ya sasa ingekuwepo miaka 30 nyuma , ni wazi leo tungekuwa washindani wa Mataifa kama Vietnam.

Kwa mujibu wa Benk ya dunia,kufikia mwaka 1990, uchumi wa Tanzania ulikuwa dola 4.5bn nyuma ya Vietnam ikiwa na dola 6.5bn huku Kenya ikiwa mbele ya Vietnam kwa uchumi wa dola 8.4bn. Leo mwaka 2020, ikiwa ni miaka30, Uchumi wa Vietnam ni dola 260bn, ikiipita Kenya yenye dola bilion 90 na Tanzania dola 60bn.

Ujenzi wa miradi mikubwa kimkakati kama Stirglers Gorge utakaozalisha umeme zaidi ya 2100MW na Ujenzi wa Reli ya kati ya sanjari na kufufua shirika la ndege ndio majibu kuelekea huko.

Nisisi watanzania tuliopiga kelele Serikali kumiliki ndege1 tena mbovu na wakati mwingine kukodi ndege kwa gharama kubwa kuliko gharama ya kununua ( CAG report 2015/16). Nisisi tuliopiga kelele reli iliyozeeka kutoka uwezo wa tani milioni 5 mpaka tani laki4.

Nisisi tuliopiga kelele kuhusu sekta ya umeme ilivyonyonga uchumi wetu kwa biashara za mitambo ya kukodi ambayo imekamua uchumi na kuacha nchi mifupa mitupu.

Kinachofanyika sasa ndio safari kuelekea vietnam japo ilipaswa tuanze zamani.Mikopo kwa miradi ya kimkakati kama hii ina uhalali kulinganisha na tulikotoka ambapo tulikopa kulipa mishahara na kuendesha Serikali ( Recurrent Expenditure)

Hoja ya ujenzi wa rasilimali watu. Haihitaji miwani kuona mapinduzi makubwa haya. Sekta ya Elimu, Afya na Maji zimepiga hatua kubwa. Tafiti zinaonesha kwamba kila dola1 inayowekezwa kwenye maji inaokoa dola 4.2 ambazo zingewekezwa kwenye dawa ambazo ni matokeo ya tatizo la maji safi. Kuna mafanikio makubwa lakini changamoto za sekta hii kwa kiasi kikubwa ni miradi ya kurithi tulikotoka.

# Kuongeza mikopo elimu ya juu kutoka 360bn mwaka 2015 mpaka 450bn ni juhudi zilizo bayana. Kupeleka 23bn kila mwezi kuhakikisha Elimu- bure ni ndoto iliyogeuka kweli na kusababisha takribani watoto 1m waliokuwa wakikosa shule kila mwaka sasa wanasoma.Changamoto za ubora ni suala endelevu kuhakikisha tunazalisha nguvu kazi yenye uwezo wa kuhimili ushindani wa soko la ajira.

#Aidha mapinduzi ya Sekta ya afya nayo ni bayana. Ripoti za NHIF zinaonesha mwamko mkubwa kwa watanzania kuwa na bima ya afya kutoka milioni 9 kabla ya awamu ya tano mpaka zaidi ya milioni16.

# Ongezeko la fedha za dawa na vifaa na tiba kutoka 31bn mwaka 2015 mpaka 269bn sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 700% ni mafanikio ya mfano.

# Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonesha kasi ya maambukizi ya malaria kushuka kutoka asilimia 14% mwaka 2015 mpaka asilimia7%.

-Nimalizie na hoja hii ya kijana Zitto anayosema Serikali inaficha madeni ya mifuko ya hifadhi.

Kwanza ni changamoto ya madeni yenyewe kwa namna yalivyopatikana kabla ya awamu yake ya tano, Sio siri kwamba kabla ya Rais John Magufuli, mifuko ya hifadhi iligeuzwa shamba la bibi na mali ya genge fulani.Huu ni ukweli unaothibitishwa na taarifa ya taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya E& Y ya Disemba2015, habari za uchunguzi za majarida makubwa ya kimataifa kama Africa Confidential na Africa Research Institute.

Kwa mfano, Ujenzi wa Chuo Kikuu UDOM, mifuko ilikuwa ikidai jumla ya TZS 5.3Trilioni lakini baada ya ukaguzi deni halali likakutwa TZS.3.2Trilion sawa na deni hewa la zaidi ya TZS.2.1Trilion.

Sielewi Kiongozi kama Kijana Zitto anaesisitiza deni lilipwe kama lilivyo kama kweli ana mapenzi na watanzania walipa kodi? Hata kama hana mapenzi na walipa kodi wa nchi hii vema awe japo na huruma basi! Je unataka tumkamue ng'ombe hadi itoke damu badala ya maziwa.

Hoja kwamba Serikali ya Awamu ya tano ina kesi nyingi kwa kuvunja mikataba.
Hapa ni vema ikaeleweka kwamba;

Kwanza kesi hizo ni matokeo ya mikataba mibovu ya zamani ambayo Rais John Magufuli amerithi kutokana na udhaifu mkubwa huko tulikotoka na sio mikataba ndani ya awamu ya tano

Mfano, uamuzi wa Serikali kufuta mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion iliyorithi mitambo ya Dowans/ Richmond, imepunguza mzigo wa kinachoitwa tozo ya gharama ya uwekezaji ( capacity charges) kwa mwezi kutoka dola milioni 16.35( zaidi ya bilioni 37.6)mpaka dola milioni 9.75 ( sawa na bilioni 22.4) kwa mwezi( Rejea CAG report 2017).

Inahitaji ukatili sana kwa Taifa lako na roho ya husda na chuki binafsi kumlalamikia Rais Magufuli kufuta mikataba mibovu kama Symbion kwani kinachoitwa tozo ya ya gharama za uwekezaji ni mfano wa mbaya wa mikataba ya hovyo ambapo mwekezaji analipwa bila kujali amezalisha umeme au la eti kufidia gharama alizotumia kuwekeza.

Vema kufahamu kwamba zama za Serikali kulipa madeni ya mikataba mibovu tumeshavuka. Huko tulikotoka Serikali iliwahi kulipa deni la Dowans kinyemela kiasi cha dola milioni 94 ( zaidi ya bilioni 200 wakati huo).Hakika inahitaji roho kutamani zama hizo, ni Taifa la 'wapumbavu' linaloweza kupigania Serikali yao ilipe madeni ya aina hii!

Nimalizie kwa kusema haya na Zitto usikie, Rais John Magufuli ndiye Rais kwa mfano wa Mwalimu Julius Nyerere anayeongoza Serikali inayozingatia maslahi ya watu wote wenye nacho na wasio nacho,wenye sauti na wasio na sauti,

Kijana Zitto ilipenda sana nchi iendeshwe kwa maslahi yako binafsi kama sasa ulivyo tajiri,Rais Magufuli anajenga Taifa ambalo mtanzania hatokosa fursa ya elimu bora,huduma bora ya afya kwa sababu ya umasikini wa familia yake,tumeanza kutoka kwenye Taifa lililokuwa kwenye mikono ya mishenitown na kurudi kwenye Taifa la Watanzania.

Ahsante Mh David Kafulila kwa kuwa Mzalendo,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki Rais wetu John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa, Mimi ni

Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 

mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,575
2,000
Acheni kujifanya wajinga hamjui jiwe amechukua makusanyo yote ya serikali ndo yanaonekana yamepanda mpaka ada za wanafunzi? Enzi za jk vyanzo vya halimashauri vilibakishwa,maduhur ya taasis hayakuhesabiwa yey amejumlisha yote ndo hayo yanaonekana matrilion.

Eti eeh miradi mingi ameanzisha wamesahau hata deni la taifa limevunja record kwa maana amekopa sana, ni wajinga watakubaliana na vuvuzera anayelamba sukari ya mfalme juha apingane naye
 

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
622
1,000
Tunaojua tunakuangalia tu. Serikali hii kelele nyingi, angalia inavyokopa kwa kwenda mbele! Hayo makusanyo kama yanatosha mbona matatizo ndiyo kwanza yanaongezeka?

Matatizo ya serikali hii ni mengi kuliko mafanikio, ingekuwa ni vema ukaacha mahaba na propaganda. Hii serikali haijatufikisha popote na tunakoelekea ni kubaya zaidi.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,096
2,000
Umesahau kuelezea miradi mikuu ya mkakati Reli, bwawa la Nyerere, Daraja Kigongo,Busisi, Sarenda, zahanati, vituo vya afya,hospitali za wilaya, mkoa na rufaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chance yake ya kukamilika ni ngapi? Isije kuwa imewekewa mawe ya msingi na kuchimba chimba ili mpate kuongopea watu kwenye uchaguzi ukishapita tu nayo imelala.

Yule bwana hajali kuhusu riba au hasara lijapo swala la sifa kwanza.Check marudio ya chaguzi zisizo za lzm ya kuchezea Kodi zetu, manunuzi, nk kwake sifa ni muhimu kuliko Kodi zetu.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,096
2,000
Kwa miaka 5 ya awamu hii deni la taifa limeongezeka pa kubwa kuliko awamu zote tokea Uhuru.Miaka 5 ni zaidi ya jumla ya madeni ya awamu zote nne tokea Uhuru.

Tunafikia mwisho wa kukopesheka sijui itakamilikaje miradi kwa kutegemea kukopa
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,521
2,000
Sasa Polepole umebaki kusubiri wachambuzi wengine kisha wewe kuedit na kuirusha. Ulipaswa ww uandike ya kwako na sio kusubiri ya Kafulila kisha uhairiri.

Na vyema ungeongelea hiyo 1.7t ambayo Zito kasema haikupitia mfuko mkuu wa serikali.
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
6,290
2,000
Huyo jamaa ni muongo sana, na ukichangia nyuzi zake Mods wanafuta, hivyo nimeamua kuachana na nyuzi zake. Ni muongo halafu hataki kuambiwa ukweli. Analindwa na Uongozi wa JF.
Aliwahi kuwa waziri kivuli wa kambi ya upinzani akachemka kuwasiliana bajeti mbadala kanajua kukosoa tu amemiss uenyekiti wa pac maana ndipo alipokuwa anafanyia dili zake
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,096
2,000
Umesahau kuelezea miradi mikuu ya mkakati Reli, bwawa la Nyerere, Daraja Kigongo,Busisi, Sarenda, zahanati, vituo vya afya,hospitali za wilaya, mkoa na rufaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Awamu hii imeanzisha miradi mingi Kama sehemu ya kupigia badala ya kukamilika ya zamani au kuiboresha.Ataingia mwingine nae ataanzisha ya kwake apate pa kupigia. Hii tabia ya kila ajae huacha aliyoikuta na kuanza na ya kwake ni ngumu sana kuendelea wanachezea tu Kodi zetu
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,610
2,000
Kwamba unakusanya mara mbili halafu hautoi ajira, huna pesa za kupambana na corona, budget ya kilimo iliyopita haijatekelezwa kwa 70%+, pesa za elimu hazijapelekwa kwa 30% mwenzio unayesema akukusanya kodi kila mwaka alikuwa anamwaga ajira, mikopo vyuo vikuu mpato yake graph yake ilikuwa ikipanda kila mwezi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom