Sawa una First Class degree, una A ya Hesabu na wewe ni best student. So what?

Sawa una First Class degree, una A ya Hesabu na wewe ni best student. So what?

Naona vilaza mliofeli darasani mnafarijika sana mnapoona sie tuliokua tunawaongoza kitaaluma shuleni tunapofeli maisha.

Kusoma sana na kufaulu kuna umuhimu wake. Usiache kumkazania mwanao akawa best in academics maana the future will be very bright kwake despite of some minor corrugations on the way!!!

Ni wachache sana wataelewa mlengo wa hoja hii kwa sababu uwasilishwaji wake sivyo ulivyotegemewa.
[emoji1787]
 
Kiti cha ziada ni kipi bongo wewe

Wengi hawapati nafasi ikiwapo Lugha ni tatizo, hakuna mtu mwenye kitu cha ziada bwana,

Wenye kitu cha ziada sio hao

Kuna wengine unaweza kuwahoji kwa kiswahili pekee na bado akawa hana content zaidi ya kusema alivyokariri darasani
 
Naelewa kwa nini huwezi kuelewa.
[emoji1787]

Kupata A na first class ni mafanikio. Mimi I did so well in school, nilipa degree in Accounting kwenye year 2002, na CPA 2004.

Sikuwahi ajiriwa mda mrefu, only 8 months mpaka leo nafanya biashara, najitegema, hizi biashara nazo fanya sio kwa kutumia taaluma yangu.

Ila nataka nikueleze elimu yangu na performance zangu nzuri zimenipa fursa nyingi sana katika biashara, relevant discussions na uelewa.

Kupata A zote, GPA nzuri ina impact na ni jambo jema, ni upumbavu na ujuha kuleta swala la Ajira na kuhoji sababu za kupambana ku perform vizuri.
 
Kila nyakati Zina mahitaji yake na Kila kizazi kina akili na uelewa wake.Wanafunzi wengi wa vijijini hawafaulu sana wakati mwingine sio kama hawana akili bali background na wapo ambao ni genious wanatoka vizuri pia.Lakini kwa Dunia ya Leo inahitaji vyote ufaulu mzuri na maarifa.

Mtu akifeli na hana maarifa anakuwa tegemezi,mtu akifaulu vizuri akawa hana maarifa ni mzigo pia.

Kwangu Mimi A A zenye kufanya tofauti ni muhimu sana kwa Dunia ya sasa japo muhimu ni umezipataje pengine umetazamia au umekariri .Miaka ya nyuma tulikesha usiku wa manane kusoma vitabu huku tukikariri sana ndio maana tunaweza tusiwe na impact kwa kuwa tulikua na uwezo wa kukariri jambo ambalo ni ngumu sana kukonvert hayo mambo kwenye reality.

Lakini nyakati hizi zinataka uelewa na reality.Ukipata nafasi ya kufanya jambo lifanye kwa bidii kwa akili zako zote na kwa uwezo wako wote maana hutakuja wakati huo.

Pia GPA ya 4 au 3 even Gentleman inaweza kuwa positive au negative impact kutegemeana mazingira.Mtu aliyepo China,UK,German anaweza kuonekena tofauti kwa kuwa mazingira yao yanahitaji kitu cha pekee yeye kushine ukija kwetu kwenye vyeti mtu anaweza asioneshe utofauti kulingana mazingira hayamlaximishi bali Yanamtukuza zaidi hivyo naye anaweza kuwa mzembe pia.
 
Kupata A zote, GPA nzuri ina impact na ni jambo jema
Hivi kupata A ndiyo kuwa na akili? Au ni kuwa na uwezo mkubwa wa darasani?

Unajua mpaka leo hii Tanzania imeongozwa na wanafunzi bora kwenye taasisi na wizara wangapi? Lengo limefikiwa? Hawana akili?

Mimi huwa naamini kupata A ni kipaji kama vipaji vingine( hasa kwa bongo )na haimanishi una akili.

Bongo tunashindana kukariri, ambaye mwenye kipaji cha kukariri ataibuka mshindi
.

Tembea mtaani uone akili zinavyofanya kazi halafu uone A yako na G.P.A zina msaada gani.Hizi zimewekwa kama mchujo kwa lengo fulani.

Elimu ni muhimu na lengo lake lazima litimie ambalo ni kutoa ujuzi, maarifa na uzoefu lakini haimanishi ukivipata hivi una akili!!!!!
 
Hivi kupata A ndiyo kuwa na akili? Au ni kuwa na uwezo mkubwa wa darasani?

Unajua mpake leo hii Tanzania imeongozwa na wanafunzi bora kwenye taasisi na wizara wangapi? Lengo limefikiwa? Hawana akili?

Mimi huwa naamini kupata A ni kipaji kama vipaji vingine( hasa kwa bongo )na haimanishai una akili.

Bongo tunashindana kukariri, ambaye mwenye kipaji cha kukariri ataibuka mshindi
.

Tembea mtaani uone akili zinavyofanya kazi halafu uone A yako na G.P.A zina msaada gani.Hizi zimewekwa kama mchujo kwa lengo fulani.

Elimu ni muhimu na lengo lake lazima litimie ambalo ni kutoa ujuzi, maarifa na uzoefu lakini haimanishi ukivipata hivi una akili!!!!!

Akili ni nini wewe Mtu? Maana huo ni mjadala, dunia nzima, ulimwengu wote umeweka namna ya utambuzi na ufanyaji kazi, na huo unahusisha performance kwenye grades A, B..... Sasa sijui shida yako ni nini.
 
Akili ni nini wewe Mtu? Maana huo ni mjadala, dunia nzima, ulimwengu wote umeweka namna ya utambuzi na ufanyaji kazi, na huo unahusisha performance kwenye grades A, B..... Sasa sijui shida yako ni nini.
Punguza mhemko na papara ndugu, hivyo ni viwango vya mchujo na siyo akili. Au wewe ndiyo unaamini kuwa huo mchujo ni akili? Nimesema kuwa huo mchujo umewekwa kwa lengo maalumu.

Shida yangu ni kuhusisha huo mchujo ndiyo akili wakati siyo kweli!

Ninyi ndiyo mnaamini kuwa ufaulu wa darasani lazima uendane na maisha mazuri, halafu mkiwakuta waliofeli darasani wana maisha mazuri mnabaki na masikitiko, huzuni, roho mbaya, chuki, hasira, vijiba,fitina na majungu! Toka gizani!


Is intelligence more than the ability to perform well in school?


Intelligence is much more than the ability to perform well in school as it is the ability to comprehend the world, reason rationally, and effectively employ resources to deal with the challenges of life.


Testbook.com - India's No.1 Govt Exam Preparation Site | Online Course | Mock Test › question-answer
 
Elimu ni nzuri mno endapo itatumiwa ipasavyo, kinyume na hapo lazima hitilafu itokee.
 
Mtoa mada anasema A flat
Katika taaluma zikija mtaani
Tunatarajia matokeo sawa na uwezo wao darasani yani katika jambo mtu atakalofanya liwe na matokeo makubwa sana kuendana na uwezo wake shule tofauti na watu wengine
Lakini mambo huwa tofauti kwanini?

Wewe unatuambia ulaya wanalipa vyeti

Na zaidi unaleta story za kitambo ambazo ushindani ulikuwa mdogo form four walikuwa wanatamba
Nafikiri wakati huu ndiyo ungekuwa mzuri zaidi kwa hao mabwana kuipeleka nchi kwenye level nyingine
 
Nchi za wenye akili ambao si manyani , unapata kazi nzuri , with high pay. Nadhani umezaliwa juzi kwenye shule za kata na na University za kata.

Ukipata A A A ....University unabaki pale (enzi hizo za dunia ya watu) kuwa Totorial Assitant, then unasoma masters, unakuwa Lecturer. PhD unagombea Uprof.... Mshahara mkubwa na research kwa wingi...means pesa.

On top of that na Heshima kwenye jamii! (hili ndilo la muhimu sana. ) Magufuli aliwatumia so called Profs sana kwenye teuzi zake.

For the academic year 2021-2022, at Harvard University
  • The Professor salary is increased by 3.15 % from $245,268 to $252,991 over 995 Professors.
  • The Associate professor salary is increased by 5.32 % from $147,508 to $155,351 over 135 Associate professors.
  • Sorry boss hio salary uloandika inalipwa hapa TANZANIA au nchi za wenzetu ni kwa muda gan Monthly au Annually na vp ni USD au TZ Currency kulingana na ulivyoandika

    nawasilisha
 
  • Sorry boss hio salary uloandika inalipwa hapa TANZANIA au nchi za wenzetu ni kwa muda gan Monthly au Annually na vp ni USD au TZ Currency kulingana na ulivyoandika

    nawasilisha
soma vema rafiki Havard University/month/usd... na nimesema nchi za wenzetu siyo zetu hizi za manyani, wezi etc etc
 
Acheni hizo siamini kama wewe na GPA yako ya 2.1 kama unaweza kumshinda kwenye interview mtu mwenye 4.5, siamini?

Japo mimi ni mzee wa makalai, lakini hao wanaopata GPA kuanzia 4.5 ni exceptional aisee!
Mkuu umenichekesha kinoma , kwamba wewe ulikua unasoma ili umalize tu chuo , mengine achia wasongolist
 
soma vema rafiki Havard University/month/usd... na nimesema nchi za wenzetu siyo zetu hizi za manyani, wezi etc etc
OOOH hapo sawa nimeelewa, nilidhan bongo hii kuna mtu monthly ana salary ya hivyo sisi tutakaki na vi 300k zetu maisha yaendelee
 
Back
Top Bottom