Leo tuangazie wasongo.
Unaweza kuwa kumefaulu vizuri na unaweza kuwa ni bora masomoni. Lakini unapokuja mtaani watu hawataki kuona vyeti bali wanataka wasikie kitu tofauti ulichonacho ukifananisha na pengine wanavyovijua au vya wenzako ambao mupo pamoja kwenye interview (usahili)
Wengine ushangaa kuna wale ambao darasani walikuwa midiocre (vilaza) lakini kila interview wakienda upata kazi, ili sio suala la kupendelewa au sijui ana ndugu bali ni kitazamo wa fikra.
Kuna watu wanaajiriwa pasipo kuulizwa vyeti, yaani professional resume (wasifu wako wa kitaaluma) pekee unatosha kukupa kazi.
Phrase ya SO WHAT? Ni namna unavyotakiwa kueleza mafanikio yako ya kishule unayashabihiaha vipi na kitu watu wanafanya au wanataka.
Yaani umefaulu Computer science na first class sasa tuambie kwenye mfumo huu wa biashara ama kwa biashara yetu ama kwa wateja wetu taaluma uliyonayo utakuja na njia gani mbadala ya kuwezesha ubora wa biashara.
Namna yote utakavyo jinasibu inabidi isharabu kwa nafasi au majukumu unayotarajia kuyaganya kwenye fursa iliyoko mbele yako.
Kwa hivyo basi tumia muda mwingi kujigenga kwenye business environment yaani namna gani biashara inafanywa, mapungufu yalipo kisha buni jinsi utakavyoweza kutatua changamoto zilizopo au zitakazo kuja.
Kwa kujenga fikra za namna hii basi Muhitimu au mtafuta fursa utakuwa katika nafasi nzuri ya kupata nafasi.
TUZIDI KUTAFAKARI ZAIDI
Hii Ni emotional pain trauma umebeba. So watu wasipate first class na A za hesabu ama unamaanishaje.
Inaonekana ulizitafuta ukazikosa so brain inatafuta namna ya kujifariji Ni sawa na wale waliofeli wanaongea kuwa Nina pesa elimu ya Nini.
Ni kawaida ama Ni nature ya brain kutafuta sababu za kuondokana na maumivu makali ama habari ambayo inaenda kinyume na inavyotaka.
So tujishushe tusipate A ama wani.
Ndio unadhani utakuwa vizuri mtaani. Kila mtu Ana kipaji chake ,wewe Kama uko mtaani vyema ndipo panapokufaa na huyo Kama amekuzidi shuleni usitake kuonekana kuwa hujapungukiwa na kitu kwa kumshusha huyo hapo.
Ndio wale akina msukuma anawaponda wasomi baadaye anaenda kununua elimu ili lile pengo lake la kutokuwa na elimu alizibe,Mana Anazo hela Ila ndani ya nafsi yake bado anateseka ana feel inadequacy,sense of mattering,yaani binadamu bana akifanikisha kitu yeye Ni mjanja akifanikisha mwingine amebahatisha.
Akichelewa binadamu Ni bahati mbaya Mara jam njiani akichelewa nguruwe Ni kawaida yake kuchelewa huyo akazoea.
Kasomeni cognitive dissonance inavyofanya tunafanya maamuzi ya self-service.
Ukishindwa maisha unatupia lawama serikali ama wazazi ama mtu yeyote Ila ungefanikisha unajisifu kuwa mie Ni mjanja nimepigana bila ya kushikwa mkono,sijasoma,yaani nimetoka kwetu masikini nimetoboa. Watu Wana tafuta attention Mana hawakuipata,Wana maumivu ya kukosa vitu tokea udogoni, nyumbani,shuleni na huko mtaani so akifanikisha anakuwa anapooza Yale maumivu yake,Kama Kuna jirani walikuwa wanaishi maisha mazuri Basi wao hawana ndio hapo hapo akifanikisha maisha anamalizia ama anapoozea maumivu yake