Sawa tutaondoka wote, una gari?

Stanboy

JF-Expert Member
Jul 4, 2013
1,114
1,300
Wazee tafuteni hela mnunue magari,ni muhimu sana kuliko mnavyochukulia.

Siku moja niko zangu club moja hapa mji pendwa unaoongoza kwa raha za kila aina hapa Tanzania.Mara hatua kama 5 hivi nikamuona mrembo matata mwenye shepu ya kike hasa, sura yenye kuvutia na rangi ya kichaga kaketi pekee yake huku anakunywa dompo taratibu bila papara basi moyo ulipasuka vibaya kumbe si mimi tu niliyemuona kila mwanaume alikuwa anamkodolea macho alionekana ni mdada anayejielewa siyo kama wengi wa wadada wa club za hapa mjini ambao wengi wao wanaenda kudanga basi nikawa namlia timing tu, kilichonipa hofu kila mwanaume aliyeenda kukaa naye au kumsemesha wala hakumjibu kitu aliwaangalia tu mpaka walipoondoka wenyewe.

Basi Dj akagonga ngoma ya Diamond ft Fally Ipupa inama demu akasimama akaanza kucheza taratibu..dah lile shepu na kiuno chake tu balaa..midume kibao ikamfuata lakini hakukubali kucheza na mtu basi nikajisemea moyoni ngoja na mimi nimfuate nione atakataa kucheza na mimi!!kijana nikasimama nikajiangalia kwanza(offcourse am a gentleman) nilipiga jeans yangu nyeusi,tisheti nyeupe na raba nyeupe shingoni cheni kiaina na mwili wa mazoezi kwa mbali nikaanza kucheza style anayocheza yeye huku namsogelea taratibu bila uoga yaani as if tunajuana huku natabasamu yaani nafurahia wimbo mara tukakutanisha macho demu akatabasamu pia kwa wanaoujua wimbo kuna sehemu wanasema ale inamaa hebu pinda mgongoooo ile anainama tu nikashika kiunooo kiuno laini kileee mtoto ndo akaongeza kukipinda sasaa.

Basi tu shorten za story tukaendelea kucheza pale huku kila mwanaume anashangaa nimewazaje kucheza na yule yaani macho yalikuwa kwetu dada anajua kucheza na mimi najua kiasi chake..kumbe yule dada alikuwa anawasubiria rafiki zake mara wakafika wadada wawili wakajiunga na sisi pale,akanitambulisha as her new friend kijana nikawa nashika viuno vya wadada watatu kwa raha zangu nikawaongezea vinywaji pale na baadaye makange ya kuku demu naye akawa anaongezea vinywaji pale yaani hana njaa..basi siku yangu ikawa tamu kweli kweli.

To shorten the story,

Mida ya saa 9 hivi demu akaniambia kachoka hivyo wanataka wakapumzike,so anashukuru sana kwa kampani yangu ameenjoy mno!

Nikajisemea moyoni hivi namuachaje aondoke hivi hivi?nikamwambia hata mimi nimeenjoy sana,sikutegemea kama siku yangu ingekuwa tamu hivi yaani umenipa kitu sikutegemea basi akaniangalia na kutabasamu huku ananilalia begani nikamwambia hakika nimefikiria mengi kuhusu wewe natamani tukapumzike wote ili nikueleze ni yapi?demu akawa hanijibu kitu nikajua ishakula kwangu nikaendelea kuongea maneno kibao ya kutoa aibu na kupotezea mada ya kupumzika wote mara akaenda kaunta akaomba kihandbag chake akarudi akaniegemea begani na kutoa funguo za gari kwenye kile kihandbag akampa mdada mmoja kati ya wale marafiki zake na kumwambia utaenda na gari yangu nitaikuta kesho kwako halafu akawaaga marafiki zake na kuniambia twende, basi nikawaaga wale wadada kwa tabasamu zitoooo najua nishamaliza kazi...

Kabla ya kutoka mlango wa mwisho wa club akaniuliza una gari? nikajibu ndio ninalo ila nimeliacha nyumbani sijaja nalo hapa club...mdada akaniangalia kisha akaondoka kimya kimya kurudi club,nilibaki pale nikijua kwamba kafuata funguo ili tuondoke na gari lake...huwezi kuamini demu hakurudi tena pale...ukweli ni kwamba gari ninalo na nililiacha nyumbani siku hiyo maana lilikuwa na shida kidogo,roho iliniuma nikarudi club sikupata tena nguvu ya kumfuata yule mdada...iliniuma sana maana huyu demu niliwaza hata kumuoa kama mambo mengine tungematch.

Ndg zangu wanaume fanyeni kazi kwa juhudi,nunueni gari zinasaidia sana katika maisha ya kila siku...achaneni na misemo ya kuwa hakuna baba mwenye gari ila kuna baba mwenye nyumba tu...ukiwa na gari status inapanda mno kuliko mwenye nyumba japo nyumba ina thamani kubwa...hata kipindi hiki cha corona umuhimu wa gari binafsi umeonekana.

Asanteni sana.
 
Eti
Mungu alikuepusha Jambo kwa huyo mdada ..ulikuwa umeporwe gari na maiti yako kukutwa chini ya daraja...
Don't regret kumkosa huyo mdada...shukuru..
eehhh?kivipi sasa? Wakati tulikuwa tunaenda kwangu?
 
Mmmh shukuru mungu ulikiacha kigari chako nyumbani, hiyo gari ingepigwa siku hiyo, huyo demu ni mwizi wa magari 😂😂😂
Kivipi sasa mkuu wakati tulikuwa tunaenda kwangu?
 
hapo gari ingekusaidia kuondoka na pisi..
Lakini wewe unatuambia tu inasaidia kwenye maisha
Maisha ni demu tu?

Nb: kuwa na gari ni muhimu.
Nimejaribu tu kuhusanisha mkuu
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom