Mods Uzi huu uachwe ujitegemee tafadhari.🫷
Awali ya yote Mimi mpango wa kwenda mbinguni ni kama haupo maana kila nikipiga tathimini Bado najiona Sina sifa hizo
Kwanza Zaka sitoi,sadaka nishakataa kuipeleka kanisani.
Ukija namna ya kuishi napo Bado na pwaya maana uko zako unawaza kuchuma nyanya zako mara mdada kaumbika anapita mbele yako Tyr hapo natamani (naingia dhambini) so kwa kifupi yapo mengi na mengi ambayo nikijifanyia tathimini najiona Bado sitatoboa kuingia yerusalemu mpya.
Sasa mtuambie ninyi watakatifu mtakao Uingia mji ule!.......
Ikiwa tu hapa Duniani tunapopoteza wapendwa wetu huwa tunakuwa na msongo wa mawazo wengine huzimia na wengine hujihisi upweke usio Isha.
Wengine Bado hadi Leo hawajapona mioyo Yao baada kuondokewa Baba,mama ndg na jamaa zao
Vipi wewe mtakatifu wa Bwana utakuwa na furaha Gani iwapo familia yako yote itachomwa moto ?
Mke/mme na watoto pamoja na wazazi wako wadogo zako na wakubwa zote wamechomwa moto utakuwa na furaha Gani?
Kama mtaishi kwa raha huku watoto wenu wanachomwa moto huko jehanamu sasa sijui akili yenu itakuwaje vile.
View attachment 3541708