Haaaaaa haaaaaa!!!! We jamaa kweli shenene unajificha kichwa wakati mkia unaonekana kujihami kwako kumeweka wazi wewe ni SHIA MKUU.
Kama kuuchukia utawala wa Saudiya ni kuwa Mshia haya.
Haya ndiyo matango pori mnayolishwa kuhusu Saudi Arabia kwamba yeyote atakayekuwa against na utawala wao basi ni Mshia. Shia wana shahada tatu mi nina shahada 2 tu. Shia wanaamini Qur'an haijakamilika mimi kwangu ni " laa rayba fiyyyh" Shia wana "taqiyya" na kusema uongo. Sunni wal Jamaa tupo nayo mbali hayo. Shia muanzilishi wa hayo madh' hebu ni Abdillah ibn Saaba. Ni myahudi huyu aliyesilimu kinafiki kwa Mtume na Mtume alifahamu kwamba alisilimu kinafiki.
Saudi arabia was formed by Ibn Abdul Wahhabi na Ibn Saudi alliance. Wakaibadili Najid na kuwa Ufalme wa Saudi Arabia(rejelea ahadith ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake inayohusu mtu wa Syria, Yaman na Najid waliyohitaji Dua kwa ajili ya miji yao. Rejelea Mtume alisema kwa kumuambia nini mtu wa Najid). Kwanza hamna kitu kinachoitwa Kingship katika Dini ya Kiislam. Hii wamelitoa wapi? Kama siyo bidaa? Na nioneshe ni wapi katika Uislam uongozi wa Kiislam unaruhusu madaraka ya Kifamilia ndiyo itawale milele kama Saudi Arabia? Umesahau wa Yemen walipokwenda kuhiji Makkah na kuchukua maji ya Zamzam, unajua mamlaka ya Saudi Arabia iliwaambiaje? Ili waambia wayalipie kutumia maji ya Zamzam wakati maji ya Zamzam ni bure na ni kisima kisichokauka kwa rehma zake Mungu. Mahujjaj Wayemen wakakataa kuyalipia, unajua kilichofuata ni nini? Waliamuriwa na Mamlaka ya Saudiya maji yote ya Zamzam wayamwage chini na yalimwaga ki lazima.
Sasa akitokea Muislam ambaye anayakemea mambo maovu yanayofanywa na Utawala wa Saudiya wanajitokeza miongoni mwa Waislam na wanawathubutukia kuwita Mashia. Ukitizama kisa ni nini(?) Eti ni kusemea maovu ya tawala ya Saudiya.
Tuje kwenye Mali wanazomiliki, zote zimetokana na Mali ya nchi waliyokalia. Kwenye "Aamu rramadah" Ukhalifa wa Umar radhi za Allah ziwe juu yake, mkewe Umar alikuwa anahamu na haluwa. Umar hakuwa na uwezo wa kumpatia haluwa kwa kipindi hicho. Mke wake akamwambia basi kopa katika hazina ya "baytul maal" halafu baadaye atarudisha. Yeye Umar si ndiyo kiongozi kwa wakati wake na Mali zote za Waislam zipo chini yake. Unajua alimjibu nini mkewe? Alimwambia Waislmu ndiyo wenye haqi zaiiiidi kuliko yeye. Yeye ni msimamizi. Turudi kwa Dola ya Saudiya, nchi yao ina utajiri mkubwa sana wa mafuta na mtawala anasema anaongoza kwa mila ya Kiislam, kama hiyo ni hoja ina maana mali zote za nchi wenye mamlaka nazo zaiidi ni Waislam. Swali juu yako. Kwa nini mali zote za nchi utawala wa Saudiya ndizo unamiliki? Familia yao una utajiri mkubwa sana na yote ni utajiri wa nchi yote wameupora wao. Uislam umeweka utaratibu wa Dola kuweza kujiendesha na kusimamia Mali za Dola yenyewe na mfano Mzuri ni hapo juu wa Sahaba ya Mtume Umar r.a. Niambie familia ya kifalme Saudi Arabia mamlaka ya kumiliki mali zote za nchi na huo utajiri wamepatiwa wapi hali ya kuwa nchi inaongozwa Kidini?
Hayo yote ya juu hapo wakijitokeza Waislam wakiyasema wanakuja akina ninyi na mnathubutu kuwaita Mashia.
Ni nani aliyeufanya utawala wa Saudiya kwenye hilo jangwa kama siyo Mbritish? Na baada ya Mbritish kuanguka anayemlimda ni Marekani. Dola inayodai ya Kiislam ina lindwa na Dhalimu Mmarekani(?!) Hili nalo hamlioni? Tangu lini baatwil ikawa juu ya haqi? Haya nayo hamyaoni?
Dhehebu la Salafi/Wahhabi/Ansar Sunnah( majina yote hayo ni ya dhehebu moja tu) % 90+ ni watiifu sana kwa Utawala wa Saudiya na hii haijaja kwa bahti mbaya. Rejelea muasisi wa hayo madh' hebu na muasisi wa taifa la Saudiya.