Sasa ni rasmi, TAMISEMI imemshinda Bashungwa, imebidi Waziri Mkuu aingilie kati, ndio wizara yenye kelele za uozo

Bashungwa anafanya kazi nzuri ya ufuatiliaji miradi, ila kashindwa kuwa mkali na kutumbua wapigaji! tulisema tangu mwanzo namna ya kudeal na watumishi wapigaji etc ni kutumia zile mbinu za mwendazake, kutumbua, kuweka ndani ,kufilisi au kupanda pale kisutu na lile shitaka pendwa ,short of that watu wataendelea kuchezea pesa ya Mama.
 
Bashungwa atolewe kabisa, hata michezo alipokuwa Waziri alifeli.

Anafaa kuwa askofu au Mzee wa kanisa
🤣🤣🤣🤣🤣 Tanzania sihami Mimi ata mchele uwe 10000 kwa kilo,nihame niende wapi nikafe bure na stress!
 
tuko awamu ya waswahili, mambo za kuchapa kazi za nini sasa? kusafiri na hotuba za kila siku ndio mpango mzima
 
Tatizo tulilonalo ktk awamu hii hatuna wabunge wa maana mpk Rais anakosa wa kumteua. Magufuli ametuletea wabunge wasio na uwezo wengi wao. TAMISEMI inahitaji aina ya watu km Unny Mwalimu, Selemani Jafo, Mchengerwa angalau, labda Jumaa Awesso. Hv km mpk ktu km Ashatu Kijaji ni waziri unategemea nini. Rais naye aache kuendekeza udini aangalie wachapakazi. Dini ibaki msikitini.
Mbunge gani alikuwa wa maana ambae aliachwa na Magufuli?

Ummy, jafo, mchengerwa walikuwa hapo Tamisemi Ila mama Samia aliwatoa. Unahisi aliwaonea?
 
Mbona Jafo aliweza na aliibua madudu mwenyewe

Hata bashungwa ameibua madudu tofauti Yao ni uwasilishaji Tu Kwa jamii

Umewahi kusikia madudu yakiibuliwa na Mzee Mwanri? Yule alikuwa RC tabora?
 
Kwa utendaji wa Bashungwa tulisema wizara ile haiwezi, TAMISEMI inataka mtu wa purukushani leo huku kesho kule na asimamie miradi kwa karibu sana
Duh, kwa hiyo waziri awe anazurura nchi nzima kama Jafo NA kiki za waandishi wa habari full kufoka?

Shida ni mfumo mbovu wa hii nchi mfano ripoti za CAG hazifanyiwi KAZI, wakaguzi wa ndani wapo kama vivuli, DSOs wapo ila wakurugenzi wanaiba wanavyotaka, TAKUKURU hadi wapewe amri NA mkuu wa wilaya au RC ndio wafanye KAZI.

Nchi iuzwe tu tugawane hela kila MTU apite hivi.
 
Hauogopi kudhulumiwa gawio lako baada ya hayo mauzo ?
 
Bashungwa, Waziri kijana, ambaye ilitarajiwa "damu iwe inachemka" awe anapanda na kushuka,anakaba huku na kule, ameonekana Mzee kuliko Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anaenda Arusha, anaenda Singida, anajua mambo ambayo alitakiwa Bashungwa awe ameshayajua na kuchukua hatua....hamna kitu.

Alikuwa na Rais Mkoa wa Mara, hakuna hatua iliyochukuliwa.

Hii wizara ndio injini ya nchi, ndiyo inamgusa mwananchi, na ndio mishipa ya damu ya nchi, mirija ya kufikisha huduma kwa mwananchi ni kupitia Tamisemi.

Nadhani kwa Sasa Bashungwa apumzike, Rais afanye scouting ya mtu ambaye hatacheka na kima.

Waziri wa Tamisemi anatakiwa awe more than active.

Ila ombi letu Bashe asitolewe kilimo. Binafsi naona Mchengerwa atamudu kukabana na hawa jamaa wa Tamisemi
Tukiacha ukabila na udini hii wizara apewe Kalemani jamaa ni mfuatiliaji mzuri sn
 
Tatizo tulilonalo ktk awamu hii hatuna wabunge wa maana mpk Rais anakosa wa kumteua. Magufuli ametuletea wabunge wasio na uwezo wengi wao. TAMISEMI inahitaji aina ya watu km Unny Mwalimu, Selemani Jafo, Mchengerwa angalau, labda Jumaa Awesso. Hv km mpk ktu km Ashatu Kijaji ni waziri unategemea nini. Rais naye aache kuendekeza udini aangalie wachapakazi. Dini ibaki msikitini.
Udini unamtesa sn
 
Bashungwa, Waziri kijana, ambaye ilitarajiwa "damu iwe inachemka" awe anapanda na kushuka,anakaba huku na kule, ameonekana Mzee kuliko Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anaenda Arusha, anaenda Singida, anajua mambo ambayo alitakiwa Bashungwa awe ameshayajua na kuchukua hatua....hamna kitu.

Alikuwa na Rais Mkoa wa Mara, hakuna hatua iliyochukuliwa.

Hii wizara ndio injini ya nchi, ndiyo inamgusa mwananchi, na ndio mishipa ya damu ya nchi, mirija ya kufikisha huduma kwa mwananchi ni kupitia Tamisemi.

Nadhani kwa Sasa Bashungwa apumzike, Rais afanye scouting ya mtu ambaye hatacheka na kima.

Waziri wa Tamisemi anatakiwa awe more than active.

Ila ombi letu Bashe asitolewe kilimo. Binafsi naona Mchengerwa atamudu kukabana na hawa jamaa wa Tamisemi
Sawa kama ndio maoni yako ila yapo kama una mambo nae personal sijaona tatizo kwamba ulitaka waziri mkuu akae!

Bashungwa kama unamfuatilia vizuri kila siku yupo na hekaheka anatatua changamoto nyingi tu kila siku

Ila maoni yangu hii wizara ni kubwa sana ndio maana akapewa kutokana utendaji lakini bado hatoshi labda ndio maana na waziri mkuu anasaidia kwasababu inagusa maslahi mapana ya nchi

Labda tujiulize sasa kwanini waziri mkuu baadhi ya mambo amekua wa kwanza kuona au kufuatilia? Mimi na wewe hatujui kwanini ila tunaweza kufikiri tu kawaida waziri mkuu ndio anayesimamia shughuli zote za serikali kwahiyo basi Bashungwa yeye kaja kamkuta huenda tayari waziri taarifa anazo kabla hata hajafika Bashungwa kinachotokea waziri mkuu anaendelea na mipango yake ya kazi kama kawaida lakini pia anamtuma Bashungwa

NB: Kazi ya waziri mkuu NI kuwatuma na kusimamia mawaziri wote katika shughuli zote za serikali.

Kwahiyo USIPOTOSHE !
 
Bashungwa, Waziri kijana, ambaye ilitarajiwa "damu iwe inachemka" awe anapanda na kushuka,anakaba huku na kule, ameonekana Mzee kuliko Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anaenda Arusha, anaenda Singida, anajua mambo ambayo alitakiwa Bashungwa awe ameshayajua na kuchukua hatua....hamna kitu.

Alikuwa na Rais Mkoa wa Mara, hakuna hatua iliyochukuliwa.

Hii wizara ndio injini ya nchi, ndiyo inamgusa mwananchi, na ndio mishipa ya damu ya nchi, mirija ya kufikisha huduma kwa mwananchi ni kupitia Tamisemi.

Nadhani kwa Sasa Bashungwa apumzike, Rais afanye scouting ya mtu ambaye hatacheka na kima.

Waziri wa Tamisemi anatakiwa awe more than active.

Ila ombi letu Bashe asitolewe kilimo. Binafsi naona Mchengerwa atamudu kukabana na hawa jamaa wa Tamisemi
Huu ni udhaifu katika mfumo wa uongozi. Sio kazi ya,waziri mkuu wala waziri tamisemi kutembelea mikoa au wikaya au mashirika ya umma kutoa maagizo. Tumeweka mfumo wa Kiki za kisiasa badala ya mfumo wa uongozi. Unavizia kusikia udhaifu na mara nyingine majungu tu then unakimbia huko na msululu wa waandishi as if hakuna wahusika. Tuwape wahusika au wataalam uhuru wa kufanyakazi sio MaRC, DC, Mawaziri kufanyakazi za wataalam. Kama mtaalam hawezi athlete na siyo maigizo ya kisiasa. Wao ni wasimamizi wa sera na,wawezeshaji wa wataalam.
 
Back
Top Bottom