Tatizo ni kwamba hata hawa wanaopinga jpm kwenda kupumzika kwao ni wale ambao hawana utamaduni wa kwenda kutembelea ndugu zao huko vijijini walikotoka. Mtu ana uwezo lakini anakaa Dar miaka 15 hajawahi kwenda kwao kusalimia kisa yupo Dar utadhani kwao dar kumbe ni wa kuja tu kwao hukoooo! Hata marais wa Marekani na nchi nyingine zilizoendelea rais kwenda kwao kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu hasa za kidini pamoja na mwaka mpya ni jambo la kawaida sana. Hata Nyerere mwenyewe alikuwa anakwenda kwao butuama mara kwa mara kupumzika pale alipokuwa anapata nafasi ya kufanya hivyo. Mzee wa msoga ndio usiseme mara nyingi tu alikuwa anazuka msoga kusalimia. MBONA JAMBO LA KAWAIDA SANA SISI MIAFRIKA BWANA NDIO MAANA TUNAZIDI KUWA MASKINI KWA SABABU YA ROHO MBAYA NA CHUKI ZISIZO NA SABABU!