Sasa Lema, Nassari na CHADEMA wataamka?

Sasa Lema, Nassari na CHADEMA wataamka?

Kuna kitu kinanishangaza sana kuhusu CHADEMA, bado hawaamini kuwa uhuni wanaofanyiwa unatokea mbali zaidi ya polisi, zaidi ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa. Nilikuwa nikiwasikiliza Lema na Nassari walivyokuwa wakidai watampelekea mh. Rais ushahidi wa madiwani kuhongwa nikasikia kichefuchefu!

Nafikiri nilisema mahali ninyi toeni huo ushahidi, in public, sasa baada ya kubezwa na TAKUKURU na Mnyeti kupewa ukuu wa mkoa, kupandishwa, nadhani akili itawajia. Maana walichokuwa wakikifanya ni kumtumia mtu ujumbe kuwa, "The magic of fear is working"

Na kama hawatakuwa na mkakati wa pamoja wa kujua namna ya kupambana kisiasa very forcefully, 2020 wakibakizwa wabunge 5 wa CHADEMA niiteni mbwa!

Why I say so!

1) Kama mwenzenu anapigwa risasi mchana kweupe, reaction inakuwa ni unyonge, ukishinda ubunge wakamtangaza mwingine utafanyaje?

2) Kama Kigaila anakamatwa na polisi kwa kuhoji kwanini Makonda anazunguka na wenye bunduki reaction yenu inakuwa hii, mkinyang'anywa ubunge mtaweza kufanya nini?

3) Kama mtu bustani zako zinaharibuwa unalia lia unajibu uhuni kwa sheria ukinyang'anywa ubunge hata kama umeshinda kwa asilimia 90% utafanyaje!

4) Hivi neno, " Jecha apewe tuzo" linaashiria nini kwenu?

5) Hivi pamoja na kuonyesha wazi Mnyeti alihusika kuhonga madiwani na bado akapandishwa cheo inaashiria nini kwenu!

Endeleeni kulia goodluck, pengine mtaonewa huruma! Guys mnachokifanya ni kutuma ujumbe kuwa hata mfanyiwe nini hamwezi fanya lolote, "And the envelopes will be pushed real far in 2020 by the look of things"

Halafu acheni madharau!
Naona mantiki ya hoja yako. Nilijiuliza sana wakati wa uteuzi wa wakurugenzi mbalimbali akiwepo aliyekuwa wa Kilombero ambaye alihamishiwa Bagamoyo. Pindi ushindi wa kesi ya uchaguzi ulipotoka na kumpa ushindi mgombea wa upinzani, yule mkurugenzi alitumbuliwa!! Wengi wa wakurugenzi walichauliwa kutokana na wanachama wa ccm, na kwa mwendo huu wa kuwapandisha vyeo wale wanaodaiwa kuchezea rafu wapinzani, haitii shaka hata kidogo kuwa hawa wateule hawatakuwa tayari kumkwaza muajiri wao kwa vyovyote. Wasiwasi wangu, ni kama tukienda na mdundo huu hadi 2020 (hakuna dalili ya kubadilika), ni wazi kuwa wakurugenzi wote watawatangaza wabunge wote na madiwani wote wa ccm kuwa ndio washindi (hii iwe kwa kuagizwa au kutokuagizwa).

Hivyo nadhani ni vyema kuanza kutafuta uwanja wa kupata muafaka wa kitaifa katika hili kabla ya kufika huko kwani inaweza kuzorotesha utengamano wa Watanzania.
 
Kuna kitu kinanishangaza sana kuhusu CHADEMA, bado hawaamini kuwa uhuni wanaofanyiwa unatokea mbali zaidi ya polisi, zaidi ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa. Nilikuwa nikiwasikiliza Lema na Nassari walivyokuwa wakidai watampelekea mh. Rais ushahidi wa madiwani kuhongwa nikasikia kichefuchefu!

Nafikiri nilisema mahali ninyi toeni huo ushahidi, in public, sasa baada ya kubezwa na TAKUKURU na Mnyeti kupewa ukuu wa mkoa, kupandishwa, nadhani akili itawajia. Maana walichokuwa wakikifanya ni kumtumia mtu ujumbe kuwa, "The magic of fear is working"

Na kama hawatakuwa na mkakati wa pamoja wa kujua namna ya kupambana kisiasa very forcefully, 2020 wakibakizwa wabunge 5 wa CHADEMA niiteni mbwa!

Why I say so!

1) Kama mwenzenu anapigwa risasi mchana kweupe, reaction inakuwa ni unyonge, ukishinda ubunge wakamtangaza mwingine utafanyaje?

2) Kama Kigaila anakamatwa na polisi kwa kuhoji kwanini Makonda anazunguka na wenye bunduki reaction yenu inakuwa hii, mkinyang'anywa ubunge mtaweza kufanya nini?

3) Kama mtu bustani zako zinaharibuwa unalia lia unajibu uhuni kwa sheria ukinyang'anywa ubunge hata kama umeshinda kwa asilimia 90% utafanyaje!

4) Hivi neno, " Jecha apewe tuzo" linaashiria nini kwenu?

5) Hivi pamoja na kuonyesha wazi Mnyeti alihusika kuhonga madiwani na bado akapandishwa cheo inaashiria nini kwenu!

Endeleeni kulia goodluck, pengine mtaonewa huruma! Guys mnachokifanya ni kutuma ujumbe kuwa hata mfanyiwe nini hamwezi fanya lolote, "And the envelopes will be pushed real far in 2020 by the look of things"

Halafu acheni madharau!

Chifu, nimeshawahi kuwashauri CHADEMA humu kwamba wameshafanya kazi ya kutosha. Wanachopaswa kufanya sasa ni kuwa kwenye cruise control mode tu! Wa-ride along liCCM na maCCM, wahakikishe mifuko yao imetuna, then basi. Maana wanapoteza nguvu na muda wao kuwapigania watu ambao hawawezi kuamka! Kwanini unataka wahatarishe maisha yao au pengine kuuawa kwa ajili ya watu walio wafu tayari?

Mimi siwezi kuwalaumu CHADEMA hata punje. Yaani kama bado watanzania hawaelewi na hawaamki toka amsha amsha za Mzee Slaa hadi leo hii za Lissu, hakika hakuna namna wanaweza kuamka. Jambo zuri ni kuachana nao tu.

Kama kuna mhusika wa CHADEMA ananisoma humu, huo ndiyo ushauri wangu. Kaeni kimya tu, pigeni pesa, na hacheni CCM itunyooshe vizuri watanzania. Siku tutakapoelewa, ndipo tutaelewa nini CHADEMA wamekuwa wakifanya.
 
Sikh watapokuwa wasomi wengi ndiyo itafahamika pumba na mchele in upi
 
Kweli tupu.. Ifike mahali sasa Chadema wawe wana react fiercely..!!

Na sio ku-react kwa kuitisha press conference..

Enough is enough..

Hawa watawala wapo tayari hata kupoteza uhai wa mtu ili watawale tu..

Chadema ibadili mkakati sasa..

Aggressiveness is needed now.
Machadema mnataka kutawala nini,na kwanini mnalazimisha mtawale nyie?
 
Chifu, nimeshawahi kuwashauri CHADEMA humu kwamba wameshafanya kazi ya kutosha. Wanachopaswa kufanya sasa ni kuwa kwenye cruise control mode tu! Wa-ride along liCCM na maCCM, wahakikishe mifuko yao imetuna, then basi. Maana wanapoteza nguvu na muda wao kuwapigania watu ambao hawawezi kuamka! Kwanini unataka wahatarishe maisha yao au pengine kuuawa kwa ajili ya watu walio wafu tayari?

Mimi siwezi kuwalaumu CHADEMA hata punje. Yaani kama bado watanzania hawaelewi na hawaamki toka amsha amsha za Mzee Slaa hadi leo hii za Lissu, hakika hakuna namna wanaweza kuamka. Jambo zuri ni kuachana nao tu.

Kama kuna mhusika wa CHADEMA ananisoma humu, huo ndiyo ushauri wangu. Kaeni kimya tu, pigeni pesa, na hacheni CCM itunyooshe vizuri watanzania. Siku tutakapoelewa, ndipo tutaelewa nini CHADEMA wamekuwa wakifanya.
Natamani turejee wote ca ch ma ili tuone minyukano na watanzania ndo labda tutaamka na kuona uzuri wa upinzani
waache unyonge na kutegemea huruma ya hawa mbwa
 
The great question of the day shall not be solved by majority resolution peaceful and dialogue but by using blood and iron

Watasubiri sana huruma kila siku chama kimelaani kimelaani mwisho mtaanza kutalaani wanachama wenu sasa

Chadema mmeanza kuniboa ngoja tusubiri command wetu Lissu
 
Time will tell mtoa mada...mamb mazur hayaitaji haraka haraka
 
Ninaunga mkono hoja 100%... Upinzani wanatakiwa kubadilisha mikakati, na Mbunge Nasiri aonde mashitaka takukuru ile kesi haina maana
 
Kweli TL. Marandu, kama opponent wako yuko tayari kuua huyo sio wa kumwendea kwa matamko, Chadema wanatakiwa kuwaonyesha advertise moja ambayo hawatasahau kiasi kwamba kila wakitaka kufanya hujuma lazima wajiulize mara mbili mbili, mtu anapigwa risasi mnajibu kwa press conference kweli?

Kuna haja ya CHADEMA kubadilika kuendana na hali halisi
Unanikumbusha yule Shehe wa Mwanza marehemu ........
 
AKILI ZA WATANZANIA WENGI ZIMEDUMAA

KWANI MATESO YA KIUONGOZI WANAYAPATA CDM

WAHANGA NI WANANCHI WOTE

MI NADHANI KWA KUNASHIDA NA MATESO BASI YAONGEZEKE MARA DUFU MPAKA AKILI ZITUKAE SAWA NDIPO KILA MTU ATAFANYA MAAMUZI YAKE

MAMBO YA KULAUMIANA HAYANA HAJA

CCM NA CDM WOTE NI WATAFUTAJI KAMA WATAFUTAJI WENGINE
 
kwa mawazo yako ina maana watu wako tayari kupoteza hata robotatu ya watanzania ili mradi wakae madarakani?
 
Andamana tuone,miaka miwili sasa no maandamano hi awamu nyingine mkuu
Hayo maandamano tuombe tu yasitokee maana simuoni aliye salama
Nilishangaa majuzi kampuni ya matairi iliungua, zilikuja zimamoto toka kila kona ya Dar hazikufanikiwa. Nikajiuliza hivi likitokea la kutokea watu wanawasha moto kila kona ya nchi nani atakayezuia.
Naomba hayo yasitokee.
 
Back
Top Bottom