Kuna weza kukawa na mazingira fulani ya kufanana kwa hali ilivyokuwa Libya na Tanzania. Lakini hakuna mfanano wowote ule kati walubya na watanzania.
Kuna mifananisho ilitolewa miaka ya nyuma juu watanzania na hiyo mifanano ndiyo umewakaa na kuwagandeni kama laana.
Ule msemo kwamba Jomo Kenyatta aliwahi kumwambia Nyerere kuwa yeye anaongoza wagonjwa lakini Nyerere anaongoza maiti.
Mbili, ule msemo wa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwamba Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu. Hizo laana hazitakuja kuwatoka na matokeo yake mtakuja kuchagua hadi wendawazimu ili wawaongoze.
Zaidi katika mazingira ya sasa hakuna kijana wa kitanzania anateweza akafanya vurugu. Sababu ni Kwanza, kila kijana ana account kwenye social media, pili kila mmija ana miliki simu yenye camera, tatu kila mmija anataka kuwa reporter sasa hapo utampata nani? Kuna siku nadhani ni mwezi wa August or July nilifika hapo 'Small Fishing Village', nikaona vijana kama 8 au 10 wa CHADEMA wanaandamana kutoka maeneo ya Ubungo nadhani wakipitia Manzese na Magomeni ili kwenda Kinondoni. Waandamanaji walikua nane au kumi tu huku mvua ikinyesha, lakini waliosimama pembeni ya barabara, majumbani na pembeni ya biashara zao na kwenye magari kushuhudia tukio lile nadhani walikua ni zaidi ya 13,000 kwa uchache na nina uhakika waliolipiga picha tukio lile kwa simu zao ni zaidi ya watu 700.
Hebu fikiria vizuri unapojaribu kutegemea mabadiriko kwa watu na jamii ya aina hii. Watanzania mjikubali tu mlivyoumbwa kwamba mliumbwa hivyo hivyo mlivyo.
Yanayotokea yataendelea kutokea mpaka nature itakapoamua kuyabadirisha, wala siyo ninyi kupitia masanduku ya kura wala bunge wala maandamano.
Amkeni mkuu.