Sasa Lema, Nassari na CHADEMA wataamka?

Sasa Lema, Nassari na CHADEMA wataamka?

Chadema hawana smg sasa wafanyeje?

kuonyesha hisia zako na dola ikajua ni nini mnahitaji hakuhitaji SMG, silaha ni watu na ukiwa unawatu wakutosha ni silaha tosha kufikisha hisia zako kwa dunia... kwa hali hii sioni future ya CDM..
 
Kuna kitu kinanishangaza sana kuhusu CHADEMA, bado hawaamini kuwa uhuni wanaofanyiwa unatokea mbali zaidi ya polisi, zaidi ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa. Nilikuwa nikiwasikiliza Lema na Nassari walivyokuwa wakidai watampelekea mh. Rais ushahidi wa madiwani kuhongwa nikasikia kichefuchefu!

Nafikiri nilisema mahali ninyi toeni huo ushahidi, in public, sasa baada ya kubezwa na TAKUKURU na Mnyeti kupewa ukuu wa mkoa, kupandishwa, nadhani akili itawajia. Maana walichokuwa wakikifanya ni kumtumia mtu ujumbe kuwa, "The magic of fear is working"

Na kama hawatakuwa na mkakati wa pamoja wa kujua namna ya kupambana kisiasa very forcefully, 2020 wakibakizwa wabunge 5 wa CHADEMA niiteni mbwa!

Why I say so!

1) Kama mwenzenu anapigwa risasi mchana kweupe, reaction inakuwa ni unyonge, ukishinda ubunge wakamtangaza mwingine utafanyaje?

2) Kama Kigaila anakamatwa na polisi kwa kuhoji kwanini Makonda anazunguka na wenye bunduki reaction yenu inakuwa hii, mkinyang'anywa ubunge mtaweza kufanya nini?

3) Kama mtu bustani zako zinaharibuwa unalia lia unajibu uhuni kwa sheria ukinyang'anywa ubunge hata kama umeshinda kwa asilimia 90% utafanyaje!

4) Hivi neno, " Jecha apewe tuzo" linaashiria nini kwenu?

5) Hivi pamoja na kuonyesha wazi Mnyeti alihusika kuhonga madiwani na bado akapandishwa cheo inaashiria nini kwenu!

Endeleeni kulia goodluck, pengine mtaonewa huruma! Guys mnachokifanya ni kutuma ujumbe kuwa hata mfanyiwe nini hamwezi fanya lolote, "And the envelopes will be pushed real far in 2020 by the look of things"

Halafu acheni madharau!
Ukweli Lema, Nasari na CHADEMA kwa ujumla wamefanya sehemu yao ya kazi. Na wameifanya kwa ustadi mwingi kuliko ilivyofikiriwa. But wamevuna kejeli. Ni kweli kabisa hata uchaguzi ujao wanaweza wasishinde due to mazingira but wamefanya kazi yao vizuri. Kazi ya mwanafunzi ni kusoma kwa bidii na kujibu maswali kwa ufasaha, lakini kufaulu inategemea mazingira. Kama Yesu alivuna kejeli, kama Mtume alivuna kejeli lakini leo karibu watu wote duniani wanaishi kufuata mafundisho yao, kuna shida gani kwa Mwanadamu kama Lema na Nasari kukejeliwa, kudhihakiwa nk?
 
Siku hizi ninao ujasiri wa kusema hadharani kuwa Tanzania HAKUNA WAPINZANI!! Yupo mmoja tu ambaye kwa sasa ni magonjwa, wengine wote ni watafutaji tu kama walivyowatafutaji wengine!
 
TL asante kwa mada nzuri.

Upinzani Tanzania (UKAWA, CHADEMA, CUF...) una tabia 2 ambazo zote ni mbaya.

1) Upinzani umekuwa wa kujilinda zaidi na sio kushambulia (offensive) kwa mada na hoja nzito nzito (defensive and reactive model).

2) Upinzani umekuwa passive and opportunistic (ndio kudhaniwa kuwa ni wa matukio au msimu).

Lazima Upinzani wawe na agenda zao, zijulikane, ambazo wataziuza kwa wananchi muda wote na kwa kutumia njia zote (hata kama mikutano ya siasa imezuiwa mpaka 2020). Kuonyesha tu maovu, madhaifu na makosa ya CCM bila ya ninyi kuonyesha ubora, uimara na uwezo wenu sio kushika dola. Pia ni lazima muwe na hoja, sera, itikadi, mawazo na uwezo wa kuonyesha kwamba ninyi mtakuwa chaguo bora kuliko walioko madarakani.

Halafu lazima muwe na mkakati uliogawanyika (segmented) kwa vipindi na maeneo. Kwa mfano:- Je mnataka wenyeviti wa mitaa/vijiji au madiwani au wabunge wangapi 2019/20? Mnapaswa kujua bayana kuwa kabla ya kuzungumzia Urais ni kada hizo mbili ndio zitakazobeba (mhimili) wa kampeni na kufanikisha lengo kuu (Urais).

Niliwahi kuandika mahali, miezi ya nyuma, kuwa CCM na mwenyekiti wao waliwaagiza viongozi wao kupitia Serikali za Mitaa (madiwani wao, wenyeviti nk) kuwa wahakikishe wanakuwa na mabalozi kwa idadi fulani (10, 20, 30 nk) kwa kila kijiji. Hata mahali pengine ambapo mwenyekiti na serikali ya mtaa ni upinzani lakni bado kwa kutumia nguvu huo mkakati ulitekelezwa. Kilichofanyika ni "mabalozi wa nyumba kumi" kupachikwa kinyamela na kuzua migogoro kwenye baadhi ya mitaa lakini hatimaye wakafanikiwa kwa vile ulikuwa ni mkakati wa chama toka juu, na kwa sehemu kubwa wamefanikiwa. Kuna mahali hata Polisi, Wakurugenzi DEDs, Wakuu wa Wilaya DCs walitumika lakini walimaanisha na kupata walichotaka (ruthlessly).

Huwezi kujenga siasa na ushawishi wa kura hewani. Pia ni makosa kuujenga kwenye ngazi fulani mfano Wilayani au Kata, jengeni na jikiteni vijijini. Mkifika (na mnatakiwa muwe mnafika mara kwa mara huko) vijijini mtajua kwa makundi aina za wapiga kura na kile wanachokitaka. Mtakuwa na majibu sahihi kwa maswali sahihi badala ya jibu moja kwa maswali mengi. Kadiri ulivyo na mtandao mpana mashinani (kule chini kabisa vijijini) ndio uimara na uhakika wako wa ushindi kwenye nafasi za juu (udiwani, ubunge na urais) unavyopatikana.

Nimalizie hivi; agenda kama ufisadi na rushwa ni nzuri lakini hazijitoshelezi (inadequate and unappealing in all weather). Lakini agenda kama za afya, elimu, makazi, usalama, haki, ardhi (kilimo na ufugaji), maji, uvuvi na zenye kufanana na hizi ndio mzibebe mbele. Muziweke kwenye lugha rahisi na iliyozoeleka kwa walengwa.

Badilisheni mbinu na matendo yenu ili mpata matokeo mazuri na bora kwenye chaguzi.
 
Hii message ina ukweli mchungu ndani yake.Ni kweli pasipo kufanya namna nyingine basi kuna uwezekano mkubwa 2020 wa kuporwa ushindi asipatikane hata diwani wala mbunge yeyote toka CDM.Uongozi wa CDM taifa litazameni hili jambo kwa umakini wa hali ya juu saana.
Kuna mtu kajipanga kukimaliza chama (CDM) kwa njia zote haramu na halali.
 
Kuna kitu kinanishangaza sana kuhusu CHADEMA, bado hawaamini kuwa uhuni wanaofanyiwa unatokea mbali zaidi ya polisi, zaidi ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa. Nilikuwa nikiwasikiliza Lema na Nassari walivyokuwa wakidai watampelekea mh. Rais ushahidi wa madiwani kuhongwa nikasikia kichefuchefu!

Nafikiri nilisema mahali ninyi toeni huo ushahidi, in public, sasa baada ya kubezwa na TAKUKURU na Mnyeti kupewa ukuu wa mkoa, kupandishwa, nadhani akili itawajia. Maana walichokuwa wakikifanya ni kumtumia mtu ujumbe kuwa, "The magic of fear is working"

Na kama hawatakuwa na mkakati wa pamoja wa kujua namna ya kupambana kisiasa very forcefully, 2020 wakibakizwa wabunge 5 wa CHADEMA niiteni mbwa!

Why I say so!

1) Kama mwenzenu anapigwa risasi mchana kweupe, reaction inakuwa ni unyonge, ukishinda ubunge wakamtangaza mwingine utafanyaje?

2) Kama Kigaila anakamatwa na polisi kwa kuhoji kwanini Makonda anazunguka na wenye bunduki reaction yenu inakuwa hii, mkinyang'anywa ubunge mtaweza kufanya nini?

3) Kama mtu bustani zako zinaharibuwa unalia lia unajibu uhuni kwa sheria ukinyang'anywa ubunge hata kama umeshinda kwa asilimia 90% utafanyaje!

4) Hivi neno, " Jecha apewe tuzo" linaashiria nini kwenu?

5) Hivi pamoja na kuonyesha wazi Mnyeti alihusika kuhonga madiwani na bado akapandishwa cheo inaashiria nini kwenu!

Endeleeni kulia goodluck, pengine mtaonewa huruma! Guys mnachokifanya ni kutuma ujumbe kuwa hata mfanyiwe nini hamwezi fanya lolote, "And the envelopes will be pushed real far in 2020 by the look of things"

Halafu acheni madharau!
mkuu, I can't put it any better!

UKAWA wakiendelea kusubiria huruma watasubiri sana hadi siku ya kiama!
 
Umeandika vizuri, tena sana, sasa wafanyeje? If it were you, what would you have done in a forceful way? Resistance ya ndani ni ngumu. sisi tuliwahi shuhudia Idd Amin, tunajua ugumu wa unachokiongea.
Upinzani umejaa watu wenye maneno kama wewe ndio maana haufiki popote. Hata bila kufanya vurugu bado wangeweza kutumia akili zao vizuri zaidi. Mikakati haipangwi kwa mihemko na ubishi wenye maneno mengi.
 
Hata Gwajima nae kwenye isssue ya Bashite alikuwa ananikera sana kuonyesha imani kuwa mkulu atachukua hatua wakati ndio kwanza alikuwa anamlinda.

Ifike mahali waacha kuonyesha imani na huyu mtu maana hawasikilizi.
Semeni tu ukweli kwamba mnammiss dr mihogo ili mueleweke.. Vinginevyo mtabweka wee! Lkn mbowe hatawasikiliza ng'oo
 
Back
Top Bottom