Samwel Sitta: Magufuli anashauriwa vibaya!

Samwel Sitta: Magufuli anashauriwa vibaya!

Some people has a cow farm manager mentality, walizoea nchi hii inaendeshwa kama watakavyo, kwa kulindiana status, sasa hivi hata kama una nyume tano, utapigwa tu, ubabaishaji kwisha Kazi
 
Pasco boi wa mamvi. Tulipofikia Tz tunahitaji Rais dikteta hata wa kuwauwa wahalifu. Nchi haihitaji tena Rais mbembelezaji. Kagame na udikteta wake kainyoosha Ruanda. Turudi huku Reli kuwe na kashfa hakuna kashfa hao viongozi wana faida gani hapo? Wakwende zao tu hamna namna
 
Huyu mbakaji wa mchakato wa katiba mpya has no moral authority to speak about anything essential to this country. he had his time but he wasted it.

Very good, Sita hana la kusema kwa sababu hana nia njema kabisa na wa-TZ aliharibu kabisa kwenye Bunge la Katiba alijaribu kupendelea serikali na watawala wasio waaminifu wasio litakia mema Taifa hili. Ni dhambi kubwa kubaka katiba kwa kudharau maoni ya Wananchi. Na kuendesha bunge la ajabu lisilowahi kutokea.
 
Najua Samweli Sita unajua ushauri mzuri na mbaya, Huyu aliyekushauri vizuri kwa haya ninani?
  • Aliyekushauri kuzima maoni ya wananchi katika katiba mpya ukaweka ya chama tawala CCM.
  • Aliyekushauri kupuuza wito wa kusitisha vikao vya bunge la katiba hata baada ya wajumbe wengi kulisusia hususan UKAWA
  • Aliyekushauri kubuni mbinu ya marehemu kuipigia kura ya kuipitisha katiba ya Chenge kuwa katiba pendekezwa.
  • Aliyekushauri kuzuga watanzania kuwa mahujaji waliokuwa wakimrushia shetani mawe waliipigia kura ya ndiyo ya katiba ya Chenge kuwa katiba pendekezwa.
  • Aliyekushauri kuchakachua kura za waliopiga kura za siri za hapana kwa katiba ya Chenge zikageuka kuwa za ndiyo baada ya kuahirisha bunge kuwa zitahesabiwa kesho yake wakati muda wa kuzihesabu ulikuwepo.
  • Aliyekushauri kuaminisha wananchi kuwa wabunge wa bunge la katiba wamekubaliana kwa asilimia kubwa kuipitisha katiba ya Chenge kuwa katiba Pendekezwa.
  • Aliyekushauri ukiwa waziri wa Uchukuzi kumuhonga Tulia Ackson ujumbe wa bodi ya bandari baada ya kubuni kanununi za kuvuruga bunge la katiba.
  • Aliye ushauri kuwa kwa kazi mbovu uliyoifanya katika bunge la katiba sasa ungefaa kuwa rais wa Tanzania.
  • Aliyekushauri kuwa, baada ya kukatwa katika kinyang'anyiro cha kugombea uraisi wa Tanzania sasa urudu kugombea uspika huku ukijua kuwa tayari wananchi waliishakerwa na uhuni wako na utapeli wa kisiasa.

Kama uliona ushauri wooote huo ni mzuri, bila shaka utawaona washauri wabaya wanaomshauri Rais Mheshimiwa, Dr. Magufuli Surgeon wa Majipu kutumbua majipu ya TRA, TPA, RELI, N.K.

Kwanza nimekumbuka kuwa nawewe SITA ni mkusanyiko wa majipu. Hebu angalia,

  1. Pesa ya posho zizosusiwa na wajumbe wa UKAWA katika Bunge la Katiba ulizipeleka wapi?
  2. Ikiwa waziri mwenye dhamana, Ukiukwaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati ya standard gauge ulifanyika ukiwa wapi?
  3. Haraka ya kuingia mkataba huo kabla ya awamu ya nne kuisha na wewe kutema uwazili ilikuwa ya nini?
  4. Hilo jengo la ofisi ya spika ulilojenga Urambo Ndungai atalitumia je?
  5. Ukiwa spika 2005 hadi 2010 Kwanini ulizima hoja ya Richmond na kuifufua mwaka 2015 ulipoona Lowasa anagombea urais kupitia UKAWA?
  6. Ukiwa mkuu wa kitengo cha uwekezaji, we sindo uliileta Richmond? Hukujua kuwa ni kampuni ya mfukoni?
  7. We sindiye ulichapwa na Nyerere viboko kwa utovu wa nidhamu, ulitaka tuwe na rais mwenyesifa ya migomo?

  • Nikiwa Mwana CCM MFU, Nashauri Rais wangu, Dr, (surgeon wa majipu) John Joseph Pombe Mgufuli mwana NGOSHA, apasue majipu ya Samweli Sita kwa SHOKA na Chain Saw, maana ni makubwa saaana kama mbuyu na magumu kama mpingo na yana harufu mbaya kama nanilii, nanilii, na, na ahhh, basi Bwana!
 
mbona yy alikataa ushauri wakati wa bunge la katiba? nadhani awamu zao walishindwa kutekeleza hamu na kiu ya watz walowengi, sasa ni wakati wa wao kukaa pembeni ili wanaume wafanye kazi.
 
Kuna wana CCM humu waliokuwa wanaitetea ccm kwa maneno na kejeli mbn wamegeuka baada ya magufuli kuingia madarakani. Acheni magu aongoze nchi. Sit alitakiwa kufunguliwa hata mashitaka
 
Acheni kumsimanga Masia wa Mungu kwa wa Tz. Watu wamemuomba Mungu sana hali ilikuwa mbaya taifa lilikuwa nusu kubiduka. Mwacheni Magufuli afanye kazi. Tuache ujinga wakukosoa kaz zake pindi anagusa masilah yenu. Tumempata kiongoz hata misitu, tembo na faru walio hama mbuga zetu wameamua kurudi tanzania.

This is a blasphemous statement.
 
watu na madudu yao wanaangaika kila siku

Mwacheni Magufuli awashikishe adabu majizi nyie
 
sijawahi kuwa shabiki wa Sitta lakini kwa hili kuna jambo la kujifunza.......

Mkuu upo sambamba na mimi kabisa. Japokuwa huwa sipendi kumuunga mkono Sitta(Kwa sababu ya Unafiki na Usaliti wake kwa watanzania) lakini katika hili alilosema sasa Sitta, nadhani kuna Kitu cha maana sana tunapaswa kukitafakari.
Lets watch and wait. Ipo siku huenda labda tukayakumbuka haya maneno ya Sitta.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
 
Hata sisi tulishapita huko. Enzi za Nyerere pamoja na kuwakuna kipindi hatukuwa na bidhaa madukani, watu walitembea nusu uchi au kuvaa bipande vya nguo/magunia, lakini tukipiga kura tunampa juu ya asilimia 80! Ya Wanyarwanda si ya kushangaza yalitegemewa.

Ulikuwa umezaliwa au unaongea simulizi za sungura kasema? Mtanyooka tu
 
Katika ile dhana ya kusoma namba, ni wazi imeendelea kuwatafuna wanachama wa chama changu. Katika gazeti la leo, aliyekuwa spika wa bunge la tisa ametoa kali na kusema Rais Magufuli anashauriwa vibaya. Hasa baada ya kutumbua jipu la Reli.

Samwel Sita, kasema Magufuli kachukua hatua hiyo baada ya kushauriwa vibaya, na vile vile ingemfaa achukue muda wa kujiridhisha kwanza!...

Mtanzania, 24.12.2015

Sitta alijuwa jina lake litarudi kwenye mawaziri waliobaki, alipokosa uspika akaona atapewa wizara jina halikuja akawa na matumaini kwenye Wizara zilizobaki pia jina lake halikuja sasa bada majina kutajwa hayumo ndo amedai eti anastaafu siasa wakati roho inamuuma sasa ndo anakuja kukosoa Washauri wa Magafuli na baadae atakuja kusema ata Magufuli sio mtu poa., Madaraka ni matamu sana
 
Raana za watanzani zinanza kumtafuna na bado walitumia pesa nyingi kwenye bunge la katiba bila kufanya chochote na wakazarau Mawazo ya watanzani wakati wakinamama na watoto wanakufa kwa kukosa dawa mahospitalini
 
Alitaka amshauri yeye wapige tena kura za walio kufa kama kwenye rasimu ya katiba??? Sita ulijiharibia mwenyewe sasa kaa kimya watu wajenge Tanzania yao. Wewe ulituingiza shimoni.
 
Ulikuwa umezaliwa au unaongea simulizi za sungura kasema? Mtanyooka tu
Nimepiga kura mara nyingi na ninajua anayeweza kuandika ulivyoandika huna zaidi ya mara mbili kupiga kura nchini!
 
Najua Samweli Sita unajua ushauri mzuri na mbaya, Huyu aliyekushauri vizuri kwa haya ninani?
  • Aliyekushauri kuzima maoni ya wananchi katika katiba mpya ukaweka ya chama tawala CCM.
  • Aliyekushauri kupuuza wito wa kusitisha vikao vya bunge la katiba hata baada ya wajumbe wengi kulisusia hususan UKAWA
  • Aliyekushauri kubuni mbinu ya marehemu kuipigia kura ya kuipitisha katiba ya Chenge kuwa katiba pendekezwa.
  • Aliyekushauri kuzuga watanzania kuwa mahujaji waliokuwa wakimrushia shetani mawe waliipigia kura ya ndiyo ya katiba ya Chenge kuwa katiba pendekezwa.
  • Aliyekushauri kuchakachua kura za waliopiga kura za siri za hapana kwa katiba ya Chenge zikageuka kuwa za ndiyo baada ya kuahirisha bunge kuwa zitahesabiwa kesho yake wakati muda wa kuzihesabu ulikuwepo.
  • Aliyekushauri kuaminisha wananchi kuwa wabunge wa bunge la katiba wamekubaliana kwa asilimia kubwa kuipitisha katiba ya Chenge kuwa katiba Pendekezwa.
  • Aliyekushauri ukiwa waziri wa Uchukuzi kumuhonga Tulia Ackson ujumbe wa bodi ya bandari baada ya kubuni kanununi za kuvuruga bunge la katiba.
  • Aliye ushauri kuwa kwa kazi mbovu uliyoifanya katika bunge la katiba sasa ungefaa kuwa rais wa Tanzania.
  • Aliyekushauri kuwa, baada ya kukatwa katika kinyang'anyiro cha kugombea uraisi wa Tanzania sasa urudu kugombea uspika huku ukijua kuwa tayari wananchi waliishakerwa na uhuni wako na utapeli wa kisiasa.

Kama uliona ushauri wooote huo ni mzuri, bila shaka utawaona washauri wabaya wanaomshauri Rais Mheshimiwa, Dr. Magufuli Surgeon wa Majipu kutumbua majipu ya TRA, TPA, RELI, N.K.

Kwanza nimekumbuka kuwa nawewe SITA ni mkusanyiko wa majipu. Hebu angalia,

  1. Pesa ya posho zizosusiwa na wajumbe wa UKAWA katika Bunge la Katiba ulizipeleka wapi?
  2. Ikiwa waziri mwenye dhamana, Ukiukwaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati ya standard gauge ulifanyika ukiwa wapi?
  3. Haraka ya kuingia mkataba huo kabla ya awamu ya nne kuisha na wewe kutema uwazili ilikuwa ya nini?
  4. Hilo jengo la ofisi ya spika ulilojenga Urambo Ndungai atalitumia je?
  5. Ukiwa spika 2005 hadi 2010 Kwanini ulizima hoja ya Richmond na kuifufua mwaka 2015 ulipoona Lowasa anagombea urais kupitia UKAWA?
  6. Ukiwa mkuu wa kitengo cha uwekezaji, we sindo uliileta Richmond? Hukujua kuwa ni kampuni ya mfukoni?
  7. We sindiye ulichapwa na Nyerere viboko kwa utovu wa nidhamu, ulitaka tuwe na rais mwenyesifa ya migomo?

  • Nikiwa Mwana CCM MFU, Nashauri Rais wangu, Dr, (surgeon wa majipu) John Joseph Pombe Mgufuli mwana NGOSHA, apasue majipu ya Samweli Sita kwa SHOKA na Chain Saw, maana ni makubwa saaana kama mbuyu na magumu kama mpingo na yana harufu mbaya kama nanilii, nanilii, na, na ahhh, basi Bwana!

Mkuu nakupigia saluti umepiga mlemle huyu Mzee anajiaibisha anafikiri watu wamesahau maovu yake .
 
Back
Top Bottom