Samwel Sitta: Magufuli anashauriwa vibaya!

Samwel Sitta: Magufuli anashauriwa vibaya!

kwa hiyo anataka amshauri asome vile vitabu vyake alivyosema ataandika baada ya kustaafu siasa sio??
 
Mbona Wanyarwanda wameendelea kumuamini Kagame tena kwa Wingi.
Magu akitutoa tulipo akae milele.

Bado kidogo mtamtaka awe mungu wenu, manake hammkumbuki Muumba wenu tena bali mmeshampa Magu cheo hicho! Angalia msije mkakufuru, jamani. Huyo ni mwanadamu tu, wa kushangaza na wa ajabu ni Mungu an Malaika zake tu, na sio Magu. Magu hana jipya ndani ya kijani!!! Pasco kamaliza!
 
Kama ataendelea hivi na akaweza kukamata majizi yaliyopo humu ccm na serikalini, vilevile tuyaone mafanikio ya kweli, hata akikaa miaka 29 poa tu!
 
Mchakato wa katiba ya wananchi utawatafuna kwelikweli
 
ni kweli anaangushwa na washauri wake

kaka mvinyo ni ile ile, ila imebadilishwa chupatu. Kwa washauri wale wale walio mbwaga vibaya mzee jakaya na kupelekea slogani ya maisha bora kuwa hadithi za isopo. Kwa watu wale wale usitegemee matokeo tofauti na ya aliyemtangulia. Kama mh magufuli anataka matokeo tofauti basi na mvinyo sharti iwe mpya, na siyo kutia mvinyo kuu kuu, kwenye kibiba kipya. Mambo yakakuwa yale yale mwisho wa siku asubui ya 2020 inawadia unakosa cha kuwambia wananchi kwa haadi ulizotoa mwisho wake unapigwa chini, maana watanzania ni kama wameipa ccm nafasi ya mwisho.
 
Anashauriwa vibaya kwasababu kamstaafisha siasa!!wanasiasa wengi ni wanafiki sana!
 
Hakukosea kumwambia jk aongeze ukali kwani ndo matokeo yake tumeyaona.
Pia ana haki kumwambia jpm anashauriwa vibaya endapo kuna mahali ameona ameona kuna mahali amekosea

Kwa hiyo jk alitakiwa kuongeza ukali na jpm anashauriwa vibaya.

Yeye aliyeshindwa kurudisha chenji iliyobaki kwa wabunge wa ukawa kujitoa kwenye BMK na hajatuambia alizipeka wapi?
watendaji walio chini ya wizara yake kwenda kukopa matirioni ya Pesa kwa ajiri ya kufufa miundo mbinu ya reli na kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa
badala yake wakaamua kujilipa mishahara na kuiachia serikali mzigo wa deni ndio wako sahihi?

Narudia tena sita ajitafakari akae kimya vinginevyo atajishushia hata heshima kidogo aliyobakiza.

Amwache raisi afanye kazi yake haya ndiyo mabadiliko tuliyoyataka yakikupitia rekibisha mambo yako kaa kimya.
 
Kuna kitu kinaitwa manipulation ndugu, viongozi wa kiafrika wanauwezo wa kumanipulate chaguzi mbalimbali, in short mwenye haki ktk chaguzi za kiafrika sio mpiga kura bali mhesabu na mtangaza mshindi! Kwahiyo suala la sijui Kagame anapendwa na wanyarwanda hiyo ni subjectivity!

Well written comrade, halafu hajui Siasa za Rwanda huyo. Kagame is a killer my friend, hata the so called 1994 genocide kwamba wahutu wameua watutsi is one the conspiracy in Rwanda as it's vice versa. In rwanda if u utter anything against Kagame your dead. If there should be uchaguzi wa haki na huru kagame na chama chake kamwe hawezi kuchukua dola. Back to Magufuli he is doing a good job lakini msipuuze maono ya watu. Mimi binafsi nadhani ni busara kufuata sheria na kuheshimu haki za binadamu wakati wa kutumbua hayo majipu.
 
Sita kasingiziwa na watu wenye ajenda ya kumchonganisha na rais kipenzi cha wanamageuzi na wanamabadiliko. Hata mbowe kishamkubali. Sita hawezi kusema hayo kwa sababu alivurugwa na washauri wake na akakubali kuvuga katiba ya watanzania. Kama washauri wenyewe ni kama hao waliomshauri sita kwenye mchakato wa katiba basi rais magufuli asiwaruhusu wasije wakamsita. Songa mbele kiongozi wa watu.
 
Bwana sita sikia haya na kuangalia tu maana mmengekuwa ninyi na serikali yenu mbona mngeamishana mkoa na vyeo, leo serikali yetu hatulembi ni kufunzwa na kutumia sheria
 
Wewe pasco hujitambuagi wewe !! Mimi binafsi cjawahi kukuelewa, ni kama mnafiki flani amazing!! Nahisi hata wewe ni jibu na utatumbuliwa tu iwe kwa busara au kwa kurupuka!!!
 
Wanyarwanda wamelazimika kubadilisha katiba ili Kagame aendelee kutawala si kwa matakwa yao na siyo kwamba katika wanyarwanda wote hakuna mwenyeuwezo wa kutawala isipokuwa ni Kagame tu.

Isipokuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wao,Kagame ni gaidi ambaye akiachwa bila kuwa na madaraka ya urais ndiye atakaye wamaliza wanyarwanda kwa kuwachinja,njia pekee ya wanyarwanda kuendelea kuwa salama ni kumfanya Kagame kuwa rais wao wa kudumu.

Kagame hana historia ya kuwa chini ya mtu kuanzia kipindi kile alichokuwa msituni kila aliyeonekana kuwa ana weza akawa mtawala wake,Kagame alitumia kila mbinu za kummaliza.

👍Thumbs up TUKUNDANE
Watu humu JF hawana clue na Kagame na watutsi juu ya rwanda na great lakes countries in particular
 
Hata kama kipengele cha miaka 5*2 kikiondoka lakini bado anafanya kazi nzuri kwa watanzania ni bora kuliko kuwa na rais mwengine atakaye turudisha tulikotoka.
 
Mwambieni Sita akapumzike kwenye ofisi ya spika aliyojenga Tabora. Kuna upepo mzuri mule
 
Wanyarwanda wamelazimika kubadilisha katiba ili Kagame aendelee kutawala si kwa matakwa yao na siyo kwamba katika wanyarwanda wote hakuna mwenyeuwezo wa kutawala isipokuwa ni Kagame tu.

Isipokuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wao,Kagame ni gaidi ambaye akiachwa bila kuwa na madaraka ya urais ndiye atakaye wamaliza wanyarwanda kwa kuwachinja,njia pekee ya wanyarwanda kuendelea kuwa salama ni kumfanya Kagame kuwa rais wao wa kudumu.

Kagame hana historia ya kuwa chini ya mtu kuanzia kipindi kile alichokuwa msituni kila aliyeonekana kuwa ana weza akawa mtawala wake,Kagame alitumia kila mbinu za kummaliza.
Ujengi mfumo kwa kuangalia mtu bali mfumo unaweza kumchukua/kumsimamia yeyote yule.
 
Back
Top Bottom