Samwel Sitta ashangiliwa sana UDSM

Inawezekana wewe ulipokuwa bado kazini ulikuwa ukiogopa sana kwenda kinyume na mkuu wako lakini Sitta hajaogopa hilo, na ameendelea kupingana ata na chama chake kwenye mambo yenye maslahi ya nchi, sio wengi wenye ujasiri huo.

Mzalendo wa kweli hawezi kusubiri kuwa chama fulani ndipo aanze kupinga uovu au ufisadi unaofanyika, tumeanza lini kuvipenda vyama kuliko nchi yetu? mheshimu sana mtu anayehatarisha maslahi yake binafsi kwa jili ya kupigania maslahi makubwa ya umma.

Hatudanganyiki!!!! Sitta ana uzalendo gani? Unamjua Sitta wewe au unafanya ushabiki? jiulize kwanini Mwl. nyerere alimweka benchi Sitta? Sitta ni mwizi, fisadi and above all ni mnafiki na. 1. kama upo naye karibu mwambie arudishe nyumba aliyojikodishia ambayo analipiwa U$ 7,000 kwa mwezi wakati nyumba za serilkali zipo na amezikataa eti hazina hadhi yake!

Tuondolee upupu sie, kwanini hajitowi CCM na kwenye baraza la mawaziri kama kweli ana uchungu ili apambane akiwa nje ya hao anaowaita mafisadi? Muulize CCJ imeishia wapi? Mnafiki tu.
 
Huwa nikiona habari za Sitta nahisi kichefuchefu.

Alishirki kufunga majadala wa mkataba wa richmond ghafla. Angeruhusu mjadala leo hii Dowans wasingetusumbua.

Waliomzomea Kikwete walikosea, huyu hasa ndiye anayepaswa kuzomewa.
 
SITA,MWAKYEMBE na Wenzie wote wanaojidai wapiganaji akati wanaogopa vivuli vyao wote ni wanafiki wakubwa
mbona itakuwa maafa zaidi kama watakimbia halafu waiache ccm mikononi mwa mkulu, riz1, nape na mwigulu huku wameshikilia usalama wa taifa, polisi na bakwata. bora wabaki wapambane huko huko mkulu ni nuksi
 
Huwa nikiona habari za Sitta nahisi kichefuchefu.

Alishirki kufunga majadala wa mkataba wa richmond ghafla. Angeruhusu mjadala leo hii Dowans wasingetusumbua.

Waliomzomea Kikwete walikosea, huyu hasa ndiye anayepaswa kuzomewa.[/QUOTE]

Dah! Unajikanyagakanyaga tu katika jitihada zako za kumfagilia msanii. Kikwete mangapi ambayo yako ndani ya uwezo wake ameshindwa kuyafanya? Kama huyakumbuki ngoja nikuwekee baadhi tu: kuondoa janga la nchi kuwa gizani na hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji nchini ambao sasa umeanguka kwa kiasi kikubwa, kuhakikisha kwamba mikataba ya madini inabadilishwa ili kuwanufaisha Watanzania. Kuwafukuza kazi wale wote ndani ya baraza lake la Mawaziri ambao utendaji wao ni sifuri ikiwamo Ngeleja, Malima, Mkullo na wengineo wengi
 
Jina la Samwel Sitta lilipotajwa ili apokee recognition pale udsm kama Spika aliyesoma kitivo cha sheria alishangiliwa sana. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe. Kushangiliwa kwake tena na wasomi inaonyesha watanzania wana imani kubwa nae. CCM wakifanya mizengwe namshauri ajiunge Chadema, atapata nafasi nzuri, watanzania wanamhitaji sana.

Ibange sijui jina lako maana yake nini ila nakueleza Sitta haba sifa hata moja ya kuingia Chadema na kudhania Sitta akiwa Rais CCM ita change unapoteza muda wako sana tu .Mwache akae huko huko .Mshangilieni mbebeni lakini si Chadema .
 
Sita ni bogasi sana. Alikuwa mtandao asilia wa kikwete pamoja na hao akina fisadi hadi akajenga ofisi ya spika kule Urambo kama vile yeye atakuwa spika pamanenti!!

Mwulize zile pesa za CDA zilikwenda wapi kama anatofautiana na akina George Mlingwa na Nalaila Kiula siyo unafiki tu
 
Sita ni bogasi sana. Alikuwa mtandao asilia wa kikwete pamoja na hao akina fisadi hadi akajenga ofisi ya spika kule Urambo kama vile yeye atakuwa spika pamanenti!!

Mwulize zile pesa za CDA zilikwenda wapi kama anatofautiana na akina George Mlingwa na Nalaila Kiula siyo unafiki tu

Ebana ile kesi yako dhidi ya Msekwa kule Nebraska imefikia wapi?
 
watu bado hawajamuelewa huyu baba vizur.niwale watu wanaesimamia ukweli hata kama adui yake kafanya vizur atasema.sasa wabongo hamtaki kuambiwa ukweli ndio maana hata kipindi kile jk alivyokua anadanganya mlifurahia kwelii.
 
Inawezekana wewe ulipokuwa bado kazini ulikuwa ukiogopa sana kwenda kinyume na mkuu wako lakini Sitta hajaogopa hilo, na ameendelea kupingana ata na chama chake kwenye mambo yenye maslahi ya nchi, sio wengi wenye ujasiri huo.

Mzalendo wa kweli hawezi kusubiri kuwa chama fulani ndipo aanze kupinga uovu au ufisadi unaofanyika, tumeanza lini kuvipenda vyama kuliko nchi yetu? mheshimu sana mtu anayehatarisha maslahi yake binafsi kwa jili ya kupigania maslahi makubwa ya umma.

mimi nilikuwa napingana na bosi wangu kwenye vikao vya kazini kubwabwaja nje ya utaratibu hakuna maana!wananchi walalamike na sitta naye alalamike??he is a coward na ni mtu hatari.namsihi anyamaze na afuatilie kwa nini wazee wa EAC hatujalipwa mafao yetu.
 
Acha unafiki wewe!! Sitta ni Jasiri!! kama wewe unaona kusema ukweli si ujasiri basi tuoneshe ujasiri kwa kuandika jina lako la ukweli ili tuamini maneno yako!! otherwise shut your pie hole!!
Let the real man of people feel proud!!
mbona point yako haieleweki?kama ni hivyo mimi ni jasiri kuliko sitta,angekuwa jasiri tungemshuhudia hapa jamvini akijibu hoja dhidi yake.jina langu halisi ni jingalao na ninatokea kikonga.
 
Hata Kikwete kabla hajawa Rais alishangiliwa sana na wanachuo na kumshawishi agombee urais hata kabla ya kipindi cha kuchukua fomu. Sikumbuki kulikuwa na tukio gani lililomfanya afike.

wapo waliomnunulia fomu!kwa vboom vyao!
 
ukitaka kujua huyu jamaa ni mnafiki tembeleeni jimboni kwake urambo.....hafai hata kidogo huyu sita (6).
 
hii ni aina nyingine ya upuuzi wa kitanzania hakuna anaye sema THANKS kisa kuna kosa lilifanywa nyuma au linaendelea hata sheria zina hukumu wati kitofauti kutokana na ushirikiano wao au uwajibikaji

mimi sio mfuasi wa SITTA ila kwa maneno anayosema no matter anamaanisha amaanishi ni ya ukweli na muhimu kutolewa na mtu kama yeye sasa watu wanataka yeye afanyeji?
kama kusema ukweli sio mwanzo mzuri baadaye atajua na njia, au mpaka aseme mtu furani hapa ndio yanaoneka sio unafiki tunapima vipi sasa huo unafiki

Well said kwa kweli comment za watu wengine zinasikitisha sana.
 
Kumbe kuna wasomi wanaomshangilia huyu mnafiki?..

Hivi neno mnafiki maana yake nini hasa? Kwa bahati mbaya sana, maadui wa Samuel Sitta, ambao ni mafisadi wa Richmonduli, rada, Kagoda, TICTS na wengineo, ndio . wamekuwa wakitumia neno hili ndani ya CCM na nje kujaribu kumpiga vita na kumchafua kiongozi huyu.

Kwa nyie msiojua, Samuel Sitta ni kiongozi shupavu, msema kweli, anayethubutu, mchapa kazi na kiboko wa mafisadi. Tanzania ingempata mtu kama huyu kuwa Rais nchi hii ingeondokana na umasikini katika kipindi chake cha kwanza tu cha miaka mitano! Msiwe wavivu wa kufikiri na kuburuzwa na mafisadi kumuita eti Sitta ni mnafiki, kwa lipi wakati yeye kila siku ameonesha uongozi na ushupavu wa kusema ukweli? -- eg kupinga hadharani malipo ya Dowans, kusema serikali iombe radhi kwa mgao wa umeme, na mengine mengi.

Kwa msiojua, hata CHADEMA wanamfahamu sana Sitta kuwa ni kiongozi makini ndio maana mwaka 2010 walimuomba agombee Urais kupitia chama hicho. Sitta alipokataa ndio ilibidi CHADEMA wambembeleze Dr. WILLIBROD SLAA agombee Urais wakati alikuwa anataka kutetea kiti chake cha ubunge wa Karatu.

Na kama CCM ikimsimamisha Sitta kuwa mgombea Urais wa 2015, basi CHADEMA watapata taabu sana kupambana naye jukwaani. Huu ndio ukweli, acheni uvivu nyie kwa kulishwa maneno na propaganda za mafisadi.
 
Kama kawaida Watanzania wenye fikra mgando wanaendelea kuimba wimbo waliokaririshwa pasi kufikiri...Mnafiki....Mnafiki....Mnafiki, CCM wote Wanafiki...Wanafiki...Wanafiki, upumbavu mtupu!!

Ebu endeleni tu kuimbaimba huo wimbo huku pasi kujua mkiwakatisha tamaa waliojitolea kupambana na uovu, na kuipa nguvu kambi ya waliojitolea kula pesa za nchi.

Well said, nimegundua wanajamvi wengi humu JF aidha wanafaidi na mfumo uliopo wa kifisadi indirectly au wao ni mafisadi in the making. Haiwezekani mtu anayepinga ufisadi anaitwa mnafiki kwa sababu tu record imekuwa tainted na jambo fulani. Hii siyo haki kabisa
 
Samuel Sitta ni kiongozi shupavu pekee kwenye serikali ya Jakaya Kikwete, kwani amekuwa na guts za kusimama hadharani na kusema ukweli kupingana na ufisadi wa Dowans, mgao wa umeme, kukosekana kwa maadili ya uongozo na mwingineo. Wanafiki ni wale viongozi waliopo serikalini halafu wanalalamika chini kwa chini.

Long live Samuel Sitta, una maadui wengi sana mafisadi, but God and the people of Tanzania are with you all the way!!!
 
Kumbe kuna wasomi wanaomshangilia huyu mnafiki?..Wewe ndo mnafiki mkubwa kumbe nimegundua magamba watu wazuri hamuwapendi! Mimi magamba siwapendi lakini some person i like in magamba he is the among!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom