MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,927
- 6,850
Wahenga walisema; "Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni"; Ni ukweli usiopingika; labda kwa wale wenye bifu zao binafsi!! kwamba Mh Samwel John Sitta; kupitia falsafa yake ya "Kasi na Viwango" alilisimamia Bunge la 9 la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa weledi; umahiri na ufanisi mkubwa sana na hivyo kufaulu kujijengea heshima isiyo na kifani nchini na kwa hiyo kuwa tumaini kubwa la watanzania wengi kwake kuchukua nafasi katika ngazi kubwa katika uongozi wa taifa letu.
Moja ya mambo makubwa aliyoyasimamia akiwa Spika wa bunge la tisa ni uchunguzi wa kashfa ya "Rich-Monduli" iliyohusu mkataba tata wa kufua nishati ya umeme, ambayo ilipelekea kuzuka kwa moja ya matetemeko makubwa kabisa ya kisiasa katika historia ya Tanzania baada ya uchunguzi huo kusababisha kujiuzulu kwa Waziri mkuu wa JMT Mh Edward Ngoyai Lowassa.
Mara tu Baada ya tetemeko hilo kuu, ndipo nyota ya kisiasa ya Mh Sitta ilipoanza kufifia alipochukua hatua isiyotarajiwa na wengi ya kuuzima ghafla na bila maelezo ya kina mjadala wa kashfa ya Rich-Monduli; sina uhakika kama hatua hiyo ilitokana na kutishiwa maisha au kisiasa; kwa vyovyote vile kwa maoni yangu alifanya makosa makubwa sana kwa kuamua kuiponya ama roho yake au nafasi yake baada ya kuwa amechukua hatua za kuichunguza kashfa hiyo ambayo tayari ilishamgharimu sana mwenzie Mh Edward Lowassa! ni bora angeendeleza alichokianzisha mpaka hitimisho kamili;("logical conclusion"). Wengi wetu tulivunjika moyo na kuanza kupoteza imani kwa kasi sana kwa Mh Sitta; kumbe tulikuwa tunastaajabu ya Musa kabla ya kuyaona ya "farahani"!!
Hata hivyo Mh Sitta alifanikiwa kuiokoa nyota yake isizimike kabisa pale alipoamua kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa nje ya bunge kupitia vyombo vya habari, makongamano na makanisani japo alishapoteza "moral authority" ya kukemea maovu hayo baada ya kuuzima mjadala wa moja ya kashfa kubwa zaidi za ufisadi zilizowahi kutokea nchini; Rich-monduli!
Madhara yalishafanyika kwa hiyo kelele za Mh Six dhidi ya ufisadi hazikumsaidia kutetea nafasi yake ya Uspika baada ya kutengenezewa Zengwe la kimataifa ambalo asingeweza kulikwepa kwamba wakati ulikuwa muafaka kuwa na Spika mwanamke; Zengwe ambalo lilimfikisha Mh Anne makinda katika ofisi ya Spika akiwa mwanamke wa kwanza nchini kushika wadhifa huo adhimu.
Kwa bahati nzuri rekodi nzuri ya Bwana Sitta katika bunge la 9 na mapambano yake ya hadharani dhidi ya ufisadi na rushwa vilimsaidia Mh Sitta kubakiza matumaini miongoni mwa baadhi ya watanzania ambao walimuona kwamba alikuwa bado ni Kiongozi bora kuliko wenzie wengi katika chama tawala na kwa hiyo alipojitokeza kugombea uenyekiti wa Bunge maalumu la katiba watanzania wengi waliweka matumaini yao kwake kwamba angesaidia kuliongoza BMK kwa ufanisi kama alivyofanya katika bunge la 9 na kwa hiyo kupelekea kutuwezesha kupata sio tu katiba mpya bali KATIBA BORA kwa kurejea falsafa yake ya kasi na viwango;
Lo salalalah; maajabu ya 8 ya dunia yalikuwa yanatungojea!! mara tu baada ya Mzee Six kuukwaa ueneyekiti wa BMK; kufumba na kufumbua akabadilika "kwa kasi na viwango" vya kutisha kabisa! wengi wetu mpaka leo hii hatujaweza kuelewa ni nini kilichomsibu Mzee huyo mnyamwezi wa Urambo; hatujui kama kilichombadilisha ghafla kilikuwa ni vitisho vya kisiasa au dhidi maisha yake au haja ya kuwafurahisha mahafidhina ndani ya CCM aliowaudhi kutokana uendeshaji wake wa bunge la 9!?
Ghafla bin vuu! Mzee Six akaanza ubabe, kuchakachua kanuni za BMK, akaweka misimamo ya kuegemea matakwa ya chama chake badala ya taifa kisha akatuangushia bomu la Hiroshima kwa kutaka kuwaziba midomo wananchi; Tume ya mabadiliko ya Katiba na vyombo vya habari wasijadili jambo linalohusu mustakabali wao na taifa lao!!
Na hapo ndipo utabiri wa Mh godbless Lema mbunge wa Arusha mjini ulipoanza kutimia; Mh. Lema aliwahi kumwambiua Mh Six katika ukumbi wa BMK mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti kwamba nafasi aliyoipata ilikuwa ni kitanzi cha kujinyongea mwenyewe kwani kama angefanikiwa kulipatia taifa katiba mpya na bora basi ndoto yake kuelekea kugombea Urais 2015 ingeimarika; vinginevyo isipopatika katiba mpya na bora; basi ndoto hiyo atakuwa ameinyonga kwa mikono yake mweyewe!
Mpaka hapa tulipo hakuna mwenye shaka kwamba Mzee six amesha inyonga ndoto yake kwa mikono yake mwenyewe; kwa sasa wengi wetu tunamuona kama NYOTA ILIYOZIMIKA; Msaliti aliyenyonga matumaini ya watanzania; kwa sababu sasa tunajua fika kwamba hatuna matumaini tena ya kupata Katiba mpya wachilia mbali katiba bora!
Kwa bahati mbaya sana; kulingana na hulka za wanasiasa wa NJI hii sitashangaa kumuona na kumsikia Mh Six akijitoa akili na kuendelea kuusaka Urais 2015.
Ushauri wangu wa bure Mzee Six ajitafakari kwa kina kisha achukue hatua inayofaa; afungashe virago vyake arudi Urambo akalee wajukuu na kuanzisha kilimo cha Asali; Kura ya Urais ni ndoto ya mbali sana kwake kwa sasa!
Kwa baadhi yetu rambi rambi za maisha Mh Sitta kisiasa imeshaandikwa inasubiri tu kuchapishwa; swali sio kama itachapishwa bali lini itachapishwa?! it is only a matter of time; and that time is rapidly winding down on him;
Kwa heri ya kuonana Mzee Samwel John Sitta; asante kwa utumishi wako wa umma wa muda mrefu. Tutakukumbuka kwa jinsi ulivyoendesha Bunge la 9 la JMT; kule CDA huna la kujivunia na pale kituo cha Uwekezaji; TIC yule kijana wa Kimasai Ole naiko alikupiku ukafutika kabisa kama hukuwahi kuwepo! na sasa huu utendaji kazi wako katika BMK ni sura inayostahili kufutwa kabisa kutoka katika historia ya nchi yetu.
Adieu Sitta; Good riddance & GOD SPEED.