Hivi neno mnafiki maana yake nini hasa? Kwa bahati mbaya sana, maadui wa Samuel Sitta, ambao ni mafisadi wa Richmonduli, rada, Kagoda, TICTS na wengineo, ndio . wamekuwa wakitumia neno hili ndani ya CCM na nje kujaribu kumpiga vita na kumchafua kiongozi huyu.
Kwa nyie msiojua, Samuel Sitta ni kiongozi shupavu, msema kweli, anayethubutu, mchapa kazi na kiboko wa mafisadi. Tanzania ingempata mtu kama huyu kuwa Rais nchi hii ingeondokana na umasikini katika kipindi chake cha kwanza tu cha miaka mitano! Msiwe wavivu wa kufikiri na kuburuzwa na mafisadi kumuita eti Sitta ni mnafiki, kwa lipi wakati yeye kila siku ameonesha uongozi na ushupavu wa kusema ukweli? -- eg kupinga hadharani malipo ya Dowans, kusema serikali iombe radhi kwa mgao wa umeme, na mengine mengi.
Kwa msiojua, hata CHADEMA wanamfahamu sana Sitta kuwa ni kiongozi makini ndio maana mwaka 2010 walimuomba agombee Urais kupitia chama hicho. Sitta alipokataa ndio ilibidi CHADEMA wambembeleze Dr. WILLIBROD SLAA agombee Urais wakati alikuwa anataka kutetea kiti chake cha ubunge wa Karatu.
Na kama CCM ikimsimamisha Sitta kuwa mgombea Urais wa 2015, basi CHADEMA watapata taabu sana kupambana naye jukwaani. Huu ndio ukweli, acheni uvivu nyie kwa kulishwa maneno na propaganda za mafisadi.