Samwel Sitta ashangiliwa sana UDSM

Kama kawaida Watanzania wenye fikra mgando wanaendelea kuimba wimbo waliokaririshwa pasi kufikiri...Mnafiki....Mnafiki....Mnafiki, CCM wote Wanafiki...Wanafiki...Wanafiki, upumbavu mtupu!!

Ebu endeleni tu kuimbaimba huo wimbo huku pasi kujua mkiwakatisha tamaa waliojitolea kupambana na uovu, na kuipa nguvu kambi ya waliojitolea kula pesa za nchi.
 
kusema sio ujasiri!achukue hatua.
Mbali na kusema atachukua hatua gani? Yeye ndio maana anasema angekuwa yeyey rais asingelipa Dowans, kukema kwa nafisi yake inatosha hana nguvu za sheria kufanya zaidi. Mimi binafsi naona akigombea Dr Slaa na Sitta mimi nitaenda kulala nikiwa na hakika nchi itachukuliwa na mikono salama
 
Wanaompenda Sitta waseme Ndiyooooooooooooooo!
Na wasiompenda jk waseme Siyoooooooooooooooo!
 
Your right. Hata kama ni mnafiki kwani shida ni nini kama anatetea maslahi ya Taifa? Hao wanaojua maovu ya nchi hii na hawasemi sio wanafiki? Mimi nijuavyo mnafiki ni mtu anayezungumza kitu asichokiamini. Hakuna ushahidi kuwa Sitta hayaamini anayozungumza. Alishafika mahali hata akanukuu maneno ya Bible yasemayo: Kuishi kwangu ni Kristo na kufa kwangu ni faida. Sasa mtu bold kama huyu unataka afanye nini zaidi?
Kama kawaida Watanzania wenye fikra mgando wanaendelea kuimba wimbo waliokaririshwa pasi kufikiri...Mnafiki....Mnafiki....Mnafiki, CCM wote Wanafiki...Wanafiki...Wanafiki, upumbavu mtupu!!

Ebu endeleni tu kuimbaimba huo wimbo huku pasi kujua mkiwakatisha tamaa waliojitolea kupambana na uovu, kuipa nguvu kambi ya waliojitolea kula pesa za nchi.
 
Mbali na kusema atachukua hatua gani? Yeye ndio maana anasema angekuwa yeyey rais asingelipa Dowans, kukema kwa nafisi yake inatosha hana nguvu za sheria kufanya zaidi. Mimi binafsi naona akigombea Dr Slaa na Sitta mimi nitaenda kulala nikiwa na hakika nchi itachukuliwa na mikono salama

hata mimi kwa nafasi yangu(mzee mstaafu)nina uwezo wa kusema "ningekuwa rais ningeamuru dowans isilipwe na wahusika wanyongwe"sasa hii inamtofautisha vipi sitta na mvuja jasho wa kawaida?sitta ahame chama au aongoze maandamano ya wanaharakati tumuone yuko serious.
 
Your right. Hata kama ni mnafiki kwani shida ni nini kama anatetea maslahi ya Taifa? Hao wanaojua maovu ya nchi hii na hawasemi sio wanafiki? Mimi nijuavyo mnafiki ni mtu anayezungumza kitu asichokiamini. Hakuna ushahidi kuwa Sitta hayaamini anayozungumza. Alishafika mahali hata akanukuu maneno ya Bible yasemayo: Kuishi kwangu ni Kristo na kufa kwangu ni faida. Sasa mtu bold kama huyu unataka afanye nini zaidi?

kama waziri sitta ana uwezo wa kumshauri au kumshawishi rais kuwa dowans isilipwe,je amewahi kumuandikia barua jk kuhusu dowans?je amewahi kupeleka hoja binafsi kuhusu dowans ijadiliwe kwenye baraza la mawaziri?
 
Jina la Samwel Sitta lilipotajwa ili apokee recognition pale udsm kama Spika aliyesoma kitivo cha sheria alishangiliwa sana. Ukumbi ulilipuka kwa shangwe. Kushangiliwa kwake tena na wasomi inaonyesha watanzania wana imani kubwa nae. CCM wakifanya mizengwe namshauri ajiunge Chadema, atapata nafasi nzuri, watanzania wanamhitaji sana.
Ameishalipa pesa za dowans?

Kwa ushangiliaji huo hata Kivuitu angeshangiliwa!
 
Kwangu mimi, S. Sitta ni kama mtu aliyekua ameshika jiwe la almas,akachezea ktk tundu la choo. Likatumbukia shimoni. Alikua na uwezo wakati ule akiwa spika wa bunge la tisa,kuchukua hatua stahili,na ikibidi kujiuzulu kama angeona anakwazwa na chama chake,na wananchi siku zote wangemheshimu na angekuwa shujaa wetu. Lakini yeye aliamua kukipenda chama chake,akatutosa sisi. Ni yeye alimaliza mjadala wa Richmond bungeni,sisi wananchi tukabaki tumeduwaa. Sasa analalamika nini? Unafiki siku zote haulipi,asubiri kunyolewa na mahasimu wake.
 
hata mimi kwa nafasi yangu(mzee mstaafu)nina uwezo wa kusema "ningekuwa rais ningeamuru dowans isilipwe na wahusika wanyongwe"sasa hii inamtofautisha vipi sitta na mvuja jasho wa kawaida?sitta ahame chama au aongoze maandamano ya wanaharakati tumuone yuko serious.

Inawezekana wewe ulipokuwa bado kazini ulikuwa ukiogopa sana kwenda kinyume na mkuu wako lakini Sitta hajaogopa hilo, na ameendelea kupingana ata na chama chake kwenye mambo yenye maslahi ya nchi, sio wengi wenye ujasiri huo.

Mzalendo wa kweli hawezi kusubiri kuwa chama fulani ndipo aanze kupinga uovu au ufisadi unaofanyika, tumeanza lini kuvipenda vyama kuliko nchi yetu? mheshimu sana mtu anayehatarisha maslahi yake binafsi kwa jili ya kupigania maslahi makubwa ya umma.
 
Acha unafiki wewe!! Sitta ni Jasiri!! kama wewe unaona kusema ukweli si ujasiri basi tuoneshe ujasiri kwa kuandika jina lako la ukweli ili tuamini maneno yako!! otherwise shut your pie hole!!
Let the real man of people feel proud!!
kusema sio ujasiri!achukue hatua.
 
Huyu mzee ni mzuri na yaonekana ana uchungu sana na watanzania maskini na raslimali zao,ila sijui kwa nini anashindwa elewa kuwa hapo alipo hata apge kelele vp kamwe watanzania hawatamwelewa.kwani amesimama pachafu halaf anataka aonekane msafi.

Humjuwi huyu mzee wewe! Sitta ni bonge ya mnafiki. kama kweli anamaanisha anayoyasema hadharani ajitoe kwanza kwenye baraza la mawaziri ndio tutamuona wa maana kuliko kukubaliana na maamuzi ya baraza, akitoka nje anawaruka wenzie kama hakuwa mmoja wa wanaofikia maamuzi ya pamoja. Mie simpi kura yangu hata kwenye ujumbe wa nyumba kumi!
 
sitta alihusika kuufunga mjadala wa richmond harakaharaka kabla ya kufikia muafaka tena kwa shinikizo la magamba wenzake. ukweli ccm hakuna mpambanaji wa dhati
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom