kcamp
JF-Expert Member
- Aug 31, 2014
- 8,526
- 8,033
Wahenga wanasema haraka haraka haina baraka Kampuni ambayo inaongoza kwa kutoa matoleo mengi kwa muda mmoja ikifuatiwa na Techno Leo imesitisha Rasmi utengenezaji wa Samsung Galaxy Note 7 na Seven series devices zote.
Samsung walitoa mda kwa Wateja wao ili kuzirudisha na kuzitengeneza upya Simu hizo hazikusikia la mnadi swala wala mchota maji msikitini ni hizo hizo ambazo zilikua fixed ndo zililipuka tena na kusababisha Goodwill ya kampuni kushuka sana...
"Mtoto hawezi kunyonya maziwa ya mama wa kambo kama mama yake mzazi bado yupo hai" Samsung wamekiri hadi sasa wamepata hasara ya US $18billion Pia imetoa tangazo kuwa Wateja wake wazizime na kuzirudisha kwenye maduka walionunulia na kupatiwa fedha zao "kisicho riziki hakiliki" Katika soko la Hisa bei ya Hisa za kampuni ya Samsung imeporomoka mithili ya akili ya Lipumba Ama kweli ivumayo sana haikawii kupasuka. SUMSANG < TECNO
Social media Reactions
Ukijua jinsi gani swala la battery ni issue basi usingeongea kwa vitambo , haya mambo kweny Tech ni kawaida,General motor kuna kipind walikua na issue ya Brake - Line Failures na ni moja ya kampuni za kibabe,
Hivyo ujue ni maswala ya kawaida na sio kigezo cha kufananisha Samsung na Tecno
Nafikiri tecno ndio vimeo vinavyoongoza kwa thread za majanga humu ndani.