SAMSUNG yasitisha rasmi Uzalishaji wa Samsung Note 7

SAMSUNG yasitisha rasmi Uzalishaji wa Samsung Note 7

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,060
Reaction score
14,689
Wahenga wanasema haraka haraka haina baraka Kampuni ambayo inaongoza kwa kutoa matoleo mengi kwa muda mmoja ikifuatiwa na Techno Leo imesitisha Rasmi utengenezaji wa Samsung Galaxy Note 7 na Seven series devices zote.

Samsung walitoa mda kwa Wateja wao ili kuzirudisha na kuzitengeneza upya Simu hizo hazikusikia la mnadi swala wala mchota maji msikitini ni hizo hizo ambazo zilikua fixed ndo zililipuka tena na kusababisha Goodwill ya kampuni kushuka sana...


"Mtoto hawezi kunyonya maziwa ya mama wa kambo kama mama yake mzazi bado yupo hai" Samsung wamekiri hadi sasa wamepata hasara ya US $18billion Pia imetoa tangazo kuwa Wateja wake wazizime na kuzirudisha kwenye maduka walionunulia na kupatiwa fedha zao "kisicho riziki hakiliki" Katika soko la Hisa bei ya Hisa za kampuni ya Samsung imeporomoka mithili ya akili ya Lipumba Ama kweli ivumayo sana haikawii kupasuka. SUMSANG < TECNO


Social media Reactions




 
Hivi nikimrudishia yule mangi pale Kariakoo ataipokea kweli?? Nauli yangu ya kutoka huku Mbeya wata-refund kweli?? Najiuliza tu
 
Simu zilikuwa Nokia, mbadala wake kwa sasa ni iPhone peke yake, hizo zingine ni mbwembwe tu
 
Nokia and I-phone zitabaki kuwa simu bora kuwahi tokea hapa chini ya jua, hao wengine wanahangaika tu
 
Simu zilikuwa Nokia, mbadala wake kwa sasa ni iPhone peke yake, hizo zingine ni mbwembwe tu

Nokia ilikuwa simu inayojali kipato cha Mteja wake.

Sio hizi simu zingine ikidondoka tu unabaki unajiuliza kuiokota, je kioo kimepona.?
 
Msikariri
 

Attachments

  • 1476196687293.jpg
    1476196687293.jpg
    49.6 KB · Views: 36
Bado wahuni Tecno na Itel!
Tecno wapo vizuri shida ya sumsang anapenda kushindana na iPhone halafu hapo hapo ashindane na tecno,
Tecno wao wanakubali hawawezi kumfikia iPhone ila sumsang wanajitia jeuri
 
Nokia ilikuwa simu inayojali kipato cha Mteja wake.

Sio hizi simu zingine ikidondoka tu unabaki unajiuliza kuiokota, je kioo kimepona.?
Siyo rahisi Kuvunja kioo cha iPhone labda ufanye uzembe wa hali ya juu!
 
Acheni hizo. Samsung mshindani wake c tecno. Hii issue ya bidhaa kuwa na matatizo c ya kwanza kutokea. Kama mtakumbuka kampuni la volkswagen la Germany na hata kampuni la Toyota waliwahi kupatwa na matatizo kama haya.

Ila mleta mada kumenichekesha kusema hisa za samsung zimeshuka kama akili ya LIPUMBAvu... hahaha hahaha.
 
Hivi kampuni in model za simu zaidi ya mia ,, hizi wanazipaje updates , una optimise vipi / customize software kivipi ?, unawezaje kuweka u tofauti wa simu moja na nyingine ... Hii ndo inanifanya nisitumie Samsung milele ...
 
Techno na Samsung!? Wapi na wapi!? Techno level zake ni akina Itel na kidogo Huawei.
Samsung level yake ni akina iphone akifuatiwa na Sony, Lg na kwa mbali Motorola.
 
Watu buana ndio mfananishe sumsung na tecno embu acheni kudharau brandkubwa kama sumsung kwanza tecno western wanazitambua hv nawaza tu
 
Heri wapumzike ili wajipange upya... maana hizi hujuma zimezidi
 
Back
Top Bottom