Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Kama kuna ubaguzi cdm ilikuwaje yeye akawa m/kiti arusha bila kubaguliwa,alishawahi kufanya kazi makao makuu na kwani hakubaguliwa.pili,ilikuwaje katika kikao akatoa taarifa ya kuwasifu watu asiowaamini kama kweli yeye si mnafiki na mamluki? alimsifu mbowe ndani ya kikao ili kumfurahisha nani? huyu anatakiwa atimuliwe tu pamoja na mamluki wenzie.CDM 4 LIFE
 
Asitufanye wajinga si ahamie vyama visivyo na ubaguzi kama ccm!
 
Andiko Zuri, linajieleza, mwenye macho aone, mwenye ufahamu aelewe! hiyo ndio CHADEMA!
 
Kama kuna ubaguzi cdm ilikuwaje yeye akawa m/kiti arusha bila kubaguliwa,alishawahi kufanya kazi makao makuu na kwani hakubaguliwa.pili,ilikuwaje katika kikao akatoa taarifa ya kuwasifu watu asiowaamini kama kweli yeye si mnafiki na mamluki? alimsifu mbowe ndani ya kikao ili kumfurahisha nani? huyu anatakiwa atimuliwe tu pamoja na mamluki wenzie.CDM 4 LIFE

Acha ushabiki, rudia kusoma tena, uelewe!
 
Inaelekea bwana MwanaDiwani unamatatizo makubwa ya akili! Ni juzi tu mwenyekiti wenu wa CCM taifa bila kumung'unya maneno alisema chama chenu kimejengwa katika misingi ya rushwa! mimi nilidhani wewe ukiwa miongoni mwa viongozi wa CCM ungejikita kukiokoa chama chenu na dhahama ya rushwa badala ya kuing'ang'ania CHADEMA!
Nadhani unafahamu kuwa kuokoa kunafanyika kama kuna kitu, binadamu au mnyama anazama.

Mwenyekiti alitoa tahadhari na tahadhari haina maana CCM inazama bali CCM iwe macho.

Rushwa siyo swala ambalo ni geni duniani let alone Tanzania. Hakuna nchi duniani isiyokuwa na tatizo la rushwa na kwa maana hiyo, CCM inajidhatiti kupambana nalo pale litapojitokeza katika kupata wagombea wa nafasi mbali mbali nje na ndani ya chama.

Uongozi wa CCM siyo wa ki-imla. Kila kiongozi ana nafasi yake katika utendaji wa majukumu yake ya kila siku.

CHADEMA is not CCM and CCM will never be CHADEMA.
 
Kinachotakiwa ni kuukomesha huo ubaguzi, sio kuuacha uendelee!
Kama mnasikiliza maoni ya kila kiongozi bila ubaguzi,mbona magamba hamjavua?hadi jina la magamba mmelikubali kwa moyo mmoja kuliko kuyavua magamba hayo.Tena wala usiongee chochote maana unakumbuka hata ya kina Kolimba na wengineo.

Kauli ya kwamba maoni yake hayasikilizwi ni kutapatapa tu,kwasababu maoni yenyewe aliyaleta huku JF kujificha na huku yeye ni kiongozi,je ndipo alipoamini kuwa yale ni maoni ya kusikilizwa?ama aliwakaribisha nyie kina msalani muendeleze kejeli na propaganda chafu dhidi ya chadema?
 
Uongozi wa CCM siyo wa ki-imla. Kila kiongozi ana nafasi yake katika utendaji wa majukumu yake ya kila siku.

CHADEMA is not CCM and CCM will never be CHADEMA.
Uongozi wa CCM umejikita katika rushwa! huwezi kupata uongozi ndani ya CCM bila kutoa rushwa. Rushwa na CCM ni sawa sawa na samaki na maji, bila maji samaki atakufa!
 
Go to hell traitor mkubwa wewe,mission uliyotumwa imekua failed sasa hivi unatapatapa tu!mwisho wako ndipo ulipofikia hapo,mnafiki na msaliti mwenzako nae ataangamia kwa aibu kubwa katika maisha ya siasa!unafiki na usaliti na unafiki ni kitu kibaya sana katika maisha ya mwanadamu!
 
huyu ni mnafiki na hii dhambi itaendelea kumtesa.
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha, Samson Mwigamba, ambaye amesimamishwa kwa muda usiojulikana, ameelezea namna uongozi wa juu wa chama hicho, unavyobagua watu wa kuwaadhibu wakati wa kutoa maoni kuhusu chama.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwigamba pia alikiri kutoa maoni katika mtandao wa Jamii Forum, huku akificha jina lake, akiwasiliana na wanachama wenzake.

Alisema kwa sasa ni vema uongozi uliopo upumzike na kuwaachia wengine, kama walivyofanya viongozi wote waliotangulia. Alisisitiza kwamba alimaanisha alichokiandika na alikuwa habahatishi.

Alitaka wanachama wenzake, waelewe kuwa ni kawaida kiongozi akiwa na maoni yanayohusu mambo ya ndani anayotaka wanachama wenzake wayapate bila kuhusisha cheo chake, huchagua njia yoyote ambayo ataona inafaa, ikiwa ni pamoja mitandao ya jamii kwa kuficha jina lake.

Kawaida hiyo kwa mujibu wa Mwigamba, imetokana na Katiba ya Chadema, kukataza viongozi kutoka hadharani na kuzungumza mambo ya chama, badala yake watumie vikao. Hata hivyo, kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amewahi kufanya kazi makao makuu ya Chadema, vikao hivyo vimeshindwa kushughulikia udhaifu wa uongozi kwa kuwa kila anayejaribu kuhoji, hutangazwa kuwa msaliti wa chama.

“Ni wajumbe wachache sana kwenye Kamati Kuu kwa mfano ambao bado wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi, watu hao hawazidi watatu au wanne, ambao ni Dk Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela (amemtaja kwa jina moja) na mzee Sgerembi ambaye sasa ni marehemu,” alisema Mwigamba.

Alisisitiza kuwa viongozi wengi ndani ya Chadema, wana majina yasiyojulikana kwenye mitandao ya jamii na huyatumia kuzungumza na wanachama mambo mengi, ambayo hawataki yahusishwe na vyeo vyao na mambo hayo hubaki kuwa maoni ya mwanachama binafsi.

Alisema kama angetoka kwenye vyombo vya habari na kujitambulisha na kuanza kuzungumza yale aliyoandika, viongozi wangekuwa na haki ya kumshitaki kwenye mamlaka yake ya nidhamu.

Lakini, alidai hakuna mtu yeyote awe mtaalamu wa Teknolojia ya Habari, au vyovyote vile, mwenye haki ya kwenda kwenye mtandao na kuanza kutafuta anuani kufahamu kilichoandikwa kimetoka kwenye kompyuta gani au nani katuma.

Aliutaka uongozi huo, ueleze wanaofanya kazi ya kufuatilia kila mtu anayetoa maoni kuhusu chama katika mtandao, wametumwa na nani? “Je wanachunguza na kuingilia mawasiliano ya watu wameajiriwa na nani na kazi hiyo wameianza lini na wameshapata watu wangapi?” Alihoji.

Alisema hata kama wameanza kazi hiyo Ijumaa iliyopita na mtu wa kwanza kumpata akawa yeye, wamueleze baada tu ya tukio hilo, wameshapata wengine wangapi, maana bado viongozi wengine wanaendelea kufanya kama alivyofanya yeye.

“Au kuna mtu ama watu fulani ndani ya chama, ukiwagusa tu ndio unatafutwa au kuitwa msaliti wa chama?” Alihoji.

Alisema miezi kadhaa iliyopita, kuna viongozi walijitokeza katika mitandao na kueleza kwa kurudia rudia udhaifu wa viongozi wa chama, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto lakini hivi sasa mmojawapo kati ya watu waliosemwa sana kupitia mtandao huo (hakumtaja jina), amepandishwa cheo na kuwa Ofisa wa Makao Makuu ya chama hicho.

"Siku zijazo tutakuwa na madikteta ambao watatumia demokrasia kujihalalishia utawala wa milele ndani ya vyama vyao na hata ndani ya nchi na ikiwezekana kurithishana utawala kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto, mtoto kwenda mkwe kama ilivyo sasa,” alisema huku akisisitiza kuwa alichoweka katika mtandao alimaanisha Katika mtandao Mwigamba alimpongeza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kufanya mengi katika chama hicho.

Alitaja baadhi kuwa ni pamoja na kutoa chama kutoka kuwa cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.

“Kakichukua kikiwa na wabunge watano bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10, kina wabunge 49. Ni mafanikio makubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake Chadema imebeba ajenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa rasilimali, Katiba mpya na kadhalika,” alisema.

Hata hivyo, alisema kuna matatizo yameanza kujitokeza na wanachama wasipochukua hatua haraka, huko mbele watapata shida kubwa. Alimtaka Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo, asitake kulazimisha kusonga mbele, akidhani bila yeye hakuna Chadema.

“Akiache chama kikiwa salama, abaki kama Mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao,” sehemu ya andiko hilo la Mwigamba ilieleza.

Chanzo:H

Huu ni upuuzi huwezi kuwa kiongozi unaeingia kwenye vikao vya chama ukaleta majungu yako kwenye mitandao ya kijamii,eti unashauriana na wanachama wengine.Mambo ya chama huishia kwenye chama.Kuleta mambo ya hcma huku ni kuvuruga chama.Je ulimuona Lowasa akileta migogoro yao humu?Acheni unafiki,hata nikiwa mimi nakupiga chini tu.Unaharibu reputation ya watu iliyojengwa kwa miaka 20 utegemee public sympathy?Na huyu mjinga asije kukutana na mimi kwenye anga zangu ntamvuruga sana.
 
Hata hivyo, alisema kuna matatizo yameanza kujitokeza na wanachama wasipochukua hatua haraka, huko mbele watapata shida kubwa. Alimtaka Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo, asitake kulazimisha kusonga mbele, akidhani bila yeye hakuna Chadema.

“Akiache chama kikiwa salama, abaki kama Mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao,” sehemu ya andiko hilo la Mwigamba ilieleza.

"Asitake kulazimisha" au "asitake kujilazimisha"? Maana kulazimisha, ina maana Mbowe atawalazimisha wapiga kura wamchague katika uchaguzi ujao, regardless wanaona anafaa au la. Sidhani kama Mbowe ana hiyo jeuri ya kuwalazimisha watu wampigie kura.
It seems kama kuna watu wanamuogopa Mbowe. Wanajiuliza kama ameweza kukitoa chama kutoka cha nne hadi cha kwanza miongoni mwa vyama vya upinzani, ni nini kitatokea endapo ataendelea kuwa mwenyekiti. Kama ameweza kukipa wabunge wapya zaidi ya 40 ndani ya miaka mitano, je atakipa wabunge wangapi baada ya miaka 10 hapo 2015?
 
Chadema it is a chagga movement, kama wewe si mchaga utapata shida sana
Ndo lilokuwa lengo lenu.Kuweka heading yenye kusema chadema ni wabaguzi,kubandika habari kutoka kwenye gazeti ambayo haina uhusiano na kile mnachochangia.Mnafanya makusudi kabisa.Kwahiyo kina Baregu na Mkumbo aliowataja kuwa wanasikilziwa ndo wachagga?

Acheni upotoshaji,haiwasaidii kitu zaidi ya kupanda chuki ambazo zitawacost nyie na watoto wenu.
 
Mwigamba,

Kosa kubwa ulilofanya ni kuwa, JINA LA COMPUTER yako, umeandika Mwigamba. Sasa ulipoandika ujumbe, sijui kwa kutumia MS Office (Word) ukausave kwanza kwenye Computer yako na ulipokuja kuu-Copy, ukachukua na jina la File lilipokuwa limewekwa.

Katika jina hilo, watu wakaona jina lako la Mwigamba na hapo ndipo wengi tukafahamu kuwa ni WEWE. Usingelifanya kosa hili, nina amini hakuna ambaye angelikugusa kwa sababu itakuwa ni kuvunja Miiko ya JF. Hata kama wangelifahamu kuwa ni wewe, basi wangelikuacha tu ili waendelee kukusoma zaidi ila wanakuwa tayari wamekufahamu. Siku ile ile, huo mstari, Mods waliufuta ili kukufichia siri ila kwa bahati mbaya sana, watu wakawa wameshau-copy.

Je mnakumbuka ujumbe huu wa 5th April 2012

[h=2]Samson Mwigamba una nini na Dr Slaa?[/h]
Jana nimesoma kwa makini sana makala ya Samson Mwigamba kwenye Tanzania Daima na nikashangaa sana. Nimemtumia ujumbe kumuuliza alikuwa na maana gani lakini mpaka sasa hajanijibu. Hili ndilo nililoligundua katika makala aliyoipa kichwa "Arumeru Mashariki ilikuwa kama operation ya Kijeshi"

Ameelezea mambo mengi na kuwashukuru watu wengi sana waliofanya kazi ya ukombozi Arumeru, Ameanzia kwa Mh Mbowe, Mameneja wa Kampeni Mchungaji Natse na V Nyerere, Mkuu wa operation John Mrema, Katibu wa CDM wa mkoa, Viongozi wa Bavicha na wengine wengi. Lakini jambo la ajabu ni kuwa hakuna hata mahali ambapo alimtaja Dr Slaa. Sasa mimi nimejiuliza inawezekanaje Mwigamba asimuone Dr Slaa kwenye kampeni? Vyombo vya habari vilituambia kuwa Dr Slaa alipokewa kifalme Arumeru, tulimuona na kumsikia kwenye majukwaa akimnadi Joshua, ni yeye aliyekashifiwa kuiba pesa za ujio wa Papa, ni yeye alitukanwa matusi mazito na Ndugu Lusinde. Sasa inawezekanaje Mwigamba asimtaje katika shukrani zake? Huu ndio ukamamnda gani, hata kama kuna sintofahamu baina yao kwa nini analionyesha hadharani hivyo? Nilitamani niwawekee vipande vya shukrani zake lakini Tanzania Daima online haikuiweka hiyo makala, sijui ni bahati mbaya ama wameistukia kama mimi nilivyofanya?

Makamanda tuache unafiki, hata kama mtu ameondolewa kuwa mhasibu wa chama sio sababu ya kuweka kinyongo, tujue tu kuwa cheo ni dhamana na si haki ya mtu. Ukombozi utaletwa na watu makini wenye nia ya dhati na wasio na agenda ya siri nyuma yao. Hoja zote ni lazima ziwekwe mezani, zijadiliwe kisha tusonge mbele kwenye mapambano.

Samson angalia sana usije ukajiweka upande mbaya wa historia ya taifa letu. Katika ujumbe wangu wa jana nilitoa wito kwako uombe radhi wasomaji wako na wana CDM popote pale walipo kwa kosa hilo. Inawezekana ulipitiwa tu na hukudhamiria, kama hivyo ndivyo basi nami utanisamehe.

Soma hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/245518-samson-mwigamba-una-nini-na-dr-slaa.html

Aliutaka uongozi huo, ueleze wanaofanya kazi ya kufuatilia kila mtu anayetoa maoni kuhusu chama katika mtandao, wametumwa na nani? "Je wanachunguza na kuingilia mawasiliano ya watu wameajiriwa na nani na kazi hiyo wameianza lini na wameshapata watu wangapi?" Alihoji.

Alisema hata kama wameanza kazi hiyo Ijumaa iliyopita na mtu wa kwanza kumpata akawa yeye, wamueleze baada tu ya tukio hilo, wameshapata wengine wangapi, maana bado viongozi wengine wanaendelea kufanya kama alivyofanya yeye.

"Au kuna mtu ama watu fulani ndani ya chama, ukiwagusa tu ndio unatafutwa au kuitwa msaliti wa chama?" Alihoji.
 
"Asitake kulazimisha" au "asitake kujilazimisha"? Maana kulazimisha, ina maana Mbowe atawalazimisha wapiga kura wamchague katika uchaguzi ujao, regardless wanaona anafaa au la. Sidhani kama Mbowe ana hiyo jeuri ya kuwalazimisha watu wampigie kura.
It seems kama kuna watu wanamuogopa Mbowe. Wanajiuliza kama ameweza kukitoa chama kutoka cha nne hadi cha kwanza miongoni mwa vyama vya upinzani, ni nini kitatokea endapo ataendelea kuwa mwenyekiti. Kama ameweza kukipa wabunge wapya zaidi ya 40 ndani ya miaka mitano, je atakipa wabunge wangapi baada ya miaka 10 hapo 2015?
Wewe ndiyo hujamulelewa Samson Mwigamba ndani ya mantiki ya KULAZIMISHA.

Mwigamba ana maanisha Mh. Mbowe amelazimisha uongozi kwa kutoa kipengele kilichoweka kikomo cha uongozi katika nafasi hiyo moja zaidi ya chaguzi mbili.

Matatizo yaliyojitokeza kati ya Mh. Zitto na Mh. Mbowe kwenye chaguzi kuu zilizopita yangepunguzwa katika chaguzi zijazo na kipengele hicho kama ilivyokuwa inafantika wakati kipengele hicho kiko ndani ya katiba.

Mtei---->Makani-------->Mh. Mbowe----------->Haijulikani lini?.
 
But kipengele cha kuchaguliwa kwa kura hakijaondolewa. Wapiga kura ndio watakaoamua nani awe mwenyekiti, sio Mbowe...
 
Ndo lilokuwa lengo lenu.Kuweka heading yenye kusema chadema ni wabaguzi,kubandika habari kutoka kwenye gazeti ambayo haina uhusiano na kile mnachochangia.Mnafanya makusudi kabisa.Kwahiyo kina Baregu na Mkumbo aliowataja kuwa wanasikilziwa ndo wachagga?

Acheni upotoshaji,haiwasaidii kitu zaidi ya kupanda chuki ambazo zitawacost nyie na watoto wenu.
Chagga Development Manifesto
 
Chadema mnasema mmeanza na Mungu na kumaliza na Mungu sasa ndo kauli zenu za kilaanifu zinawadhuru maana mnazani Mungu anataka upumbavu wenu na ulaghai?
mnajitia kufuru zinawadhuru sasa. Ati tumeanza na Mungu sijui Mungu yupi anaetaka injustice. Labda hio mizimu ya wachaga ndo Mungu wenu. Nyambaf.
 
pengine Wewe ni miongoni wa CHADEMA wanaofaidi ufujaji wa fedha zinazopigiwa kelele na MWIGAMBA, ila za mwizi ni arobaini, nadhani huu ni mwisho wa MBOWE na SLAA.
Ccm jitegeni kama fisi anaesubiri mkono udondoke,MWIGAMBA hata Arusha hana jina ati akiyumbishe chama? LUMUMBA JIDANGANYENI.R.I.P CCM
 
Back
Top Bottom