Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

sikilizen niwaambie; mnapokua wapinzan ni lazima yafuatayo yawepo
1.muwe na umoja wa kweli as one system regardless hupendi,
2.Ni lazima muwe wavumilivu
3.Lazima ukubali kusubili kama mmepata kiongoz ambae ameonesha chanya kufikia lengo la kuiangusha chama tawala,kwa sababu kuna madhara ,makubwa sana ya kubadilisha uongozi wakat mmnaona mnaelekea ushindi, nakubali safu ya Mbowe,slaa,zitto,lissu na mnyika imepangwa ikapangika,wamefaulu kuwadhibiti ccm na propaganda zao, mfano ukawabasili saiv,ukamuweka mtu ambae hajazoea mikiki mikiki na uzush wa ccm lazima cdm ife, siwafichi mimi ule uzushi wa ugaidi wa lwakatare nilijua cdm ndo imeisha,lakin kutokana na safu nzuri ya uongoz,sikuamini kabisaaaaaa! Mi naona hata kama muda umekwisha wa kukaa madarakani mbowe,slaa,zitoo,mnyika,lissu wabaki tu coz tumekaribia ushindi jamani,huu muda si wa kugombana eti katiba inasema ooh we mwigamba tulia mchukue dola kama uongoz utapata tu,umetumwa?
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha, Samson Mwigamba, ambaye amesimamishwa kwa muda usiojulikana, ameelezea namna uongozi wa juu wa chama hicho, unavyobagua watu wa kuwaadhibu wakati wa kutoa maoni kuhusu chama.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwigamba pia alikiri kutoa maoni katika mtandao wa Jamii Forum, huku akificha jina lake, akiwasiliana na wanachama wenzake.

Alisema kwa sasa ni vema uongozi uliopo upumzike na kuwaachia wengine, kama walivyofanya viongozi wote waliotangulia. Alisisitiza kwamba alimaanisha alichokiandika na alikuwa habahatishi.

Alitaka wanachama wenzake, waelewe kuwa ni kawaida kiongozi akiwa na maoni yanayohusu mambo ya ndani anayotaka wanachama wenzake wayapate bila kuhusisha cheo chake, huchagua njia yoyote ambayo ataona inafaa, ikiwa ni pamoja mitandao ya jamii kwa kuficha jina lake.

Kawaida hiyo kwa mujibu wa Mwigamba, imetokana na Katiba ya Chadema, kukataza viongozi kutoka hadharani na kuzungumza mambo ya chama, badala yake watumie vikao. Hata hivyo, kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amewahi kufanya kazi makao makuu ya Chadema, vikao hivyo vimeshindwa kushughulikia udhaifu wa uongozi kwa kuwa kila anayejaribu kuhoji, hutangazwa kuwa msaliti wa chama.

“Ni wajumbe wachache sana kwenye Kamati Kuu kwa mfano ambao bado wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi, watu hao hawazidi watatu au wanne, ambao ni Dk Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela (amemtaja kwa jina moja) na mzee Sgerembi ambaye sasa ni marehemu,” alisema Mwigamba.

Alisisitiza kuwa viongozi wengi ndani ya Chadema, wana majina yasiyojulikana kwenye mitandao ya jamii na huyatumia kuzungumza na wanachama mambo mengi, ambayo hawataki yahusishwe na vyeo vyao na mambo hayo hubaki kuwa maoni ya mwanachama binafsi.

Alisema kama angetoka kwenye vyombo vya habari na kujitambulisha na kuanza kuzungumza yale aliyoandika, viongozi wangekuwa na haki ya kumshitaki kwenye mamlaka yake ya nidhamu.

Lakini, alidai hakuna mtu yeyote awe mtaalamu wa Teknolojia ya Habari, au vyovyote vile, mwenye haki ya kwenda kwenye mtandao na kuanza kutafuta anuani kufahamu kilichoandikwa kimetoka kwenye kompyuta gani au nani katuma.

Aliutaka uongozi huo, ueleze wanaofanya kazi ya kufuatilia kila mtu anayetoa maoni kuhusu chama katika mtandao, wametumwa na nani? “Je wanachunguza na kuingilia mawasiliano ya watu wameajiriwa na nani na kazi hiyo wameianza lini na wameshapata watu wangapi?” Alihoji.

Alisema hata kama wameanza kazi hiyo Ijumaa iliyopita na mtu wa kwanza kumpata akawa yeye, wamueleze baada tu ya tukio hilo, wameshapata wengine wangapi, maana bado viongozi wengine wanaendelea kufanya kama alivyofanya yeye.

“Au kuna mtu ama watu fulani ndani ya chama, ukiwagusa tu ndio unatafutwa au kuitwa msaliti wa chama?” Alihoji.

Alisema miezi kadhaa iliyopita, kuna viongozi walijitokeza katika mitandao na kueleza kwa kurudia rudia udhaifu wa viongozi wa chama, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto lakini hivi sasa mmojawapo kati ya watu waliosemwa sana kupitia mtandao huo (hakumtaja jina), amepandishwa cheo na kuwa Ofisa wa Makao Makuu ya chama hicho.

"Siku zijazo tutakuwa na madikteta ambao watatumia demokrasia kujihalalishia utawala wa milele ndani ya vyama vyao na hata ndani ya nchi na ikiwezekana kurithishana utawala kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto, mtoto kwenda mkwe kama ilivyo sasa,” alisema huku akisisitiza kuwa alichoweka katika mtandao alimaanisha Katika mtandao Mwigamba alimpongeza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kufanya mengi katika chama hicho.

Alitaja baadhi kuwa ni pamoja na kutoa chama kutoka kuwa cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.

“Kakichukua kikiwa na wabunge watano bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10, kina wabunge 49. Ni mafanikio makubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake Chadema imebeba ajenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa rasilimali, Katiba mpya na kadhalika,” alisema.

Hata hivyo, alisema kuna matatizo yameanza kujitokeza na wanachama wasipochukua hatua haraka, huko mbele watapata shida kubwa. Alimtaka Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo, asitake kulazimisha kusonga mbele, akidhani bila yeye hakuna Chadema.

“Akiache chama kikiwa salama, abaki kama Mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao,” sehemu ya andiko hilo la Mwigamba ilieleza.

Chanzo:Habari leo.
Kinachomuumiza Mwigamba ni kwamba ameshitukiwa kabla hajamaliza kazi aliyopewa na Magamba
 
Sisi wengine ngoja tuwe wasomaji tu.
 
sikilizen niwaambie; mnapokua wapinzan ni lazima yafuatayo yawepo
1.muwe na umoja wa kweli as one system regardless hupendi,
2.Ni lazima muwe wavumilivu
3.Lazima ukubali kusubili kama mmepata kiongoz ambae ameonesha chanya kufikia lengo la kuiangusha chama tawala,kwa sababu kuna madhara ,makubwa sana ya kubadilisha uongozi wakat mmnaona mnaelekea ushindi, nakubali safu ya Mbowe,slaa,zitto,lissu na mnyika imepangwa ikapangika,wamefaulu kuwadhibiti ccm na propaganda zao, mfano ukawabasili saiv,ukamuweka mtu ambae hajazoea mikiki mikiki na uzush wa ccm lazima cdm ife, siwafichi mimi ule uzushi wa ugaidi wa lwakatare nilijua cdm ndo imeisha,lakin kutokana na safu nzuri ya uongoz,sikuamini kabisaaaaaa! Mi naona hata kama muda umekwisha wa kukaa madarakani mbowe,slaa,zitoo,mnyika,lissu wabaki tu coz tumekaribia ushindi jamani,huu muda si wa kugombana eti katiba inasema ooh we mwigamba tulia mchukue dola kama uongoz utapata tu,umetumwa?
usishangae, hawa kina Mwigamba hata ndani ya ANC ya kina Oliva Tambo na Mzee Madiba walikuwepo. na hata ndani ya ccm ndo kabsaaaaaa wamejaa kibao ila wanadhibitiwa na system. kwa kawaida watu wa namna hii ni waganga njaa, wabinafs na walafi wa madaraka. CDM ni zaidi ya chama cha siasa, ni movement ya Ukombozi, chadema ni Mkuki wa Taifa, ni a democratic guerrilla group. sasa movement ya namna hiyo haiwezi kukaa chini kila wakati KUFKIRIA kugawa vyeo. tupo msituni tunapiga vita vya ukombozi, vita nyingine tena ya kugombea vyeo ya nini? ngoja kwanza tumalize kazi mbona mavyeo yatakuwepo kibao tu wandugu?! wee Mwigamba na hao unaowasemea wamekutuma?
 
haya mambo ya kubaguana yameshakuwa kelo sasa chadema lazima waweze kujitathimini vitendo vyao vya kuwanyima watu uhuru wa kuzungumza.
 
kamradi kenu kanaanza kuingia mchanga taratibu, mwishowe chali..

kaka hii SACOS lazima itakufa naona mbinu zao karibu zote zinaumbuka taratibu tena mchana kweupe.
 
Acha kabisa mkuu, naona mradi wa jamii ya kilimanjaro unakosa mashabiki..makao makuu sasa yatahamia rombo na si mtaa wa ufipa tena..
 
Mradi unaoingia mchanga ni wa mafisadi.Wadanganyika wameshaanza kuzinduka.
Hata wale waliokuwepo kipindi cha nuhu walikua wakiambiwa gharika inakuja wanabisha, sasa wewe endelea kushangaa , kama una shares mkuu nakushauri udai chako mapema maana kamradi kanakosa watoa jasho mda si mrefu, misukule inafufuka..
 
Si aende CCM mbona CCM wameboresha demokrasia yao mwenyekiti wao hapo awali alikuwa anasimama na kivuli kwenye chaguzi mbalimbali kwa sasa ni marufuku kumpinga mwenyekiti wa CCM.Ina maana hajavutiwa na demokrasia hii ya CCM mpaka aendelee kuig'ag'ania CHADEMA ambayo haina demokrasia.
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha, Samson Mwigamba, ambaye amesimamishwa kwa muda usiojulikana, ameelezea namna uongozi wa juu wa chama hicho, unavyobagua watu wa kuwaadhibu wakati wa kutoa maoni kuhusu chama.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mwigamba pia alikiri kutoa maoni katika mtandao wa Jamii Forum, huku akificha jina lake, akiwasiliana na wanachama wenzake.

Alisema kwa sasa ni vema uongozi uliopo upumzike na kuwaachia wengine, kama walivyofanya viongozi wote waliotangulia. Alisisitiza kwamba alimaanisha alichokiandika na alikuwa habahatishi.

Alitaka wanachama wenzake, waelewe kuwa ni kawaida kiongozi akiwa na maoni yanayohusu mambo ya ndani anayotaka wanachama wenzake wayapate bila kuhusisha cheo chake, huchagua njia yoyote ambayo ataona inafaa, ikiwa ni pamoja mitandao ya jamii kwa kuficha jina lake.

Kawaida hiyo kwa mujibu wa Mwigamba, imetokana na Katiba ya Chadema, kukataza viongozi kutoka hadharani na kuzungumza mambo ya chama, badala yake watumie vikao. Hata hivyo, kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amewahi kufanya kazi makao makuu ya Chadema, vikao hivyo vimeshindwa kushughulikia udhaifu wa uongozi kwa kuwa kila anayejaribu kuhoji, hutangazwa kuwa msaliti wa chama.

“Ni wajumbe wachache sana kwenye Kamati Kuu kwa mfano ambao bado wanaweza kusimama kidete na kukosoa uongozi, watu hao hawazidi watatu au wanne, ambao ni Dk Kitila Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, Mzee Shilungushela (amemtaja kwa jina moja) na mzee Sgerembi ambaye sasa ni marehemu,” alisema Mwigamba.

Alisisitiza kuwa viongozi wengi ndani ya Chadema, wana majina yasiyojulikana kwenye mitandao ya jamii na huyatumia kuzungumza na wanachama mambo mengi, ambayo hawataki yahusishwe na vyeo vyao na mambo hayo hubaki kuwa maoni ya mwanachama binafsi.

Alisema kama angetoka kwenye vyombo vya habari na kujitambulisha na kuanza kuzungumza yale aliyoandika, viongozi wangekuwa na haki ya kumshitaki kwenye mamlaka yake ya nidhamu.

Lakini, alidai hakuna mtu yeyote awe mtaalamu wa Teknolojia ya Habari, au vyovyote vile, mwenye haki ya kwenda kwenye mtandao na kuanza kutafuta anuani kufahamu kilichoandikwa kimetoka kwenye kompyuta gani au nani katuma.

Aliutaka uongozi huo, ueleze wanaofanya kazi ya kufuatilia kila mtu anayetoa maoni kuhusu chama katika mtandao, wametumwa na nani? “Je wanachunguza na kuingilia mawasiliano ya watu wameajiriwa na nani na kazi hiyo wameianza lini na wameshapata watu wangapi?” Alihoji.

Alisema hata kama wameanza kazi hiyo Ijumaa iliyopita na mtu wa kwanza kumpata akawa yeye, wamueleze baada tu ya tukio hilo, wameshapata wengine wangapi, maana bado viongozi wengine wanaendelea kufanya kama alivyofanya yeye.

“Au kuna mtu ama watu fulani ndani ya chama, ukiwagusa tu ndio unatafutwa au kuitwa msaliti wa chama?” Alihoji.

Alisema miezi kadhaa iliyopita, kuna viongozi walijitokeza katika mitandao na kueleza kwa kurudia rudia udhaifu wa viongozi wa chama, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto lakini hivi sasa mmojawapo kati ya watu waliosemwa sana kupitia mtandao huo (hakumtaja jina), amepandishwa cheo na kuwa Ofisa wa Makao Makuu ya chama hicho.

"Siku zijazo tutakuwa na madikteta ambao watatumia demokrasia kujihalalishia utawala wa milele ndani ya vyama vyao na hata ndani ya nchi na ikiwezekana kurithishana utawala kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto, mtoto kwenda mkwe kama ilivyo sasa,” alisema huku akisisitiza kuwa alichoweka katika mtandao alimaanisha Katika mtandao Mwigamba alimpongeza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kufanya mengi katika chama hicho.

Alitaja baadhi kuwa ni pamoja na kutoa chama kutoka kuwa cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.

“Kakichukua kikiwa na wabunge watano bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10, kina wabunge 49. Ni mafanikio makubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake Chadema imebeba ajenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa rasilimali, Katiba mpya na kadhalika,” alisema.

Hata hivyo, alisema kuna matatizo yameanza kujitokeza na wanachama wasipochukua hatua haraka, huko mbele watapata shida kubwa. Alimtaka Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo, asitake kulazimisha kusonga mbele, akidhani bila yeye hakuna Chadema.

“Akiache chama kikiwa salama, abaki kama Mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao,” sehemu ya andiko hilo la Mwigamba ilieleza.

Chanzo:Habari leo.

mwigulu na wasira walisema wako wengi; labda ndiyo kifo waliyotabiria,,,, mla rushwa mkubwa aitwe kijana wa mwigulu si mwennyekiti tena
 
ni afadhali chama cha wachagga kuliko chama cha majambazi ya kodi za wananchi, majangili ya pembe za ndovu na wauza sembe
hapo hakuna afadhali mkuu, hiyo jamii inasifa inayofahamika vizuri inapokuja kwenye maswala ya fedha
 
Watanzania tuache siasa za maji taka za kuhujumiana na kukashfiana ili kupata uongozi ni vizuri tufuate taratibu na kanuni tulizokubalia huwezi hukawa kiongozi ndani ya chama alafu ukawa unalalamika pembeni wakati kuna utaratibu mmejiwekea ni heri mwigamba hukiri umefanya kosa wewe kama kiongozi hukutakiwa kufanya hivo. Je endapo wewe ndio ungekuwa mwenyekiti alafu akatokea mtu na kuanza kukushutumu nje ya vikao halali ungekubali?
 
Mkuu Feedback hilo hawawezi kujibu maana kila siku wakiamka ni Slaa au Mbowe au Zitto au Mnyika mpaka wanatuchosha tusio na vyama maana wanaacha mambo ya msingi imebaki ni kujadili watu na vyama tuu
Kila siku ni CDM na CCM mbona NCCR au TLP au UDP au CUF haizungumzwi au wale wasio na vyama au wasio wafuasi waende wapi
Kwa nini msizungumzie matatizo ya wananchi wanaokosa huduma muhimu au wanaokabiliwa na njaa na umaskini wa kutupwa kila siku ni vyama tuu na watu binafsi na maisha yao

kuna kitu humu jf watu wengi hawakijui. Hawa vijana wsa ccm wanaopost mambo yanayohusu chadema kila siku na kila saa ni walinzi wa ofisi za ccm ( Dar na Dom). Wanapokezana kupost sambamba na shift zao za ulinzi, hata mambo wanayoyaandika ni yaleyale kila siku na karibu kila thread. Na hayo ni maelekezo ya kitengo cha propaganda cha chama. Hakuna sababu ya kuhangaika nao!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom