Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Samson Mwigamba: CHADEMA kuna ubaguzi

Mwigamba aende ccm pasipo na ubaguzi akapambane na ukoo wa mwinyi,nyerere,kawawa,karume,nnauye,makamba,malecela,kikwete

Kama ameuweza kuuvua nguo Ukoo wa MTEI na MBOWE CCM ataweza tu.
 
Hivi alichokizema yeye... WA CCM anaweza kusema dhidi ya VIONGOZI wakuu wa CCM? Kwanini ni kwa CHADEMA tu ndio VIONGOZI wakuu ni Wabaguzi? hawa ea CCM pia... Umejaribu kugombea U-NEC ndani ya CCM? kama haujulikwani na ukatoa hotuba nzuri watakubagua kwasababu wewe sio kwenye KUNDI LAO - A CULT WITHIN

Sasa where is the beef???

hapa ndo napo wachoka wapinzani na wafuasi wake eti kwasababu fulani yuko hivi na wewe ukiangukia kwenye mkumbo huo ukiambiwa unaanza kufanya mfanano,badala wewe ujipambanue kujiweka sawa unang'ang'ania uwozo wako huo huo,Chdema itauwawa na vitu na vijimambo vidogovidogo,huku viongozi na na makada wakibaki kubwatukia usaliti,masalia na kadhalika
 
Mtu msomi wa kariba ya mwigamba kueleza uhalo wa namna hii,anathibitisha jinsi wasomi wetu walivyo. Yeye alijiunga cdm kuja kuleta mabadiliko ya chama au alitaka nini!? Alipokuwa makao makuu hakukuwa na malalamiko km haya. Km anaona cdm kuna ubaguzi,aondoke aangalie vyama vingine,na kwa vile anamuona mbowe ni dhaifu na yeye aende akainue chama chake. Akae akijua sisi tuna akili kuliko yeye,maneno aliyosema yanapaswa kutolewa na watu wa LUMUMBA(LB-7). Hivi mwigamba km kweli ana akili,anajisikiaje maneno yake kupewa uzito na watu wa lumumba? Ujinga mwingine bhaana!
 
chadema mpango wa Mungu namna alivyo kamatwa msaliti Arusha inajizihilusha kuwa chadema ni mipango ya Mungu..
MBOWE na SLAA wakiwashinda , tutawatoa sisi tusiyo wanachama kwa sababu tunataka chama kiwe cha watu na siyo taasisi ya mtu.
 
Sasa si aende huko ambako hakuna ubaguzi au ukanda au hakuna kupigwa au hakuna wasaliti anachosubiri na kulalamika ni nini.
Na swali jingine kwani chama ni CDM tuu kuna vyama vingi kuna CCM kuna NCCR kuna TLP aende huko hakuna ubaguzi wala maneno mengi mbona anang'ang'ania tuu hapa na kutoa matamko mengi na wanamshabikia na kumuanzishia thread ni wale wale waliotuma kufanya kazi yake

Lengo ni kukinusuru CHADEMA na si vinginevyo, Akiondoka CHADEMA bado kinaendelea kuendeshwa kama Kampuni, Ni lazima akomae huko huko ili wa-ufyate.
 
Mgogoro wa CHADEMA ni wa wanachadema, wengine ni watazamaji tu na wala msitafute mchawi kwingine. MBOWE na SLAA wakubali tu wameshindwa kutokana na uchu wa madaraka na Ubinafsi na hivyo wakae pembeni wengine wakivushe chama kutoka hapo kinapotaka kuzamia.

Hao watazamaji mbona wamekuwa wao ni wapambe wakubwa wa kutoa na kuandika mabandiko humu
Watazamaji wamekuwa marefa na waamuzi wa pambano badala ya kuwaachia refa na waamuzi wake wamalize mchezo wao
Wasingekuwa wasemaji wakubwa kwani humu tungeona kila saa mabandiko ya Samsom Mwigamba au ya akina Slaaa na Mbowe na Zitto si wageyamalizia huko huko
Kuna vikao vyao na wana nafasi zao kusuluhisha mambo yao ila kila muda mada ni hizo hizo as if hatuna matatizo yetu yanayotukabili
 
Lengo ni kukinusuru CHADEMA na si vinginevyo, Akiondoka CHADEMA bado kinaendelea kuendeshwa kama Kampuni, Ni lazima akomae huko huko ili wa-ufyate.

Hakuna cha kunusuru chama hapa
Huwezi ukatoka nje ya utaratibu na then utegemee refa wa mchezo akuachie tuu kwa vile ukitolewa nje mchezo utaharibika
Na kupambana na refa unajua adhabu yake ni kutolewa kwa kadi nyekundu tuu na unatolewa nje ya uwanja kabisa
Sasa huko nje ya uwanja katafakari na ujione ni wapi ulikosea na kisha urudiufuate sheria za mchezo na sio kujiamulia tuu kucheza rough zako ambazo kisheria hazipo
Iwapo una malalamiko kuna waamuzi mpaka wa akiba na una meneja wako na kocha wako nenda kalalamike huko na nahodha wa mpira pia yupo lalamika kwake ya nini kulalamika kwa watazamaji ambao hawatakusaidia lolote
 
MBOWE na SLAA wakiwashinda , tutawatoa sisi tusiyo wanachama kwa sababu tunataka chama kiwe cha watu na siyo taasisi ya mtu.

yaani ccm mtuchagulie mwenyekiti na katibu hilo halitatokea..
 
Hao watazamaji mbona wamekuwa wao ni wapambe wakubwa wa kutoa na kuandika mabandiko humu
Watazamaji wamekuwa marefa na waamuzi wa pambano badala ya kuwaachia refa na waamuzi wake wamalize mchezo wao
Wasingekuwa wasemaji wakubwa kwani humu tungeona kila saa mabandiko ya Samsom Mwigamba au ya akina Slaaa na Mbowe na Zitto si wageyamalizia huko huko
Kuna vikao vyao na wana nafasi zao kusuluhisha mambo yao ila kila muda mada ni hizo hizo as if hatuna matatizo yetu yanayotukabili

Vita ya PANZI, furaha ya KUNGURU. sisi watazamaji ni kama kunguru tu, panzi ni CHADEMA kwa CHADEMA na siyo vinginevyo.
 
yaani ccm mtuchagulie mwenyekiti na katibu hilo halitatokea..

pengine Wewe ni miongoni wa CHADEMA wanaofaidi ufujaji wa fedha zinazopigiwa kelele na MWIGAMBA, ila za mwizi ni arobaini, nadhani huu ni mwisho wa MBOWE na SLAA.
 
kwa mtu yeyote atakayejitokeza na kusema kwamba uongozi wa chadema haufai sisi wanachadema hatuwezi kumuelewa, yaani ni sawa sawa na mtu kujifanya ni baselona alafu anasema mesi asipangwe eti anaaribu mpira
 
Hakuna cha kunusuru chama hapa
Huwezi ukatoka nje ya utaratibu na then utegemee refa wa mchezo akuachie tuu kwa vile ukitolewa nje mchezo utaharibika
Na kupambana na refa unajua adhabu yake ni kutolewa kwa kadi nyekundu tuu na unatolewa nje ya uwanja kabisa
Sasa huko nje ya uwanja katafakari na ujione ni wapi ulikosea na kisha urudiufuate sheria za mchezo na sio kujiamulia tuu kucheza rough zako ambazo kisheria hazipo
Iwapo una malalamiko kuna waamuzi mpaka wa akiba na una meneja wako na kocha wako nenda kalalamike huko na nahodha wa mpira pia yupo lalamika kwake ya nini kulalamika kwa watazamaji ambao hawatakusaidia lolote

MBOWE na SLAA wenyewe na wafuasi wao wakuu humu JF kama Ben Saanane, molemo na wiegine wameshakubali matokeo mmebaki ambao hamjui lolote kuhusu abc za CHADEMA.
 
Vita ya PANZI, furaha ya KUNGURU. sisi watazamaji ni kama kunguru tu, panzi ni CHADEMA kwa CHADEMA na siyo vinginevyo.

Sawa hao panzi wapo waleni wakamateni muwale mtuachie mambo mengine yaongelewe maana unaweza kushuhudia mpambano wa panzi siku nzima na wewe kunguru una njaa haina maana mkamate panzi mhusika umle na uache kupiga piga kelele za njaa
Umeshaona CDM ina ukabila au ukanda au sijui ni chama cha familia nenda kwenye chama ambacho hakina hayo na uache kukaa na kutoa matamko kila kukicha na waandishi watasema na ambayo hukusema kisa kwa kuwa unajua kutumia chombo cha habari
Kulalamika ni dalili ya kuwa una makosa na unalalamika uonewe huruma na ukishaona kuwa mambo hayaendi hapa jiondoe mapema
We umekaa kwenye gema na unaliona linaanguka badala ya kuondoka unaishia kumlalamikia fulani ndio alichimba mtaro hapo gema litaenda na wewe na utaishia huko
 
kwa mtu yeyote atakayejitokeza na kusema kwamba uongozi wa chadema haufai sisi wanachadema hatuwezi kumuelewa, yaani ni sawa sawa na mtu kujifanya ni baselona alafu anasema mesi asipangwe eti anaaribu mpira

Mko wachache sana mliobaki kwa MBOWE na SLAA , na mwisho wenu ni uchaguzi ndani ya CHAMA.
 
Siku ya siku kitaeleweka

1383786_213731988801068_59941850_n.jpg
 
MBOWE na SLAA wenyewe na wafuasi wao wakuu humu JF kama Ben Saanane, molemo na wiegine wameshakubali matokeo mmebaki ambao hamjui lolote kuhusu abc za CHADEMA.

hatujui na wala hatutaki kujua na wala siasa za Mwigamba na akina Slaa hazitajenga barabara ya kwenda kijijini kwangu wala hazitatoa dawa kwenye zahanati ya kijiji changu wala wale wazee wa kijijini kwangu hawatapa huduma za bure za matibabu wala ule mradi wa maji wa kijiji changu hautakamilika
Niambie namna ya kutatua hayo ndipo nitakusikiliza na sio siasa za akina Slaa na Mwigamba
Sijui na sitaki kujua
 
Sawa hao panzi wapo waleni wakamateni muwale mtuachie mambo mengine yaongelewe maana unaweza kushuhudia mpambano wa panzi siku nzima na wewe kunguru una njaa haina maana mkamate panzi mhusika umle na uache kupiga piga kelele za njaa
Umeshaona CDM ina ukabila au ukanda au sijui ni chama cha familia nenda kwenye chama ambacho hakina hayo na uache kukaa na kutoa matamko kila kukicha na waandishi watasema na ambayo hukusema kisa kwa kuwa unajua kutumia chombo cha habari
Kulalamika ni dalili ya kuwa una makosa na unalalamika uonewe huruma na ukishaona kuwa mambo hayaendi hapa jiondoe mapema
We umekaa kwenye gema na unaliona linaanguka badala ya kuondoka unaishia kumlalamikia fulani ndio alichimba mtaro hapo gema litaenda na wewe na utaishia huko

Waambie SLAA na MBOWE, sisi wanachama hatuna shida na hicho chama chao cha ukoo, tunashida na matumizi mabaya ya fedha ambazo zinatokana na kodi za walalahoi, michnago ya bakuli kwenye mikutano ya hadhara ambazo hazina muainisho wa namna zilivyotumika. Hicho ndicho tunachokihoji, CHAMA kama CHAMA hata wakipokezana kama mbio za vijiti haituhusu.
 
Back
Top Bottom