Ulaghai kisiasa ni nguzo dhaifu sana katika mazingira ya siasa endelevu.
CHADEMA kilianzishwa kilaghai na kwa maana hiyo lazima uwe mlaghai kuweza kuwa kiongozi endelevu ndani yake, ndiyo maana wale walaghai ndiyo wanapandishwa vyeo na wasio walaghai wanatapata msukosuko mpaka uongozi wao utakoma.
Samson Mwigamba uzalendo ulimshinda ndiyo maana akaamua kutoa sauti kwa watanzania kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku na vyenzo zingine zitokanazo na pesa za wananchi ambazo zinatumiwa isivyostahili kikanuni na kikatiba na baadhi ya genge la watu wanaokifanya chama kama personal investment lakini kibaya kabisa watu waliojimilisha chama hawakupenda mtu wa Magu kuwa kiongozi wa eneo lao Arusha.
CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.
Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.
Waliojimilikisha chama baada ya kugundua kuwa hawana uwezo wa kushinda katika chaguzi za ndani wameamua kuahirisha chaguzi na sasa wanakuja na sababu wakisema kwa mujibu wa katiba, uchaguzi unatakiwa kufanyika 2014 kama vile hawakufahamu wakati wanasema uchaguzi utafanyika 2013.
Hawawezi kushinda katika mapambano yao ya kilaghai kwa sababu ulaghai siku zake ni arobaini na kikubwa zaidi, Watanzania wanafahamu ulaghai wao.
Waacheni wafu wazikane.