Babu…. Better this way!
Kuliko kuwa na chama ambacho Watanganyika tunaweka matumaini yetu hapo kumbe baadhi ya viongozi nyuma ya pazia wanashirikiana na CCM kutokufikia matakwa ya wananchi yenye mlengo wa kiukombozi.
Kila Chama kifutike ili siku tukianza tuanze upya, We seriously care less about CDM ya Mbowe. In a way hamuamini tukiwaambia kuna watu wanaipenda nchi kuliko vyama.
We have been played huh! No ninyi na Mbowe wenu ndio mmetuchezea kwa Miaka Mingi. Take this way: Kuna watu sababu ya uzalendo or being Naive wamepoteza maisha, wamepoteza mali au wameumizwa kwa kupigania maslahi ya nchi kumbe ninyi na mbowe wenu mnajua mnachofanya ikiwemo kuuza mipango na mikakati, Kuvujisha taarifa za vikao na hata whereabouts kwa watu walionekana ni threat, Kirahisi rahisi hivyo unataka watu kama hawa waone unachokiona “CDM ya mbowe ilikuwa na faida blah blah”?
Mr. Strategy, Strategy ilikuwa ni ipi sasa? Kuendelea kuisindikiza CCM hadi lini? Ushirika wa wachawi….
Sisi watanganyika tutafurahi CDM ikifutwa kuliko iwepo iolewe na CCM, Tunamsaliti namba moja wa wananchi ambaye ni CCM, na viwasaliti vya wananchi vikafu? Viaisiti na vichauma hatujitaji CDM kama msaliti!!!!! Mlichukue hili mliweke kwenye notibuku zenu.
Hamuwezi kuandika historia upya ili isometric mnavyotaka nyie. Hakuna kiongozi wa Chadema ( Mwenyekiti, Makamu Wake na Katibu Mkuu) ambae amesimama hadharani kukana mchango wa Mbowe kwa Chadema. Hakuna.
Hakuna mfuatiliaji makini wa siasa za nchi yetu ambae anaweza kusema kuwa Mbowe haku sacrifice sana kwa sababu ya chama chake na nchi yake.
Mbowe alipoingia kwenye Uenyekiti, Chadema haikuwa hii Chadema ambayo leo mnajifanya kuipenda.
Mbowe amekaa mahabusu mara nyingi tuu, ametumikia kifungo, amenyang'anywa mali zake, amegharamia chama chake kwa mwili na mali.
Mbowe ameandamana hata alipokuwa peke yake na binti yake. Wakati huo mashujaa wenu wamejifungia ndani au kwa masista. Na aliandamana kupinga mauaji. Mpambanaji Hilda Newton alijificha asionekane. Lissu alipokamatwa Mbeya, Mbowe alienda mara moja kuwa nae. Lissu akatuahidi kuwa kesi hiyo ataisimamia mwenyewe na atawashitaki binafsi waliompiga. Imefikia wapi?
Mbowe alikataa kupokea ruzuku kwa sababu alipinga matokeo ya uchaguzi na alihakikisha chama chake kinaendelea na shughuli zake.
Mbowe alipigania maisha ya Lissu. Mbowe alisimamia kesi ya Mdude mpaka akashinda. Watu wangapi wametoka jela kwa sababu ya mpango wa maridhiano ya Mbowe?
Heche amekiri wazi kuwa Mbowe ndie aliyemuingiza na kumlea katika siasa za upinzani. Na wako wengi kama yeye. Lissu amelea wangapi?
Unasema Mbowe amekuwa anavujisha siri za mikutano wakati ni Lissu ndie aliyempa swahiba wake Msigwa taarifa za mikutano wakati akishindana na Mbowe!
Kweli shukrani ya punda mateke. Lakini kuna uwezekano kuwa mnatumiwa na CCM kuhakikisha kuwa Mbowe anamalizika kisiasa. Sitashangaa kusikia kuwa mpo kwenye payroll.
Amandla....