PostGE2025 Samia: Hatua za kuunda Tume ya Maridhiano zimeanza

PostGE2025 Samia: Hatua za kuunda Tume ya Maridhiano zimeanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
"Maridhiano na wahalifu" inashangaza sana walisema yaliyotokea October ni vurugu na wahalifu walitoka nje ya nchi kutuharibia "tunu yetu ya amani". Baadae wakasema tulipewa burungutu za hela.
Wakaongezea nguvu iliyotumika ilikuwa sawa kabisa kuuwa binadamu 10,000 kwasababu walikuwa wanapora simu.
 
Keki ipi? Hilo unaloita genge lake walijitoa kwenye chama wakawaachia mkiendeshe mnavyotaka. Walifanya ambacho nafsi zao ziliwatuma kufanya. Sasa kazi kwenu maana hamna wa kumsingizia.

Mpango wa CCM ni wa kutawala nchi kwa namna yeyote. Hilo ndio hamuelewi. Kwa kukurupuka kwenu kumewapa miaka mitano mingine wakati wakiwakaba pumzi. Tuna miezi michache tu baada ya wao kurudi madarakani na pumzi imekata. Wanajua hamna kitu mataifa ya nje watakacho wafanyia zaidi ya kuwanyooshea vidole.

Mbowe aliwaambia kuwa atakaa pembeni lakini hamuishi kumuandama. Badala ya kupanga mta survive vipi miaka mitano ya kutoshiriki siasa nyie mmebaki kuwaandama waliokuwa wanachama wenzenu. Inaelekea mnaogopa kupambana na CCM.

Mbowe, Chaumma n.k. sio maadui wenu. Kaeni nao muone mtafanikisha vipi adhma yenu ya kuitoa CCM madarakani. Hiyo ndio inatakiwa iwe focus na sio kingine. Mbowe alipambana alivyojua yeye sasa ni zamu yenu kutuonyesha kuwa njia yenu italeta mafanikio. Mpaka sasa hamna mlicho fan ikiwa. Mlisema uchaguzi haufanyiki lakini "umefanyika" na serikali ya CCM iko madarakani pamoja na bunge lake. Na itakuwa hivyo mpaka "uchaguzi" ujao.

Amandla...
Genge liko wapi baada ya kuondoka CHADEMA?

Huo mpango wa kutawala milele unawezeshwa na hao walamba asali, wanachotaka CCM ni legitimacy ya uchaguzi ambayo Mbowe, Zitto na Lipumba wamekuwa wakiwapa.

Kama wameshapata miaka 5 mingine, hizi tume ni za kazi gani? Nini kinawasumbua na dola wamekamata?

CCM kutoka madarakani sio process ya mtu au mwaka mmoja, we have a long way to go, ila mbinu za kina Mbowe na wenzake hakuna sehemu zingewapeleka. Leo CHADEMA ingekuwa dhaifu kama unavyodai serikali isingetumia nguvu kupambana nayo.

Umeona wapi kiongozi wa TLP ana kesi mahakamani?
 
20. De Klerk ali ridhia masharti yake kwa sababu alikuwa global icon na lolote lingempata akiwa ndani serikali yake ingeathirika vibaya sana.
Shinikizo la kimataifa (vikwazo vya kiuchumi),Hali ya kisiasa ya ndani ya nchi vilichangia hilo.... mengine ni nyongeza tu.
 
Naunga mkono kulirudisha taifa na nchi katika Umoja...

Lakini ni lazima tuzingatie utaratibu wa kupata hicho tunachokitaka...

Tunachotakiwa kuunda sio TUME YA MARIDHIANO.

Chombo kinachotakiwa kuundwa ni tume ya kimahakama inayoitwa kwa jina halisi la TUME YA UKWELI NA MARIDHIANO (TRUTH & RECONCILIATION COMMISSION)...

Na kama yuko serious kweli, aachane mara Moja na kile alichofanya, kuunda Tume ya Jaji Chande. Huo ni uchafu na ni upuuzi 100%...

TRUTH AND RECONCILIATION COMMISSION hii ndiyo itakayotafuta ukweli wa kilichotokea, kujua na kuwatambua waliohusika na mauaji, kuwatambua walioathirika na matukio hayo ya mauaji, kupendekeza hatua za kuchukua na namna ya kwenda mbele...

Katiba mpya na mengine ni moja ya Suluhu au majibu ya matatizo ya nchi na taifa letu....

Lakini hatuwezi kurukia kuanzia kufanya suluhu kabla ya kuujua ukweli wa sababu zilizotufikisha hapa mpaka serikali inaua raia wake inayojidai kuwaongoza zaidi ya 10,000...!

..Nadhani hata neno Maridhiano lisitumike tena.

..Maridhiano ni dhana ambayo imetumika vibaya, na imeingia najisi.

..Tunahitaji UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI. Sio Maridhiano.
 
Genge liko wapi baada ya kuondoka CHADEMA?

Huo mpango wa kutawala milele unawezeshwa na hao walamba asali, wanachotaka CCM ni legitimacy ya uchaguzi ambayo Mbowe, Zitto na Lipumba wamekuwa wakiwapa.

Kama wameshapata miaka 5 mingine, hizi tume ni za kazi gani? Nini kinawasumbua na dola wamekamata?

CCM kutoka madarakani sio process ya mtu au mwaka mmoja, we have a long way to go, ila mbinu za kina Mbowe na wenzake hakuna sehemu zingewapeleka. Leo CHADEMA ingekuwa dhaifu kama unavyodai serikali isingetumia nguvu kupambana nayo.

Umeona wapi kiongozi wa TLP ana kesi mahakamani?
Muda ni mwalimu mzuri. Si nyinyi ndio mnaosema kuwa NRNE ilianza chini ya Mbowe? Mbowe aliposhindwa uchaguzi Lissu na wenzake wakaibeba jumla.

Tofauti na mnavyosema, Chadema ya Mbowe iliandamwa kuliko hii ya Lissu. Viongozi wake sio tu walishtakiwa bali walihukumiwa vifungo vya kukaa jela. Viongozi wake walipotea na yeye mwenyewe Mbowe aliandamwa mpaka kwenye biashara zake. Muda wote huo hakutetereka.

Hiyo Chadema imara mnayojisifia ilijengwa na Mbowe. Hata baada ya kuondokewa na viongozi wenzake Mbowe aliendelea kuijenga. Viongozi wote wa vyama vilivyopitia mitikisiko kidogo viliufyata. Sio Chadema. Kwenye hilo mnapaswa kumshukuru sio kumbeza.

Amandla...
 
Shinikizo la kimataifa (vikwazo vya kiuchumi),Hali ya kisiasa ya ndani ya nchi vilichangia hilo.... mengine ni nyongeza tu.
Mnajidanganya. Hayatatokea. Hata Kenyatta na Ruto walipelekwa ICC kutokana na mauaji ya 2007-2008 lakini wakaishia kuwa marais. Hamna nchi itakayoiwekea vikwazo vya uchumi Tanzania. Unfortunately, nchi yetu haina umuhimu kwa uchumi wa dunia kiasi hicho. Mnajidanganya tu na hayo mambo ya ICC na vikwazo vya EU. Trump ndio kabisa hatafanya kitu. Inabidi kuwa realistic na kujipanga kwa 2029 na 2030. Chadema wangepigana ili hili zuio la kufanya siasa liondolewe. Hilo linaweza kufanywa ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa kuna demokrasia. Na Chadema haitafutwa.

Amandla...
 
Mpango wa ccm kutawala kwa aina yoyote tayari umeshakutana na pigo la kwanza Mo29. Ni juu ya cdm kukaza kamba hakuna na maridhiano ya kitapeli tena. Ni bora cdm isiwepo kuliko kuwepo huku ikiburuzwa kwa siasa za kilaghai na ccm.

Na kwa kukusaidi tu, kwa sasa cdm ndio imezidi kuimarika baada ya kugomea uchaguzi wa kihuni. Na kwa msisitizo huku kujitoa muhanga kwa cdm ndio kutaleta mabadiliko mengi ambayo chama kitakachofaidika ni cdm zaidi kuliko vyama vingine vyote. No pain no gain, kwenye uchaguzi huu cdm wamecheza heko. Ule upuuzi wa cdm ya Mbowe umehamia Chauma, na matokeo ya kuburuzwa yamewaathiri moja kwa moja. Tuko tayari cdm isishiriki hata miaka 10 hadi reforms za kweli na katiba ipatikane, kisha tuingie uwanjani ndio mtafurahia show.
Sawa. Yetu macho.

Amandla...
 
Mnajidanganya. Hayatatokea. Hata Kenyatta na Ruto walipelekwa ICC kutokana na mauaji ya 2007-2008 lakini wakaishia kuwa marais. Hamna nchi itakayoiwekea vikwazo vya uchumi Tanzania. Unfortunately, nchi yetu haina umuhimu kwa uchumi wa dunia kiasi hicho. Mnajidanganya tu na hayo mambo ya ICC na vikwazo vya EU. Trump ndio kabisa hatafanya kitu. Inabidi kuwa realistic na kujipanga kwa 2029 na 2030. Chadema wangepigana ili hili zuio la kufanya siasa liondolewe. Hilo linaweza kufanywa ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa kuna demokrasia. Na Chadema haitafutwa.

Amandla...
Kujipanga kwa 2029 na 2030 ndo kukoje?
 
Kujipanga kwa 2029 na 2030 ndo kukoje?
Chaguzi zijao zitafanyika miaka hiyo. Ni nafasi nzuri kwa vyama vya upinzani maana ndani ya CCM patakuwa na waliojipanga kushika uongozi na nchi. Hapatakuwa na incumbent wakati huo.

Hahaaaa you are so naive!

Kwani huko nyuma hakujawahi kutokea kutokuwepo kwa incumbent?

1995!hakukuwa na incumbent.

2005 hakukuwa na iincumbent.

2015 hakukuwa na incumbent.

Tatizo siyo incumbency.

Tatizo ni katiba mbovu na sheria mbaya za uchaguzi.

Kila mara huwa nasema hapa kamwe haitowezekana kwa chama kingine cha kisiasa kushinda chaguzi ambazo chombo kinachoendesha chaguzi hizo kimeundwa na CCM.

Juzi tu hapa tumeona kuwa tarehe 20 Oktoba hakukufanyika uchaguzi.

Lakini pia tukaona kuwa tume ya uchaguzi iliyoundwa na Samia ikamtangaza Samia kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi kwa takwimu ambazo ziliichekesha dunia nzima.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, ambaye aliteuliwa na Samia, alimtangaza Samia kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 97.6 ambazo ni sawa na kura milioni 31 na kitu.

Kila mwenye macho anajua kuwa hakuna watu milioni 31 waliojitokeza siku hiyo kumpigia kura Samia. Hakuna.

Katika hali ya mazingira bora ya uchaguzi, pangekuwepo na tume huru, hayo matokeo ya huo uchaguzi yangefutwa.

Samia mwenyewe yupo on record akisema kwamba hata wasiposhinda uchaguzi, CCM ndo itatangazwa mshindi. Hii ni kweli alisema na si kumlisha maneno mdomoni.

Sasa unasema hao wapinzani wajipange kwa 2029 na 2030.

Wajipange chini ya mazingira haya haya?

Wewe kwa akili yako unayaona haya mazingira yanatoa fursa sawa kwa washindani wote?
 
Cdm ya Lisu inaendeshwa kitaasisi na sio mtu.
Sawa. Haya ni maneno tu. Hata taasisi inatakiwa kuwa na kiongozi ama sivyo inakuwa kama Animal Farm. Mpaka sasa hivi hakuna anayeweza kuibeba CDM nje ya Lissu.
Unaongelea cdm ya Mbowe kama tajiri, lakini cdm chini ya Mbowe ilikuwa inaenda kudumaa maana tayari alitaka kujiona bila hela zake chama kinakufa. Cdm ya Lisu hata iwe nia shilingi 10m huo ndio uhalisia, kuliko kuwa na 100m za kificho toka kwa mafisadi.
Mnajidanganya. Mbowe alitumia pesa zake, za ruzuku, za wachangiaji wengine kukifikisha chama mahali ambapo Lissu alikirithi.
Hao akina Lisu walimkimbia Magufuli na sio Samia, na bado wangeweza kurudi kwani hawakufukuzwa.
Sasa nini kiliwazuia kurudi? Na kwa nini Lissu alimtaka Samia amuhakikishie uzima wake walipokutana Brussels? Bila Mbowe wangekuwa watu wa Club house mpaks leo.
Unataka kuonyesha ni Mbowe ndio aliwarudisha, kwani yeye ndio aliawaagiza wakimbie? Hao waliofungwa kwa uonevu ilikuwa ni haki yao kuachiwa, na hata wasingeachiwa vifungo vya hukumu zao za uonevu vingekuwa vimesha, maana hawakuwa wamefungwa maisha.
Mbowe na chama chake ndio waliwawezesha kurudi. Kwa hao waliokuwa na kesi za kipuuzi ulikuwa unataka wakae tu ndani mpaka hapo serikali itakapojisikia kuwaachia. Ni heri mtu ahukumiwe kifungo kuliko kuwekwa rumande. Wote tumeona yaliyowapata ma shehe wa uamsho.
Unauliza sasa hivi cdm iko wapi wakati chama kimezuiwa kufanya shughuli za kisiasa! Ilitakiwa kisiwe kimezuiwa kisha uje na hizi porojo zako.
Mbona hata CDM ya Mbowe ilizuiwa kufanya siasa lakini tulikuwa tunaisikia. Walizuiwa kufanya mikutano Bawacha wakawa wanafanya jogging. Wakawa wanafanya mikutano ya ndani pamoja na kukamatwa kila kukicha. Na walifanya yote hayo bila ruzuku.
Hakuna aliyetengwa acha upotoshaji wa kijinga, ukiona mtu anasema ametemgwa ujue ni team Mbowe wanataka wabembelezwe baada ya boss wao kupigwa chini.
Avaae kiatu ndio anajua kinapombana. Watu walikuwa wanashambuliwa kwa matusi na hata kipigo kila wakati bila uongozi kuchukua hatua. Na wameendelea kuandamwa hata pale walipoamua kuondoka. Chuki ya CDM dhidi ya Chaumma ilikuwa kubwa kuliko dhidi ya CCM. Cowards siku zote wanakimbilia kumuonea yule ambae hana uwezo wa kuwarudishia. Ndivyo ilivyo kwa CDM ya sasa.
Na kwa kukusaidia tu, Mbowe hakutaka uchaguzi uwe wazi vile, bali alizidiwa nguvu na team Lisu kwani hao hawakuwa tayari kwa matokeo ya kihuni. Na iwapo team Lisu wasingekaza Mbowe leo hii bado angekuwa mwenyekiti.
Kwa maelezo ya Katibu Mkuu wa CDM, chama chao hakikua na pesa za kufanya Mkutano Mkuu. Lissu alikataa kuchangia. Mbowe ndie aliyeokoa Mkutano kwa kuchangia milioni 250. Na hata wakati wa uchaguzi shutuma zote za kijinga za kuwa kuna pesa chafu zilionyeshwa kuwa ni za uongo mtupu. Nia ya wakina Lissu ilikuwa ni vurugu zitokee ili waseme wameibiwa. Lakini sekretariat ya Mbowe ikasimama kidete kuhakikisha kuwa mchakato unakuwa wa wazi na haki. Matokeo yalipotangazwa Mbowe akakubali kushindwa na kumpisha Lissu. Lakini bado team ya Lissu ikaendelea kuandama wale ambao walikuwa team Mbowe. Hilo wala hawakujificha.

Team Lissu iliahidi kuwa itaendesha chama kwa uwazi kuliko alivyokuwa akifanya Mbowe. Niambie mara ya mwisho taarifa ya mapato na matumizi waliitoa lini? Waliacha kufanya hivyo hata kabla ya kuwekewa zuio la kufanya siasa. Mimi sikushangazwa maana hamna hata taarifa moja iliyotolewa ya michango waliyochangiwa. Kuanzia ule wa kununua gari hadi leo.

Shida yenu mmegeuka kuwa cult. Anachofanyiwa Lissu pamoja na chama chake sio sawa kabisa. Lakini nanyi mnachowafanyia wanaotofautiana nanyi sio sawa.

Amandla.
 
Hahaaaa you are so naive!
I plead guilty.
Kwani huko nyuma hakujawahi kutokea kutokuwepo kwa incumbent?

1995!hakukuwa na incumbent.

2005 hakukuwa na iincumbent.

2015 hakukuwa na incumbent.
Pamoja na kuwa hapakuwa na incumbent, CCM ilikuwa na viongozi wenye nguvu za kuwaunganisha nyuma ya mgombea mmoja. Baada tu ya kupata mgombea, wote waliungana isipokuwa 2015 ambapo mgombea mmoja akaonyesha wazi kutoridhika kwaje na mchakato. Nguvu za ziada zilitumika mpaka mgombea wa CCM kutangazwa mshindi kwa asilimia ndogo kuliko wakivyo zoea.
Tatizo siyo incumbency.

Tatizo ni katiba mbovu na sheria mbaya za uchaguzi.
Tatizo sio Katiba Mbovu na Sheria. Tatizo ni kutokuwa na taasisi ambazo ziko tayari kuhakikisha kuwa Katiba na sheria zinafuatwa. Kuna wanawake 19 wamekaa miaka mitano Bungeni ingawa ni wazi kabisa kuwa Katiba ilikuwa imekiukwa.
Kila mara huwa nasema hapa kamwe haitowezekana kwa chama kingine cha kisiasa kushinda chaguzi ambazo chombo kinachoendesha chaguzi hizo kimeundwa na CCM.
Hilo sio kweli. Vyama vya upinzani vimekuwa vinashinda chaguzi pamoja na figisu figisu za CCM. Figisu figisu hizo zipo siku zote. Kinachotokea sasa hivi ni kuwa CCM inataka ishinde kwa zaidi ya asilimia tisini na taasisi za kusimamia haki zinaangalia tu.
Juzi tu hapa tumeona kuwa tarehe 20 Oktoba hakukufanyika uchaguzi.

Lakini pia tukaona kuwa tume ya uchaguzi iliyoundwa na Samia ikamtangaza Samia kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi kwa takwimu ambazo ziliichekesha dunia nzima.
Haikuanza leo. Katika uchaguzi wa serikali za mitaa CCM ilishinda kwa asilimia 100. Hqpo tatizo sio kuteuliwa na Rais bali ni wenye dhamana kukataa kutekeleza wajibu wao. Secretary of State wa Georgia ingawa alikuwa Republica alikataa kata kata kumtafutia kura za wizi Trump. Makamu wake alikataa vile vile kuahirisha kutangaza kura alizopata Biden. Kama watu hawana integrity hata muwe na Katiba nzuri vipi mtaendelea kuchezewa foul.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, ambaye aliteuliwa na Samia, alimtangaza Samia kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi kwa kupata asilimia 97.6 ambazo ni sawa na kura milioni 31 na kitu.
Kwa hiyo? Mwenye kosa hapo ni Samia au yule aliyeshindwa kusema kuwa hii haiwezekani na kukataa kutangaza?
Kila mwenye macho anajua kuwa hakuna watu milioni 31 waliojitokeza siku hiyo kumpigia kura Samia. Hakuna.
Sawa.
Katika hali ya mazingira bora ya uchaguzi, pangekuwepo na tume huru, hayo matokeo ya huo uchaguzi yangefutwa.
Suala sio Tume bali integrity ya wanaounda hiyo Tume. Hakimu anapokubali kuahirisha kesi kwa miaka kibao, anakuwa yeye ana kosa na sio kuwa sheria ni mbovu. Spika anapowatambua wabunge ambao hawajapitishwa na chama chao, anaonyesha kukosa integrity na sio ubovu wa Katiba.
Samia mwenyewe yupo on record akisema kwamba hata wasiposhinda uchaguzi, CCM ndo itatangazwa mshindi. Hii ni kweli alisema na si kumlisha maneno mdomoni.
Kama alisema hivyo ni kwa sababu alijua kuwa watendaji wake ni compliant.
Sasa unasema hao wapinzani wajipange kwa 2029 na 2030.

Wajipange chini ya mazingira haya haya?

Wewe kwa akili yako unayaona haya mazingira yanatoa fursa sawa kwa washindani wote?
Wapinzani hawana alternative bali kuendelea kupambana. Ilichukua zaidi ya miaka 60 kukiondoa chama tawala cha Mexico. Hivyo hivyo India. Congress walijua watatawala milele lakini wako wapi sasa. Hakuna short cuts, ni kuendelea kupambana. Hata kama itachukua miaka 20 mingine. Ukweli ni kuwa iko siku CCM itaondoka madarakani. Ni wajibu wa upinzani makini kuwa tayari kuwarithi watakapoondoka. Huu ni wakati wa kukaa na wananchi kuwaeleza kinagha ubaga mapungufu yaliyopo katika nchi yetu na kuwa hakikishia kuwa watakapo pokea kijiti watahakikisha Katiba bora inapatikana pamoja na taasisi imara za kuisimamia. Majibu mepesi mepesi ya mitandaoni haitawafikisha mbali.

Amandla...
 
Sawa. Haya ni maneno tu. Hata taasisi inatakiwa kuwa na kiongozi ama sivyo inakuwa kama Animal Farm. Mpaka sasa hivi hakuna anayeweza kuibeba CDM nje ya Lissu.

Mnajidanganya. Mbowe alitumia pesa zake, za ruzuku, za wachangiaji wengine kukifikisha chama mahali ambapo Lissu alikirithi.

Sasa nini kiliwazuia kurudi? Na kwa nini Lissu alimtaka Samia amuhakikishie uzima wake walipokutana Brussels? Bila Mbowe wangekuwa watu wa Club house mpaks leo.

Mbowe na chama chake ndio waliwawezesha kurudi. Kwa hao waliokuwa na kesi za kipuuzi ulikuwa unataka wakae tu ndani mpaka hapo serikali itakapojisikia kuwaachia. Ni heri mtu ahukumiwe kifungo kuliko kuwekwa rumande. Wote tumeona yaliyowapata ma shehe wa uamsho.

Mbona hata CDM ya Mbowe ilizuiwa kufanya siasa lakini tulikuwa tunaisikia. Walizuiwa kufanya mikutano Bawacha wakawa wanafanya jogging. Wakawa wanafanya mikutano ya ndani pamoja na kukamatwa kila kukicha. Na walifanya yote hayo bila ruzuku.

Avaae kiatu ndio anajua kinapombana. Watu walikuwa wanashambuliwa kwa matusi na hata kipigo kila wakati bila uongozi kuchukua hatua. Na wameendelea kuandamwa hata pale walipoamua kuondoka. Chuki ya CDM dhidi ya Chaumma ilikuwa kubwa kuliko dhidi ya CCM. Cowards siku zote wanakimbilia kumuonea yule ambae hana uwezo wa kuwarudishia. Ndivyo ilivyo kwa CDM ya sasa.

Kwa maelezo ya Katibu Mkuu wa CDM, chama chao hakikua na pesa za kufanya Mkutano Mkuu. Lissu alikataa kuchangia. Mbowe ndie aliyeokoa Mkutano kwa kuchangia milioni 250. Na hata wakati wa uchaguzi shutuma zote za kijinga za kuwa kuna pesa chafu zilionyeshwa kuwa ni za uongo mtupu. Nia ya wakina Lissu ilikuwa ni vurugu zitokee ili waseme wameibiwa. Lakini sekretariat ya Mbowe ikasimama kidete kuhakikisha kuwa mchakato unakuwa wa wazi na haki. Matokeo yalipotangazwa Mbowe akakubali kushindwa na kumpisha Lissu. Lakini bado team ya Lissu ikaendelea kuandama wale ambao walikuwa team Mbowe. Hilo wala hawakujificha.

Team Lissu iliahidi kuwa itaendesha chama kwa uwazi kuliko alivyokuwa akifanya Mbowe. Niambie mara ya mwisho taarifa ya mapato na matumizi waliitoa lini? Waliacha kufanya hivyo hata kabla ya kuwekewa zuio la kufanya siasa. Mimi sikushangazwa maana hamna hata taarifa moja iliyotolewa ya michango waliyochangiwa. Kuanzia ule wa kununua gari hadi leo.

Shida yenu mmegeuka kuwa cult. Anachofanyiwa Lissu pamoja na chama chake sio sawa kabisa. Lakini nanyi mnachowafanyia wanaotofautiana nanyi sio sawa.

Amandla.
Lisu ana nyota kali ya mvuto hilo halina mjadala. Mbowe alitumia pesa zake ili apate uhalali wa kufia kwenye hicho kiti cha uenyekiti. Hata hivyo pia alifaidika na cheo hicho wala usitake kuonyesha ni hasara tu alikuwa anapata. Na kama angepata hasara nina hakika angegoma kutumia hizo pesa zake kama alivyozira sasa.

Hiyo ya kina Lisu kurudi, wangerudi tu maana Magufuli ndio walimkimbia. Samia alikuwa anasaka sifa tu, usichanganye waliokimbia na waliofukuzwa. Watu waliokuwa wanashambuliwa ni mamluki, na wamejiweka wazi baada ya kuhama na kuanza kuichafua cdm. Walikuwa wanataka kuleta ule upuuzi ambao Lipumba aliuigiza CUF, na cdm ya Lisu wasingesimama na hao wapuuzi waliohamia Chauma wangevuna mabua.

Kuwa Mbowe alichangia na Lisu akagoma, kwani ulikuwa ni uchaguzi wa Mbowe na Lisu ama wa cdm? Kama Mbowe alitoa hiyo 250m huo ni utashi wake. Muda pekee ambao cdm haikuwa na ruzuku ni kabla ya 2010 chini ya Mbowe, bada ya hapo cdm imekuwa na ruzuku ya viwango tofauti tofauti kutokana na kiwango cha kura. Kuhusu kuwa na uwazi kuhusu mapato, Lisu kachaguliwa January, kaenda jela miezi miwili mbele, na miezi minne mbele chama kikazuiwa kufanya shughuli za kisiasa. Jambo pekee walilofanya cdm kwa kipindi hicho ilikuwa ni operesheni ya NRNE, nayo ilifanyika kwa ufanisi hadi cdm inazuiwa kufanya shughuli zake. Hakuna popote unaweza kuipima cdm ya Lisu nje ya hiyo miezi miwili aliyokalia kiti akiwa uraiani. Ukitaka kupima uongozi wa Lisu ni iwapo atatoka na kufanya shughuli za kisiasa, sio sasa chama kimezuiwa, na yeye yuko jela.

Unasema cdm ya Mbowe ulikuwa unaona hata Bawacha wakifanya jogging, kuna utofauti wa cdm ile na sasa, wakati ule cdm haukuzuiwa na mahakama kufanya shuguli za kisiasa, bali walitakiwa kufanya mikutano ya ndani na maeneo uliyopo.

Uwazi wa cdm, ni uwazi unapewa huku jf ama kwenye vikao vya ndani? Na je sasa hivi unatoa taarifa za mapato na matumizi kutokana na pesa gani, kama ni ruzuku ilishazuiwa, na chama hakifanyi siasa. Pesa za gari zilikuwa za umma ama za Lisu kutoka michango ya wapenzi wake? Kama ni pesa binafsi za Lisu ulitaka akupe ripoti hadharani?
 
Hamuwezi kuandika historia upya ili isometric mnavyotaka nyie. Hakuna kiongozi wa Chadema ( Mwenyekiti, Makamu Wake na Katibu Mkuu) ambae amesimama hadharani kukana mchango wa Mbowe kwa Chadema. Hakuna.
Hakuna mfuatiliaji makini wa siasa za nchi yetu ambae anaweza kusema kuwa Mbowe haku sacrifice sana kwa sababu ya chama chake na nchi yake.
Mbowe alipoingia kwenye Uenyekiti, Chadema haikuwa hii Chadema ambayo leo mnajifanya kuipenda.

Mbowe amekaa mahabusu mara nyingi tuu, ametumikia kifungo, amenyang'anywa mali zake, amegharamia chama chake kwa mwili na mali.

Mbowe ameandamana hata alipokuwa peke yake na binti yake. Wakati huo mashujaa wenu wamejifungia ndani au kwa masista. Na aliandamana kupinga mauaji. Mpambanaji Hilda Newton alijificha asionekane. Lissu alipokamatwa Mbeya, Mbowe alienda mara moja kuwa nae. Lissu akatuahidi kuwa kesi hiyo ataisimamia mwenyewe na atawashitaki binafsi waliompiga. Imefikia wapi?

Mbowe alikataa kupokea ruzuku kwa sababu alipinga matokeo ya uchaguzi na alihakikisha chama chake kinaendelea na shughuli zake.

Mbowe alipigania maisha ya Lissu. Mbowe alisimamia kesi ya Mdude mpaka akashinda. Watu wangapi wametoka jela kwa sababu ya mpango wa maridhiano ya Mbowe?

Heche amekiri wazi kuwa Mbowe ndie aliyemuingiza na kumlea katika siasa za upinzani. Na wako wengi kama yeye. Lissu amelea wangapi?
Unasema Mbowe amekuwa anavujisha siri za mikutano wakati ni Lissu ndie aliyempa swahiba wake Msigwa taarifa za mikutano wakati akishindana na Mbowe!
Kweli shukrani ya punda mateke. Lakini kuna uwezekano kuwa mnatumiwa na CCM kuhakikisha kuwa Mbowe anamalizika kisiasa. Sitashangaa kusikia kuwa mpo kwenye payroll.

Amandla....
HAHAHA!!!!
 
Suala sio Tume bali integrity ya wanaounda hiyo Tume. Hakimu anapokubali kuahirisha kesi kwa miaka kibao, anakuwa yeye ana kosa na sio kuwa sheria ni mbovu. Spika anapowatambua wabunge ambao hawajapitishwa na chama chao, anaonyesha kukosa integrity na sio ubovu wa Katiba.

Amandla...
Huwezi ukapata watu wenye integrity palipo na mgongano wa kimaslahi.

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais hawezi kuteua watu kwenye hiyo tume ambao anajua hawatalinda maslahi yake.

Hivi unadhani CCM wanaweza kushiriki uchaguzi ambao utaendeshwa na tume ya uchaguzi ambayo imeundwa na CHADEMA/ Tundu Lissu?

Hivyo, tatizo ni utaratibu wote unaounda hiyo tume.

Na kwa vile tume ni watu na si lidubwasha flani, tume ni tatizo kuanzia juu mpaka chini, nje mpaka ndani.

Huwezi kunishawishi kwamba huyo Jaji Mwambengele hayuko beholden kwa Samia.

Huwezi kupata integrity palipo na conflict of interest.

Ndo maana sisi wengine kwa muda mrefu sana sasa tumekuwa tukilipigia kelele hilo suala.

Na uki turn tables kwamba wapinzani ndo wawe wanaunda hiyo tume halafu sheria iwe ni kwamba neno la hiyo tume kuhusu nani kashinda ni final, na kwamba hakuna legal recourse, CCM hawatokubali kushiriki kwenye chaguzi. Jiulize kwa nini?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka 2026 Serikali imejipanga kujenga umoja wa kitaifa ambapo mchakato wa kuunda Tume ya Maridhiano tayari umeanza na Serikali itashirikiana na wadau wote ili kukubaliana muundo wa Tume hiyo.

Katika hotuba yake ya kuaga mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026 Ikulu Zanzibar, Samia amesema "Mwaka 2025 pamoja na mafanikio tuliyoyapata tulipitia pia changamoto na mitihani iliyotugusa sote tutakumbuka kuwa mwezi octoba mwaka huu tulipitia nyakati ngumu zilizohitaji subira mshikamano na uzalendo kwa dhati kabisa ninavishukuru Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama nchini na Wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kudumisha amani umoja na mshikamano wa taifa letu."

“Tumeweza kuuthibitishia ulimwengu kwamba Tanzania ni taifa imara, himilivu na lenye kujitahidi kushughulikia changamoto zake. Tunapouanza mwaka 2026 Serikali imejipanga kujenga umoja wa kitaifa nchini hatua za kuunda Tume ya Maridhiano zimeanza kuchukuliwa, Serikali itashirikiana na wadau wote katika kukubaliana kuhusu muundo wa tume aina ya wajumbe, majukumu yao na muda wa kazi wa tume hiyo"
Hiyo tume labda mwwnyekiti awe warioba
Makamu awe lema
Katibu awe mbowe
Mjumbe awe lisu
Makamu katibu awe gwajima
 
Back
Top Bottom