vifo maandamano tanzania

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Dkt. Kijo-Bisimba: Ule Haukuwa Uchaguzi, siku tumeruhusiwa kutoka tulikuta maboksi ya uchaguzi mitaani sijui yalikuwa na kura au la!

    Mkurugenzi mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mwanaharakati mkongwe, Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, amehoji uhalali wa uchaguzi, akisema alichokiona siku hiyo hakikidhi viwango vya uchaguzi. Akizungumza Septemba 15, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani...
  2. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Padri Kitima: Wananchi ndio waongoze mchakato wa Maridhiano baada ya kukubali tatizo lililopo kitaifa

    Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema dhana ya maridhiano nchini inapaswa kuanza kwa kukiri na kukubali ukweli kuhusu matatizo yaliyopo. Akifafanua kuhusu maana ya maridhiano, amesema neno hilo linapaswa kueleweka kwa upana, akitumia mfano...
  3. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mwananchi amwambia Ado Shaibu, wewe upo Bungeni unachukua posho wakati ndugu zetu walipotea. Wewe unajisikiaje?

    Katika mkutano wa hadhara wa Chama cha ACT Wazalendo wa Septemba 11, 2026, uliofanyika Kata ya Dutwa, Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu, mwananchi Fulani amesimama na kumhoji Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, kuhusu sababu za yeye kuendelea kubaki...
  4. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Sheikh Summercliff: Masheikh mnaotaka tuombee El Niño bila kutubu damu iliyomwagika Oktoba 29 bila hatia, ni unafiki

    Sheikh Summercliff amewakosoa baadhi ya viongozi wa dini waliojitokeza na kutoa wito wa kuombea taifa kutokana na changamoto ya El Niño, akisema maombi hayo yanapaswa kuanza kwa kutubu na kuwakumbuka waathirika wa matukio ya Oktoba 29. Amesema damu ya watu waliopoteza maisha, wakiwemo watoto...
  5. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Tume ya Jaji Lila: Tutachunguza nguvu iliyotumika kudhibiti ghasia za Oktoba 29

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Jaji Shaban Ally Lila, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa Tume hiyo inaenda kutekeleza kazi iliyoelekezwa ya kuchunguza na kubaini wahusika wa ghasia za...
  6. K

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Kihongosi: Wanasiasa acheni kutumia Majeraha ya Oktoba 29 kujinufaisha Kisiasa

    Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (Itikadi, Uenezi na Mafunzo), Kenani Kihongosi, amewataka wanasiasa na vyama vya siasa nchini kuacha kutumia matukio ya Oktoba 29 kama ajenda ya kujijenga kisiasa, badala yake wawe wavumilivu na kusubiri matokeo ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Rais...
  7. Mindyou

    JamiiForums Tanzania Padri Kitima: Bado hatujamsikia Rais akisema neno 'Samahani' kwa yaliyotokea

    Wakuu, Padri Kitima leo kwenye mahojiano maalum amesema japo Rais alikiri kutokea kwa changamoto na kusema matukio hayo hayakuwa ya kawaida na hayatapaswa kujirudia, bado hajatamka neno "samahani" kwa niaba ya watendaji wa serikali yake. "Ni kweli Mheshimiwa Rais alisema yaliyotokea...
  8. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Lissu adai kunyimwa nakala ya hotuba ya Jaji Chande

    Shauri la Kikatiba Na.7300/2026 lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) na wenzake linaendelea kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji...
  9. R

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Wasira: Vurugu zilifanyika usiku Oktoba 29 wakati sehemu kubwa ya nchi walishapiga kura

    Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ametetea uhalali wa serikali iliyopo madarakani na matokeo ya uchaguzi mkuu, akieleza kuwa vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi zilianza tarehe 29 usiku baada ya wananchi wengi kote nchini kuwa tayari wameshapiga kura...
  10. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Asasi za Kiraia (AZAKI): Serikali ya Tanzania imeilipa kampuni ya BGR Group Tsh. Bilioni 7.886 kuisafisha taswira ya nchi

    Wawakilishi wa Asasi za Kiraia (AZAKI) Tanzania, Julai 16, 2026, wamesema kumekuwa na jitihada za kutumia njia za mkato kushughulikia changamoto za kisiasa na kiutawala nchini badala ya kuzingatia misingi ya katiba na utawala wa sheria. Wamedai kuwa kumekuwa na matukio ya utekaji, mateso...
  11. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Mchungaji Kimondo: Tulidhani yaliyotokea Oktoba 29, yangekuwa mwisho, lakini baada ya hapo vitendo vya utekaji vinaendelea

    Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, amesema matukio ya utekaji nchini yameanza kuwa jambo la kawaida, akieleza kuwa yanapaswa kukemewa kwa nguvu zote. Amesema ingawa waathirika wa matukio hayo pamoja na familia, marafiki na majirani zao huumia, bado...
  12. The Palm Beach

    JamiiForums Tanzania Brussels na Washington zazungumza lugha moja juu ya Tanzania na Mauaji ya Oktoba 29, Uvunjifu wa Haki za Binadamu na Kuminywa kwa Demokrasia

    Na Amani K. Mrope | Ofisi ya Washington Tatizo Siyo Pesa. Tatizo ni Tanzania Kuingizwa Rasmi Kwenye Rekodi mbaya za Kimataifa. Kuna nyakati ambazo nchi hupoteza fedha. Na kuna nyakati ambazo nchi hupoteza imani ya dunia. Fedha zinaweza kurejea. Lakini imani ni vigumu zaidi kuijenga upya...
  13. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Heche: Polisi hawana weledi hata chembe, wanatuhumiwa kuteka na kuua, na ndio waliohusika kuua Oktoba 29 na 30

    Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amelitupia lawama kali Jeshi la Polisi nchini akidai kuwa limepoteza weledi na kugeuka kuwa chombo kinachotumika kisiasa dhidi ya wapinzani. Akizungumza Juni 17, 2026 katika mahojiano na Kituo cha Redio cha East Africa, Heche alifunguka kuwa jeshi...
  14. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Pascal Mayalla: Oktoba 29 vyombo vya dola vilikuwa havina namna, risasi za moto zilitumika kutuliza zile vurugu

    Akiongea hivi punde kupitia Podcast ya 'Royal" mwandishi nguli wa habari nchini Tanzania Pascal Mayalla, kasema watu waliouliwa Oktoba 29 kama walikuwa wanaandamana, waliuliwa kwa sababu vyombo vya dola vilikuwa havina namna, risasi za moto zilitumika kutuliza zile vurugu. Pascal Mayalla "Na...
  15. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mchungaji Msigwa: Mauaji ya Oktoba 29 ni ya kihistoria, kuna maiti hazijaonekani, kuna maiti hazikuzikwa

    "Katika nchi yetu mauaji haya ya nini, ni ya kihistoria. Hatujawahi kupata shida kama hii. Ni mauaji makubwa, makubwa sana. Haya mauaji yaliyotokea ni makubwa sana, kuna maiti hazionekani, kuna maiti hazikuzikwa, kuna watu wengine walienda Mochwari wakiwa hai, kuna mambo ya ajabu ya hovyo...
  16. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mpina: Hongera Gen Z, Historia ya Taifa haitawasahau Mashujaa wa Maandamano ya Oktoba 2025

    "Hongera sana Gen Z, hongera sana waandamanaji wote. Mmejitoa bila kujibakiza kwa taifa lenu; wengine mmepoteza maisha, wengine mmepoteza viungo vya miili na kuwa na ulemavu wa kudumu. Historia ya nchi yetu haitawasahau. Orodha yenu ipatikane na iunganishwe kwenye mashujaa wengine waliopigania...
  17. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Peter Msigwa: Mtoto wangu aliniuliza kama angeuawa Oktoba 29, ningeendelea kusema idumu CCM?

    Mchungaji Peter Msigwa akihojiwa kupitia kituo cha Redio cha Nuru FM, amesema; "Mimi ni mtu wa kusema haki, mimi ni mtu wa kunyosha maelezo, mtu wa kusema ukweli. Sasa kuna vitu ambavyo naona nikiwa upande huu, ile umimi nashindwa. Naanza kuwa bata wakati natakiwa niwe tai. Sasa hii dunia...
  18. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

    Rais Samia Suluhu amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Ally Lila, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Picha hii imeboreshwa na AI Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa...
  19. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Madeleka: Ukitaka kuwajua waliohusika na Matukio ya Oktoba 29, rudi kabla ya Uchaguzi, Jeshi liliambiwa lijipange

    Wakili Peter Madeleka amesema Jaji Shande anaeleza ukweli kuhusu madai ya jaribio la mapinduzi lililoratibiwa, kufadhiliwa na kutekelezwa, ingawa hakufafanua waliohusika moja kwa moja. Amesema kauli hizo zinaonyesha kuna mambo muhimu ambayo jamii bado haijayaelewa kikamilifu. Madeleka amedai...
  20. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Maduhu: Nilikagua Hati za Mashtaka 1,651, sikukuta Mtu kutoka Nje ya Nchi, Matukio ya Oktoba 29

    Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Maduhu, amesema hawakuona ushahidi wowote unaoonesha kuwa vijana kutoka nchi jirani walikodiwa kuja kushiriki katika maandamano yaliyofanyika nchini mwaka jana Oktoba. Maduhu ameyasema hayo Mei 16, 2026, katika Mjadala wa Kitaifa...
Back
Top Bottom