Waweza kuthibiti mtumishi yeyote utakavyo ila si Mwalimu, ukimlazmisha kuingia darasani ataingia tu ila utaelewa baadae kaenda kufanyaje.Walimu wa serikali hutumia 10%tu ya taaluma Yao nyngne ni ktk mambo mengne ya kujikimu kwa kipato. Mtasema Sana tu.
Nakuelewa sana kamanda wangu. Mm nilipangwa shule moja maporini sna huko mkoa fulani, walimu wa serikali tulikuwa 3 na mmoja ndio headmaster, hakai kituoni wala nini, watoto wanakuja shule na visu, sime n.k. kwenye gradu wanakijiji wanakuja na mapanga na wanalazimisha kucheza na wanafunzi.
Muda ukapita kidogo nikapewa shule kama headmaster. Nikasema sasa NAWANYOOSHA. Utaratibu wa viboko kwa wale watukutu ulikuwa kila siku viboko 10 au sepa ukalime mihogo. Palitembea mkong'oto wakutisha kabisa na ukidinda naweka fimbo tunakula palingi, nakutoa manundu na hakuna kufukuza shule uache mwenyewe.
For 2 years shule ikatoa watoto 5 kwa mara ya kwanza kwenda A level. Ile shule ilikuwa kama Guantanamo katika wilaya ile mwalimu akikosana na afisa elimu anahamishiwa hapo, hakuna network, hakuna umeme, shule ipo katikati ya pori, si mara moja tumeshafunga shule kwakupata taarifa karibu na shule kunakundi la majambazi wamejificha msituni.
Baadae nikaanzisha program za wanafunzi kunywa uji shuleni, kuongea na wazazi wanafunzi wahamie shuleni walale madarasani hta kama hawana magodoro walete nyasi watalala, wazazi wakaitikia vyema watoto wakaleta milago, nikanunua generator na kupiga wiring vyumba 2 pindi likaanza hadi usiku. Walimu waliokuwa wanaletwa na hatari tupu, bangi, pombe n.k
Mpambano ukaendelea kwa viongozi wa katabna vijiji sasa, hawa jamaa, wengi wao wanachangia sana uzoroteshaji wa elimj, mwalimu anakuwa na utitiri wa mabosi hata wengine hawaelewi wanachokifanya kina athari gani katika elimu. Wengine wanasukumwa na mihemko yakisiasa hivyo kuharibu mipango mingi sana wanayojiwekea walimu katika kuwaendeleza vijana.
Katika uongozi wangu nilishapambana na hawa watu hadi ikafikia mwenyekiti wa kijiji fulani kukataliwa na wananchi wake, alitaka kuzuia tofali zisiende kujenga nyumba za shule, wananchi wakakomaa na ukizingatia zimepigwa na wananchi.
Kuwa mwalimu ni shida sana, wanafunzi wanakuchukia, viongozi wa vijiji wanataka kuwatawala na kuwaendesha, ofisi za halamashauri ndio kabisaaaaa, walimu ndio wanyonge wakutolea stress zao.
Naomba walimu mjiamini na msimamie kile mnacho amini kuwa ni sahihi na kina maslahi kwa maisha yenu, hakuna atakaye jisumbua kuwafikiria.