Ukiona mwanao hajui kusoma na kuandika ujue tatizo ni wewe mzazi
Wewe unakuwa unafanya nini hadi mtoto wako anashindwa kutofautisha kati ya R na W?
Shule ni sehemu ya kumsogeza mwanafunzi asonge mbele zaidi lakini mtu anayetakiwa kuhakikisha mtoto anajua kusoma na kuandika ni mzazi. Kwa mzazi aliye makini na anayependa elimu kweli mtoto huanza kufunzwa nyumbani na husimamia hilo na uzuri kuna vitabu vinauzwa mitaani ambavyo vinaweza kumsaidia mtoto kusoma na kuandika.
Mzazi ndio mwalimu wa kwanza wa mtoto na mtoto anapo feli lazima uanze kwanza kujiangalia wewe kama kweli unatimiza wajibu wako ipasavyo.
Mtoto unampeleka kuanza shule hajui hata kusoma a,e,i,o,u halafu umpe lawama mwalimu? hivi unafikiri kuna wanafunzi wangapi wa namna hiyo? Mzazi umechukua jitihada gani?