Sam Mahela sasa ndani ya TBC1

Sam Mahela sasa ndani ya TBC1

naona umekuja kujitangaza huku kutafuta kiki ili upate ukuu wa wilaya,
fanya kazi we mwanaume acha sifa za kipumbavu hivyo
kama ipo ipo tu
Mtangazaji Sam Mahela aliyekuwa ITV sasa hivi yuko TBC. Akiwa itv alikuwa na staili yake ya kuhitimisha habari. Naona tbc kaja na staili nyingine.
View attachment 849643
Mods kama haiko jukwaa sahihi iamishieni sehemu yake.
 
Amekuwa kituko tu!!hata kama ni kutafuta utambulisho sio kwa staili hii sasa!!mala ya kwanza kumuona alikuwa ana ripoti sehemu kulipo kuwa na ugomvi hivyo nilihisi labda anakwepa mshale/jiwe!!badaye nilipoona anatoa tabasamu nikajua tayari kumbe mwezi umeandama!!Je angekuwa ana ripoti toka kivu /goma si angekuwa ana ripoti huku anatimua mbio!!kwani wakati mwingine analipoti yupo posta ila wasiwasi utadhania hajiamini!!!
 
Binafsi sina shida na watangazaji wa TBC. Wanafanya vizuri tu. Wachangamfu sana hasa kwenye taarifa za habari! Kuhusu Mahela ni reporter asiechosha kumuangalia!

Ila kuna mambo inabidi wabadilishe kwenye muonekano na vipindi. Mfano yale maneno ya kuonyesha taarifa ya habari inaanza na habari za michezo yamekaa kizamani sanaaaa. Halafu rangi zao hazing'ai kuvutia kama TV Stations nyingine!

Halafu aina za vipindi. Kama kile cha mazungumzo baada ya habari yaani hakivutii kabisa! Wanaweza kukiacha ila waweke ubunifu. Na kile cha kumbukumbu za vifo etc. Yaani wasitengeneze vipindi ili mradi tu (bora liende)!. Na kwa kila kipindi wajiulize kama watu wanaangalia?

Sababu unaweza kukuta wanapigia debe serikali kumbe hata viongozi wenyewe wa serikali wanaangalia shilawadu clouds TV!! Unaweza kuwa na content inayoonekana boring ukaifikisha kwa hadhira kubwa kwa kutumia ubunifu. Kwa hiyo wasijipime tu kwa content wanazoweka kusifia serikali wajipime kwa kukubalika kwa wanachotangaza kwa hadhira.

Ndio sababu humu ndani nilianzisha:
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya TBC!!!! - JamiiForums
 
mimi naipenda sana hiyo staili na ninakubali jinsi anavyoongea kwa vitendo.
ngojea nione watu ambao huwa wanadai hawaangalii tbc watakavyoponda
Wewe huo muda mchafu wa kuangalia tbccm unaitoa wapi mkuu?! Au hauna kazi ya kufanya
 
Msisahau kwamba hivi ni vyombo vya propaganda hakuna professionalism kwa upande mmoja na kujiuza kwa upande wa pili.
 
Mchicha umekuwa Mchunga ila bado ni mbago ile ile
 
Me nimeacha kuangalia vipindi vyake hasa kile cha dakika 45 alivyo kuwa Itv
 
Back
Top Bottom