Mpaka leo ni Wakala tena mkubwa tu na anayetambuliwa na FIFA Mkuu. Jamaa ni mjanja mjanja na Mtoto wa mjini sana. Kala sana Pesa za Manji miaka mitatu iliyopita ambapo Simba SC tumeshafanya vibaya sana huku akishirikiana na Kiongozi mmoja Mkuu wa Simba SC mwenye jina la ' Tabaka ' fulani la Wazungu la Afrika ya Kusini ambalo liliwatesa mno Waafrika huko na hasa hasa Hayati Mzee Mandela.
Wawili hawa ndiyo walikuwa wakimuuzia Manji na yule wa TFF Ramani zote za Vita za Simba SC hadi kupelekea Simba SC kuteseka mno katika hiyo miaka na Mwenyezi Mungu akasikia Kilio chetu ambapo yule yule Nyoka aliyekuwemo ndani ya Simba SC yakamkumba ya kumkumba na huku tena na yule wa TFF nae yamemkuta huku Simba SC yetu sasa ikichanja tu mbuga kimafanikio. Amini usiamini Wawili wote hawa ni wana Yanga SC wa Kufa Mtu ila wana Simba SC wengi hawajui.