Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Pia maofisini wazee wengi tu ukifanya nao kazi sana mkiwa na urafiki hawapendi uwape shikamoo hata kama amekuzidi sana.
Ni salamu iliyojengwa na misingi ya woga sio heshima.
Tatizo sio salamu,tatizo ni hao wazee na fikra zao za kiuwoga uwoga.

Wewe unaewaza shikamoo ni utumwa ndo mwenye attizoo,mwenye fikra za kitumwatumwa.

Shikamoo sio tatizo tatizo ni watu
 
hiyo shikamoo ukijagundua uliemsalimia hivo umemzidi umri au aliekusalimia hivo ni mzee zaidi yako, unabaki na maswali mengi kichwani, inakera sana dah!!!!!
 
hiyo shikamoo ukijagundua uliemsalimia hivo umemzidi umri au aliekusalimia hivo ni mzee zaidi yako, unabaki na maswali mengi kichwani, inakera sana dah!!!!!
Ni ujinga kupoteza muda kukadiria umri wa kila mtu mpya unaekutana nae. Ndio maana watanzania tupo slow sana kwenye shughuli zetu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Siipendi hio salamu, Ni bora "Habari yako" ingekuwa poa sana... Maana salamu hata haiingiliani na heshima Bali ni kujuliana hali tu.... Habari yako mama, Habari yako baba...Ova.
 
Tamu na chungu ya utandawazi ndio hii sasa.......tukifuta hili tuje kufuta na lipi jingine.....??
 
hiyo shikamoo ukijagundua uliemsalimia hivo umemzidi umri au aliekusalimia hivo ni mzee zaidi yako, unabaki na maswali mengi kichwani, inakera sana dah!!!!!
Bila kujali umri!

Nikisalimiwa: "shikamoo" na mwanamke ninayemsorolea, huikataa shukamoo yake kwa swali:

...."Unavyoniamkia shikamoo unataka kuninyima nini?"....
 
Mama si unaona hajataka kuchanganya changanya na imani kaitafuta yake kaipachika wote tuitikie kazi iprosidi.... kuna hawa wazee wetu hizi shikamoo kama wanazitumia kishirikina usipo mpa anaweseseka kwa kisingizio cha unamdharau sasa nani alisema shikamoo heshima
waufutilie mbali ushamba huo wa shikamoo iwe tu
Wanaikataa ile "Heshima yako " ila hii ipitishwe tuachane na maunyakanzikanza
Nawasilisha
 
Ni mvurugano tu. Mbona makabila hayana hii salamu watu wote wanatumia salamu moja iwe mdogo au mkubwa. Inasemekana hii salamu imetokana na maisha ya utumwa. Kwa nini tumeishikilia kama salamu rasmi ya Kiswahili?

Hivi unajuaje kama mtu uliyekutana nae mara ya kwanza unastahili kumpa shikamoo kwa kumwangalia kwa macho? Ni mtu aliyekuzidi miaka mingapi anastahili hii salamu?

Solution itafutwe salamu moja ya Kiswahili itakayotumiwa na watu wa rika zote kama ilivo salamu za kidini, lugha za kigeni na lugha za makabila yetu. Tuondoe huu mvurugano kwenye jamii. Kama Serikali haina mbadala wa hii salamu itangaze mashindano wananchi wapendekeze mbadala.

C.c. Wizara ya Sanaa na Utamaduni
C.c. BAKITA
C.c. TATAKI
Binti yangu wa miaki nne nimemfundisha kunisalilia "greetings Daddy'na maisha yangu yako salama na yenye afya sana
 
Back
Top Bottom