Huwezi kupima umri wa mtu kwa macho.
Umri ni namba tu mzee.
Kama huwezi kupima umri basi angalia muonekano wa mtu,kama kakuzidi utamuamkia.
Wewe kijana mtu aliyekuzidi miaka nabakawa mtu mzima utamjua tu.
Ukikutana na mtu ambae una mashaka kwamba mnaendana umri basi usimuamkie utampa salamu zingine za heshima kama vile habari za asubuhi,habari za mda huu n.k
Kwa sababu shikamoo sio lazima kama ambavyo salamu zingine pia sio lazima bali ni uungwana tu.
Na bila shaka hapa hatuzungumzii ulazima tunazungumzia uungwana tu wa
Shikamo haina heshima ila ni salamu kwa ajili ya watu waliokuzidi umri.
Shikamoo ina heshima kwa sababu ndio inavyotumika kwa muktadhwa huo,huwezi kusema haina heshima.
Ukimuambia baba yako shikamoo alafu umuambie baba mpuuzi wewe bila shaka utapata jibu kuwa heshima ni ipi inatambulika hapo.
Shikamoo ni heshima kwa sababu haitumiki popote isipokuwa katika mazingira ya heshima.
Ukikusudia kumtukana mtu huwezi kumuambia shikamoo kwa sababu hiyo ni heshima bali utamuambia wewe mjinga,mpuuzi n.k
Sasa unaposema sio heshima kwa hoja gani mkuu ?
Maana ya neno shikamoo na marhaba ni nini?
Maana yake inapatikana kwa mujibu wa vile inavyotumika.
Shikamoo ni moja salamu ya kutoa heshima kwa aliekuzidi wewe kiumri ama kimajukumu(sio rasmi sana).
Na marhaba ni kupokea heshima uliyopewa.
Hizo ndo maana zake.
Ukikataa kuwa hizi sio maana zake basi niambie kuwa ili kitu kiwe na maana hiyo maana inatakiwa iwe na sifa ipi ?
Kwa sababu neno "SAMAHANI " ukiulizwa maana yake utasema ni kujishusha pengine unapokosea n.k
Hii inaelezea maana ya neno hilo kwa mujibu wa muktadhwa wake vile inavyotumika.
Kwa hiyo ukija kukataa maana ya shikamoo na marhaba itabidi ulete hoja ambazo zitaonesha kwamba ili kitu kiwe na maana fulani basi kikidhi vigezo hivi na hivi.
Maana za shikamoo na marahaba ndio hizo nilizokupa.
Napengine zipo maana nyingine nyingi tu.