Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Naunga mkono hoja.
Tungetumia salamu ya JAMBO kama inavyotumiwa na askari ingependeza sana.
Unakutana na mwenzio unamsalimia JAMBO na yeye anaitika JAMBO.
Kama ni mtoto anamsalimia mzazi wake, anamsalimu kwa JAMBO MAMA/ BABA. Mzazi anaitikia JAMBO mwanangu.
Mheshimiwa mtoa hoja, ndugu kiwiko naomba kiwasilisha.
 
Jiandae kugombana na watu. Kuna jirani nilimsalimia hivo aliwaka balaa.

Niamkie weweeee.....
Nakufungulia turbo hutaamini, yani utajuta kwanini umeng'ang'ania salamu.😂😂😂
 
Halafu kuna vizee huku kitaani vidwanzi sana eti vina maind ukiviambia "habari yako"

Kuna siku natimba home nikakuta vimeniwekea kikao vinamchana mshua eti mwanao hana adabu anatuambia sisi "habari zenu"

Mzee naye ana protocol za kiujana kwa hasira huku akipayuka akaniambia "we scars unaanzaje kuwaambia wazee wako habari yenu pasipo kuwajulia hali yao kwa kuwauliza hamjambo"

Nikaona taratibu wazee wameanza kunyanyuka mmoja mmoja anasepa
 
Mimi natumia salam ya kikabila mara nyingi hata huku mjini nikikujua mfano wewe ni mmasai au kabila lingine nakusalimia kwa lugha yako kadhalika nasalimia kwa salam ya kidini pia.

Hiyo imenisaidia sana.

Salam ya Shkamoo kiukweli ni salam ya Kitumwa kabisa.
 
Kuna vitu havina maana kabisa na nikuchosha tu brain yani ukikutana na mtu inabidi kwanza uanze kuprocess brain kuwa unampa salamu gani mimi nimeacha kabisa kutoa shikamoo ni ovyo sana hio salamu, nimefanya kazi na wazungu hata mambo ya kuitana boss hakuna wao wanataka kama anaitwa Kelvin basi muite Kelvin kama ni Mike muite Mike vitu vingine tunafanya ni Ujinga
 
Sipendi hii salam ya kitumwa. Mimi kukwepa kuwa chini ya miguu ya mtu huwa napiga Good morning. Au Bonjour.
 
Me pia naunga mkono hoja, sioni umuhimu wa kumsalimia mtu shikamoo ili hali haina mrejesho wake maana anajibu marahaba, marahaba ni nini? Au marahaba inatoa taarifa gani ambayo mimi niliyesalimia natakiwa kuelewa kuwa akisema marahaba labda anamaanisha hivi au vile. Au akijibu marahaba wewe mtoa salama ufanyeje kinachofuata au uelewe huyo mtu yupo kwenye hali gani na huo ndio upungufu wa hiyo salamu yetu pendwa.

Lakini tukitumia salama zetu mfano habari za asubuhi, utajibiwa nzuri/mbaya hayo majibu yana mrejesho wa hali iliyopo kwa msalimiwa ambapo kuanzia hapo unaweza pata cha kuendelea nacho mfano umejibiwa mbaya utauliza kwanini mbaya ana kadharika.

Au habari za kuamka, habari za mchana, habari za jioni majibu yake yana mrejesho wa moja kwa moja ambao unakupa picha halisi ya hali aliyonayo msalimiwa lakini pia inatoa urahisi wa kujua hali ya msalimiaji kwa kurejesha salam hiyo hiyo kwake. Mfano umeamkaje? Atajibu nimeamka vizuri/vibaya vipi wewe/ninyi mmeamkaje? Kisha kuanzia hapo maongezi ya kujuliana hali yanaendelea.

Nawasilisha.
 
Hata baba angu na mama angu nawasalimiankwa kilugha.
Ni mvurugano tu. Mbona makabila hayana hii salamu watu wote wanatumia salamu moja iwe mdogo au mkubwa. Inasemekana hii salamu imetokana na maisha ya utumwa. Kwa nini tumeishikilia kama salamu rasmi ya Kiswahili?

Hivi unajuaje kama mtu uliyekutana nae mara ya kwanza unastahili kumpa shikamoo kwa kumwangalia kwa macho? Ni mtu aliyekuzidi miaka mingapi anastahili hii salamu?

Solution itafutwe salamu moja ya Kiswahili itakayotumiwa na watu wa rika zote kama ilivo salamu za kidini, lugha za kigeni na lugha za makabila yetu. Tuondoe huu mvurugano kwenye jamii. Kama Serikali haina mbadala wa hii salamu itangaze mashindano wananchi wapendekeze mbadala.

C.c. Wizara ya Sanaa na Utamaduni
C.c. BAKITA
C.c. TATAKI
 
Mama angu sikuhizi tukipigiana simu tunasalimiana kikabila
Mfano; "ndauli" = vipi
"kamwene"=nimekuona.
Then deal done!!!
 
mtu shikamoo ili hali haina mrejesho wake maana anajibu marahaba, marahaba ni nini?
Mkuu mara unasema haina mrejesho mara unasema marejesho wake marahaba,sasa huo si ndio mrejesho ?

NENO Marahaba ni mrejesho wa shikamoo.

Kuhusu maana mkuu maana yake ni hiyo kuwa ni mrejesho wa shikamoo.sijajua unataka kujua nini zaidi.

Au marahaba inatoa taarifa gani ambayo mimi niliyesalimia natakiwa kuelewa kuwa akisema marahaba labda anamaanisha hivi au vile.
Sasa mkuu taarifa inayotoa si ni muitikio kuonesha kuwa anaeamkiwa ameitikia.
Kwa sababu ukimuambia mtu shikamoo akikuambia marhaba inakuwa hujaelewa kwamba marhaba ni muitikio mkuu?

Kwa sababu kila sehemu katika sisi waswahili ukisema marahaba tu from no where utaulizwa ama watakushangaa kwani kuna aliyekuamkia hapa ?

Hii kuonesha kuwa marahaba inafahamika maana yake kuwa ni jawabu la shikamoo.

Sijui unataka maana ipi mkuu ?
Au akijibu marahaba wewe mtoa salama ufanyeje kinachofuata au uelewe huyo mtu yupo kwenye hali gani na huo ndio upungufu wa hiyo salamu yetu pendwa.
Kazi ya shikamoo na marahaba sio kujua hali,bali ni kutoa heshima tu.

Na heshima unatakiwa umpe mtu aliyekuzidi haijalishi yupo katika hali gani,kwa hiyo maadamu heshima ni lazima utoe kwa mtu aliyekuzidi bila kujali hali yake,basi hapo ndo shikamoo na marahaba ni PAHALA PAKE.

Ukitaka kujua yanayofuata utaongeza na maongezi mengine kama vile vipi hali,salama,unaendeleajeee ?

Kwa hiyo lazima utambue kwanza kwamba shikamoo/marahaba nii ni kwa ajili ya heshima na sio kwa ajili ya kujua hali.

Ukitaka kujua hali usitumie shikamooa kwa sababu shikamoo hapo sio pahala pake.
Ni kama ambavyo mkionana mnapeana mikono kwa kuonesha mnajaliana na kupendana..

Huwezi kuhoji kuwa kupeana mikono ifutwe ati kwa sababu ukimpa mtu mkono unakuwa hujui hali yake kama anaumwa au ana njaa ?

Au kupungiana mikono mkiwa mbali uone haifai ati kwa sababu ukimsalimia hivyo mtu inakuwa hujui hali yake kama mgonjwa au mzima ?

Kupungiana mikono ni ishara ya kuonana kwa mbali nayo ni salamu na hii salamu kazi yake sio kujua hali ya mtu bali kuonesha mmeonana japo kwa mbali.
Lakini tukitumia salama zetu mfano habari za asubuhi, utajibiwa nzuri/mbaya hayo majibu yana mrejesho wa hali iliyopo kwa msalimiwa ambapo kuanzia hapo unaweza pata cha kuendelea nacho mfano umejibiwa mbaya utauliza kwanini mbaya ana kadharika.
Sasa hapa hizi ni salamu za kujua hali na sio salamu za heshima ama kuonana.

Ukitaka kujua hali ya mtu sasa uliza hivyo ulivyoandika.kuuliza hali ya mtu ni kinyume na kumsalimia tu kwa kumpa heshima.

Kama ambavyo neno pole anaambiwa yule ambae anahisiwa kuwa kapata shida ama kusumbuka ndivyo ambavyo shikamoo anaambiwa mtu mkubwa aliekuzidi umri.

Kwa hiyo kujua hali ya mtu ni tofauti na salamu ya heshima.lugha ya kiswahili nayo ni tajiri.sio kwamba ukisema habari ukinibiwa ndo umejumuisha kila kitu hapana.
Au habari za kuamka, habari za mchana, habari za jioni majibu yake yana mrejesho wa moja kwa moja ambao unakupa picha halisi ya hali aliyonayo msalimiwa lakini pia inatoa urahisi wa kujua hali ya msalimiaji kwa kurejesha salam hiyo hiyo kwake.
Hapa ndo pale pale kuwa UNAIJAALIA SHIKAMOO NA MARAHABA KUWA NI SALAMU YA KUJULIANA HALI,HAPANA

sahikamoo marahaba ni salamu ya heshima sio kujuliana hali kabisa,ni heshima ambayo salamu hii ataanza mdogo kusema shikamoo na mkubwa ataitikia marhaba.

Usiifanye kuwa ni salamu ya hali hii ni salamu ya heshima,na heshima unatakiwa umpe mtu skiwa katika hali yeyote,ya uzima,ugonjwa n.k

Kwa hiyo salamu ya jeshima ina mrejesho wa moja kwa moja kuwa shikamoo mrejesho wake marahaba.

Huo ni nrejesho mujarrabu kabisa ambao kila mtu anaufahamu kindakindaki kuwa ukisalimiwa hivi itikia hivi.
Kisha kuanzia hapo maongezi ya kujuliana hali yanaendelea
Kwa maneno yako haya mkuu ☝️☝️☝️☝️☝️ kumbe unakubali kuwa hata hizo salamu ambazo unazitaka tuzifanye bado zinaweza sizitosheleze kujua hali ya mtu kama ambavyo shikamoo haiwezi kutosheleza kujua hali ya mtu moja ?

Kwa hiyo sio shikamoo tu ndo ambayo haifanyi mtu kujua hali ya mwingine zaidi,bali hata hizo salamu zingine pia zinaweza zisitoe majawabu ya hali ya mtu mpaka maongezi mengine yaendelee kama ulivyosema mkuu.

Kwa hiyo kuibatilisha shikamoo kwa hoja ya kuwa haitoshelezi kujua hali ya mtu manake unazibatilisha hata hizo salamu zingine ulizozionesha huko juu kwa sababu hata hizo pia pekee hazitoshelezi kujua hali ya mtu moja kwa moja.

Ili ujue hali ya mtu itabidi utoke katika salamu uingie katika maongezi,na huku ni kuonesha kuwa SALAMU haileti jawabu la kutosheleza kujua hali ya mtu.

Kwa hivyo mimi SIUNGI MKONO HOJAHII
 
Unajuaje kuwa mtu anastahili hio heshima? Salamu nyingine hazina heshima?
Mkuu mara unasema haina mrejesho mara unasema marejesho wake marahaba,sasa huo si ndio mrejesho ?

NENO Marahaba ni mrejesho wa shikamoo.

Kuhusu maana mkuu maana yake ni hiyo kuwa ni mrejesho wa shikamoo.sijajua unataka kujua nini zaidi.

Sasa mkuu taarifa inayotoa si ni muitikio kuonesha kuwa anaeamkiwa ameitikia.
Kwa sababu ukimuambia mtu shikamoo akikuambia marhaba inakuwa hujaelewa kwamba marhaba ni muitikio mkuu?

Kwa sababu kila sehemu katika sisi waswahili ukisema marahaba tu from no where utaulizwa ama watakushangaa kwani kuna aliyekuamkia hapa ?

Hii kuonesha kuwa marahaba inafahamika maana yake kuwa ni jawabu la shikamoo.

Sijui unataka maana ipi mkuu ?
Kazi ya shikamoo na marahaba sio kujua hali,bali ni kutoa heshima tu.

Na heshima unatakiwa umpe mtu aliyekuzidi haijalishi yupo katika hali gani,kwa hiyo maadamu heshima ni lazima utoe kwa mtu aliyekuzidi bila kujali hali yake,basi hapo ndo shikamoo na marahaba ni PAHALA PAKE.

Ukitaka kujua yanayofuata utaongeza na maongezi mengine kama vile vipi hali,salama,unaendeleajeee ?

Kwa hiyo lazima utambue kwanza kwamba shikamoo/marahaba nii ni kwa ajili ya heshima na sio kwa ajili ya kujua hali.

Ukitaka kujua hali usitumie shikamooa kwa sababu shikamoo hapo sio pahala pake.
Ni kama ambavyo mkionana mnapeana mikono kwa kuonesha mnajaliana na kupendana..

Huwezi kuhoji kuwa kupeana mikono ifutwe ati kwa sababu ukimpa mtu mkono unakuwa hujui hali yake kama anaumwa au ana njaa ?

Au kupungiana mikono mkiwa mbali uone haifai ati kwa sababu ukimsalimia hivyo mtu inakuwa hujui hali yake kama mgonjwa au mzima ?

Kupungiana mikono ni ishara ya kuonana kwa mbali nayo ni salamu na hii salamu kazi yake sio kujua hali ya mtu bali kuonesha mmeonana japo kwa mbali.
Sasa hapa hizi ni salamu za kujua hali na sio salamu za heshima ama kuonana.

Ukitaka kujua hali ya mtu sasa uliza hivyo ulivyoandika.kuuliza hali ya mtu ni kinyume na kumsalimia tu kwa kumpa heshima.

Kama ambavyo neno pole anaambiwa yule ambae anahisiwa kuwa kapata shida ama kusumbuka ndivyo ambavyo shikamoo anaambiwa mtu mkubwa aliekuzidi umri.

Kwa hiyo kujua hali ya mtu ni tofauti na salamu ya heshima.lugha ya kiswahili nayo ni tajiri.sio kwamba ukisema habari ukinibiwa ndo umejumuisha kila kitu hapana.
Hapa ndo pale pale kuwa UNAIJAALIA SHIKAMOO NA MARAHABA KUWA NI SALAMU YA KUJULIANA HALI,HAPANA

sahikamoo marahaba ni salamu ya heshima sio kujuliana hali kabisa,ni heshima ambayo salamu hii ataanza mdogo kusema shikamoo na mkubwa ataitikia marhaba.

Usiifanye kuwa ni salamu ya hali hii ni salamu ya heshima,na heshima unatakiwa umpe mtu skiwa katika hali yeyote,ya uzima,ugonjwa n.k

Kwa hiyo salamu ya jeshima ina mrejesho wa moja kwa moja kuwa shikamoo mrejesho wake marahaba.

Huo ni nrejesho mujarrabu kabisa ambao kila mtu anaufahamu kindakindaki kuwa ukisalimiwa hivi itikia hivi.
Kwa maneno yako haya mkuu [emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516] kumbe unakubali kuwa hata hizo salamu ambazo unazitaka tuzifanye bado zinaweza sizitosheleze kujua hali ya mtu kama ambavyo shikamoo haiwezi kutosheleza kujua hali ya mtu moja ?

Kwa hiyo sio shikamoo tu ndo ambayo haifanyi mtu kujua hali ya mwingine zaidi,bali hata hizo salamu zingine pia zinaweza zisitoe majawabu ya hali ya mtu mpaka maongezi mengine yaendelee kama ulivyosema mkuu.

Kwa hiyo kuibatilisha shikamoo kwa hoja ya kuwa haitoshelezi kujua hali ya mtu manake unazibatilisha hata hizo salamu zingine ulizozionesha huko juu kwa sababu hata hizo pia pekee hazitoshelezi kujua hali ya mtu moja kwa moja.

Ili ujue hali ya mtu itabidi utoke katika salamu uingie katika maongezi,na huku ni kuonesha kuwa SALAMU haileti jawabu la kutosheleza kujua hali ya mtu.

Kwa hivyo mimi SIUNGI MKONO HOJAHII
 
Unajuaje kuwa mtu anastahili hio heshima?
Utajua kwa kumuangalia tu muinekano wako.

Magufuli akionana na diamond bila shaka diamond atajua kuwa anahitaji amwamkie magufuli.

Kwa hiyo kwa kuangalia tu unajua.
Salamu nyingine hazina heshima?
Tuanze na shikamoo kwanza tunakubaliana ina heshima au haina wa mujibu wa maelezo yangu hapo juu ?

Manake hapo sasa kana kwamba unna maanisha kuwa salamu zingine zina heshima kwa hiyo shikamoo tuiwache,ndo nauliza shikamoo haina heshima ili tuiwache tuangalie hizo zingine ?
 
Back
Top Bottom