Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Salamu ya shikamoo ifutwe rasmi na Serikali

Halafu kuna vizee huku kitaani vidwanzi sana eti vina maind ukiviambia "habari yako"

Kuna siku natimba home nikakuta vimeniwekea kikao vinamchana mshua eti mwanao hana adabu anatuambia sisi "habari zenu"

Mzee naye ana protocol za kiujana kwa hasira huku akipayuka akaniambia "we scars unaanzaje kuwaambia wazee wako habari yenu pasipo kuwajulia hali yao kwa kuwauliza hamjambo"

Nikaona taratibu wazee wameanza kunyanyuka mmoja mmoja anasepa

Mimi kuna mzee mmoja nilimsalimia nyakati flani hivi kwa kutumia "shikamoo" alinimind sana, baadae akanieleza haipendi hiyo salam na nisipende kuitumia, hasa maeneo ya ufukweni ama zanzibar!
Kiukweli tokea siku ile niliacha kuitumia, hiyo salamu ni ya kitumwa unaweza mwamkia mtu hiyo salam kumbe ni mwanao hasa hawa akina mama!
 
Kweli kabisa. Ni ngumu kukadiria umri wa mwanamke.
Mimi kuna mzee mmoja nilimsalimia nyakati flani hivi kwa kutumia "shikamoo" alinimind sana, baadae akanieleza haipendi hiyo salam na nisipende kuitumia, hasa maeneo ya ufukweni ama zanzibar!
Kiukweli tokea siku ile niliacha kuitumia, hiyo salamu ni ya kitumwa unaweza mwamkia mtu hiyo salam kumbe ni mwanao hasa hawa akina mama!
 
Habari ya kwako (unataja jina lake )


Mfano ;

Dkt jpm : habari ya kwako Maalim Seif

Maalim Seif : Nzuri tu /salama tu / buheri wa afya ya uzee / safi kabisa najua ntashinda zanzibar ruksa kupindisha meza .
 
Halafu kuna vizee huku kitaani vidwanzi sana eti vina maind ukiviambia "habari yako"

Kuna siku natimba home nikakuta vimeniwekea kikao vinamchana mshua eti mwanao hana adabu anatuambia sisi "habari zenu"

Mzee naye ana protocol za kiujana kwa hasira huku akipayuka akaniambia "we scars unaanzaje kuwaambia wazee wako habari yenu pasipo kuwajulia hali yao kwa kuwauliza hamjambo"

Nikaona taratibu wazee wameanza kunyanyuka mmoja mmoja anasepa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aiseee
 
Ukigeuka nyuma shikamoo ukiangalia shoto shikamboo,kaskazini shikamoo, magharibi shikamboo aisee
 
Napendekeza salamu hizi zitumike:

"Amani na upendo iwe nawe/nanyi.
.......Iwe pamoja nawe."
"Habari za /ya kazi.
......Tunashukuru aliye juu ya yote."
 
Ni ya kitumwa. Mtumwa kumsalimia Mmiliki wa Mtumwa. Sio habari Za kuzidi umri. Sema wazee wa zamani waliopenda Umungu mtu ndio wakaibeba baada ya utumwa ilhali walijua haikuwa Ina maana nzuri.
Unaemwambia shikamoo "niko chini ya miguu yako" unampa cheo cha KiMungu mtu kwamba hata life yako Yeye ndio anayeweza kuamua uwe hai au ufe kama kipindi cha utumwa.
Mimi home tangu wadogo tunasalimia wazazi kwa kilugha tu. Napataga shida Sana kumwambia mtu shikamoo. Siipendi kabisa hii salamu. Ukiwa huru hutakiwi kuwa na minyororo ya kitumwa na ndo maana hata America wamelifuta neno NIGER kulitamka sababu ya historia yake kwa watu weusi kipindi cha utumwa.
Shikamoo ni lugha gani asili yake ?
 
Mkuu mara unasema haina mrejesho mara unasema marejesho wake marahaba,sasa huo si ndio mrejesho ?

NENO Marahaba ni mrejesho wa shikamoo.

Kuhusu maana mkuu maana yake ni hiyo kuwa ni mrejesho wa shikamoo.sijajua unataka kujua nini zaidi.


Sasa mkuu taarifa inayotoa si ni muitikio kuonesha kuwa anaeamkiwa ameitikia.
Kwa sababu ukimuambia mtu shikamoo akikuambia marhaba inakuwa hujaelewa kwamba marhaba ni muitikio mkuu?

Kwa sababu kila sehemu katika sisi waswahili ukisema marahaba tu from no where utaulizwa ama watakushangaa kwani kuna aliyekuamkia hapa ?

Hii kuonesha kuwa marahaba inafahamika maana yake kuwa ni jawabu la shikamoo.

Sijui unataka maana ipi mkuu ?
Kazi ya shikamoo na marahaba sio kujua hali,bali ni kutoa heshima tu.

Na heshima unatakiwa umpe mtu aliyekuzidi haijalishi yupo katika hali gani,kwa hiyo maadamu heshima ni lazima utoe kwa mtu aliyekuzidi bila kujali hali yake,basi hapo ndo shikamoo na marahaba ni PAHALA PAKE.

Ukitaka kujua yanayofuata utaongeza na maongezi mengine kama vile vipi hali,salama,unaendeleajeee ?

Kwa hiyo lazima utambue kwanza kwamba shikamoo/marahaba nii ni kwa ajili ya heshima na sio kwa ajili ya kujua hali.

Ukitaka kujua hali usitumie shikamooa kwa sababu shikamoo hapo sio pahala pake.
Ni kama ambavyo mkionana mnapeana mikono kwa kuonesha mnajaliana na kupendana..

Huwezi kuhoji kuwa kupeana mikono ifutwe ati kwa sababu ukimpa mtu mkono unakuwa hujui hali yake kama anaumwa au ana njaa ?

Au kupungiana mikono mkiwa mbali uone haifai ati kwa sababu ukimsalimia hivyo mtu inakuwa hujui hali yake kama mgonjwa au mzima ?

Kupungiana mikono ni ishara ya kuonana kwa mbali nayo ni salamu na hii salamu kazi yake sio kujua hali ya mtu bali kuonesha mmeonana japo kwa mbali.
Sasa hapa hizi ni salamu za kujua hali na sio salamu za heshima ama kuonana.

Ukitaka kujua hali ya mtu sasa uliza hivyo ulivyoandika.kuuliza hali ya mtu ni kinyume na kumsalimia tu kwa kumpa heshima.

Kama ambavyo neno pole anaambiwa yule ambae anahisiwa kuwa kapata shida ama kusumbuka ndivyo ambavyo shikamoo anaambiwa mtu mkubwa aliekuzidi umri.

Kwa hiyo kujua hali ya mtu ni tofauti na salamu ya heshima.lugha ya kiswahili nayo ni tajiri.sio kwamba ukisema habari ukinibiwa ndo umejumuisha kila kitu hapana.
Hapa ndo pale pale kuwa UNAIJAALIA SHIKAMOO NA MARAHABA KUWA NI SALAMU YA KUJULIANA HALI,HAPANA

sahikamoo marahaba ni salamu ya heshima sio kujuliana hali kabisa,ni heshima ambayo salamu hii ataanza mdogo kusema shikamoo na mkubwa ataitikia marhaba.

Usiifanye kuwa ni salamu ya hali hii ni salamu ya heshima,na heshima unatakiwa umpe mtu skiwa katika hali yeyote,ya uzima,ugonjwa n.k

Kwa hiyo salamu ya jeshima ina mrejesho wa moja kwa moja kuwa shikamoo mrejesho wake marahaba.

Huo ni nrejesho mujarrabu kabisa ambao kila mtu anaufahamu kindakindaki kuwa ukisalimiwa hivi itikia hivi.
Kwa maneno yako haya mkuu [emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516] kumbe unakubali kuwa hata hizo salamu ambazo unazitaka tuzifanye bado zinaweza sizitosheleze kujua hali ya mtu kama ambavyo shikamoo haiwezi kutosheleza kujua hali ya mtu moja ?

Kwa hiyo sio shikamoo tu ndo ambayo haifanyi mtu kujua hali ya mwingine zaidi,bali hata hizo salamu zingine pia zinaweza zisitoe majawabu ya hali ya mtu mpaka maongezi mengine yaendelee kama ulivyosema mkuu.

Kwa hiyo kuibatilisha shikamoo kwa hoja ya kuwa haitoshelezi kujua hali ya mtu manake unazibatilisha hata hizo salamu zingine ulizozionesha huko juu kwa sababu hata hizo pia pekee hazitoshelezi kujua hali ya mtu moja kwa moja.

Ili ujue hali ya mtu itabidi utoke katika salamu uingie katika maongezi,na huku ni kuonesha kuwa SALAMU haileti jawabu la kutosheleza kujua hali ya mtu.

Kwa hivyo mimi SIUNGI MKONO HOJAHII
Kwani ukiambiwa habari za sahizi hujaheshimiwa?

Ukiambiwa goodmorning sir hujaheshimiwa?

Shikamoo ni salamu ya kitumwa.
 
Nilishaacha kutumia hiyo salamu kitambo sana.
Kwa wanao sawa lakini sikuoni kabisa ati uanbishana na baba au babu yajo hutaki kumwamkia?acha porojo wewe!waambie wanao wasikuamkie ila usithubutu kutafuta ugomvi usio na kichwa wala miguu na wazee
 
Hii salamu siipendi imekaa kitumwa sana.

Sipendi kuamkia wala kuamkiwa shkamoo. Ni salamu ya kinoko inayoondoa kujiamini na kukufanya uwe mdogo na duni.

Serikali ipige marufuku hii salamu maana tukijiamulia kuna watu watatoana ngeu kwa kulilia kuamkiwa.
Naunga mkono hoja,,, sisi tuliokulia mijini hatutumii hiyo salam. Imekaa kitumwa sana!!!
 
Ni mvurugano tu. Mbona makabila hayana hii salamu watu wote wanatumia salamu moja iwe mdogo au mkubwa. Inasemekana hii salamu imetokana na maisha ya utumwa. Kwa nini tumeishikilia kama salamu rasmi ya Kiswahili?

Hivi unajuaje kama mtu uliyekutana nae mara ya kwanza unastahili kumpa shikamoo kwa kumwangalia kwa macho? Ni mtu aliyekuzidi miaka mingapi anastahili hii salamu?

Solution itafutwe salamu moja ya Kiswahili itakayotumiwa na watu wa rika zote kama ilivo salamu za kidini, lugha za kigeni na lugha za makabila yetu. Tuondoe huu mvurugano kwenye jamii. Kama Serikali haina mbadala wa hii salamu itangaze mashindano wananchi wapendekeze mbadala.

C.c. Wizara ya Sanaa na Utamaduni
C.c. BAKITA
C.c. TATAKI
Baada ya kujua maana ya SHIKAMOO nilichoka aiseee
 
Shikamoo ni salam ambayo nyumban kwetu ilikua haitumiki kabisa, ila nikienda shule mwalim wa kiswahili akiingia darasan ni lazma tumwambie shikamoo mwaliiiim, na ukionekana husalimii unachezea bakora mabadiliko yaanzie shuleni
 
Kwani ukiambiwa habari za sahizi hujaheshimiwa?
Mimi sikatai kuwa kuna heshima zingine zaidi ya shikamoo,nakubali kabisa kwamba kuna heshima zingine zaidi ya shikamoo.

Ila sasa kuwepo kwa heshima zingine zaidi ya shikamoo hiyo haiwezi kumaanisha kuwa kutumia heshima ya shikamoo kwamba eti haifai.

Yaani huwezi kutuambia kuwa kwa kuwa kuna ist sasa hivi basi haifai kutumia NOAH sio ?

Kwa kuwa kuna smartphone kwamba haifai kutumia nokia za tochi sio ?

Kwa kuwa kuna tv flat basi haifai kutumia za chogo sio ?
Ukiambiwa goodmorning sir hujaheshimiwa?
Umeheshimiwa pia.

Hapa hatujadili kwamba hakuna heshima zingine zaidi ya shikamoo,hapa tunajadili kuwa kwa nini isifae kutumia neno shikamoo ?

Kwa nini isifae kutumia neno hilo,na sote tunakubaliana kwamba hata hiyo "za saaizi" kuna salamu nyingine nyinginza heshima zaidi ya hiyo "za saa hizi "

Sasa kuwepo kwwa salamu nyingi za heshima kama vile "za saahivi,habari yako je hiyo inaweza kuwa hoja kuwa tusitumie salamu ya ZA KUTWA ?
 
Hii salamu siipendi imekaa kitumwa sana.

Sipendi kuamkia wala kuamkiwa shkamoo. Ni salamu ya kinoko inayoondoa kujiamini na kukufanya uwe mdogo na duni.

Serikali ipige marufuku hii salamu maana tukijiamulia kuna watu watatoana ngeu kwa kulilia kuamkiwa.
Tatizo sio salamu.

Tatizo ni wewe una mawwzo ya kitumwa bwana mkubwa godizila.

Hata ukiamua usitumie gari kwa kuona kuwa zimetoka kwa wale ambao walitufanya watumwa ni sawa hayo mawwzo yako tu haina hsida.

Hata ukiamua kuwa usitumie neno samahani kwa sababu ni kujishusha sawa,ila hayo ni mawazo yako ya kiutumwa utumwa na wala sio asili ya neno samahani.

Yani tatizo sio shikamoo,tatizo fikra zako.
 
Back
Top Bottom