Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
SALA YA KUOMBEA HAKI NA AMANI
Ee Mungu tunakusifu, tunakuheshimu, tunakutukuza, tunakuabudu na kukushukuru sisi Watanzania kwa kutujalia Nchi nzuri. Tunakushukuru pia kwa zawadi ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei 2025.
Tukiwa Mahujaji katika Matumaini, tunakuomba utuepushe na changamoto zinazoweza kuvuruga Haki na Amani. Jaza nyoyo zetu Mapendo yako ili wote tuwajibike kiaminifu, na utuunganishe ili kuishi kama ndugu wa familia moja.
Ee Mwenyezi Mungu, uongozi wa kweli unatoka kwako. Tunakuomba uijalie Nchi yetu viongozi wema na waadilifu watakaoliongoza Taifa letu kuishi tunu za Upendo, Ukweli, Haki na Amani.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi ya Asili, Mlinzi wa Taifa letu.
Utuombee.