Sakata la Walimu kufukuzwa kule Tunduma kisa wimbo wa Zuchu "Honey" ni Kipimo cha Mawaziri Vilaza wa Nyakati za Sasa

Wewe ni poor brain na waziri wako pia ni poor brain
Nyimbo inapotred inapigwa kila mahali mda wote hao watoto walikiwa wanauimba kama wimbo wa taifa vile yani wanaujua sana

Eti wewe huoni kosa la waziri,serikali wala basata bali waalimu ndiyo wenye makosa
Na ukiangalia hapo shule ni kama kulikuwa na tukio maalumu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Waziri has demonstrated the possession of stereotype and fragile mindset, very primitive, if he had multidisciplinary transferable skills asingelifanya huo mkurupuko.
Kwa hiyo ni Sawa Watoto waimbe Shuleni Hani Wangu akinuna Namkatia Kiuno na Kubinua Makalio🙆🙆🤦🤦. Hata home kwako huwezi kuruhusu Mtoto wako aimbe hayo Mashairi Masikioni kwako. Well-done Waziri Linda Maadili Baba.
 
Haya wengine hao!!!🤣🤣😂
 

Attachments

Kiongozi umesema ukweli mtupu. Shuleni ni mahali ambapo nidhamu ya watoto inatengenezwa ndiyo maana mtoto kama anakuja na tabia mbaya toka kwao ataathibiwa au fukuzwa. Sasa walitaka eti kisa basata wameacha huo wimbo basi ni halali watoto wacheze. Mbona baa kuna liseni wanapewa ya kufanya biashara hiyo lakini akikutwa mwanafunzi sheria inachukua mkondo wake. Tuache kushabikia ujinga nampongeza Waziri kwa hatua aliyochukua. Kama wazazi wachache hawajitambui basi acha Waziri asaidie.Nimeangalia clip ni kitu cha ajabu sana walimu walichokifanya. Hii iwe fundisho na kwa wengine. Zipo nyimbo ambazo watoto wanaweza wekewa na wakacheza bila tatizo lolote.
 
waziri kacheza part yake nampongeza sana na jambo la kumuunga mkono
 
Imagine nchi inaongozwa na watu illogical kama huyo waziri. Hiyo hatua aliyochukua ni tatizo kubwa kuliko tatizo lenyewe.

Hell kama huyo jamaa ni waziri basi mimi Rais.
 
We ndo kilaza mshamba kabisa kawapigie watoto wako nyimbo za kipuuzi kama hizo mpuuzi mmoja ww
 
Acha kupotosha jamii,hakuna Mwl aliyefukuzwa kisa wimbo.
 
Umeandika wamefukuzwa lkn reference uliyoweka inasema wamevuliwa madaraka halafu unasema Mkenda......, Sasa hapo kosa lake ni lipi?
 
I love this post. I showed this post to my family & they also loved this post.we bought a projector & showed this post to the whole neighborhood & they also loved this post. Our lives have changed because of this post. We are grateful to you for this post,Thank you so much for this post..
 
Nashangaa mijitu ya humu ina shabikia ujinga tu..

Nilichokiona hapa wengi wanafuata mkumbo
 
Wimbo ungekuwa haufai serikali ingeufungia kama inavyofunga za Roma mkatoliki na Ney wa mitego, kila mtaa sasa hivi ni hanii hanii pengine hadi watoto wake huko nyumbani wanaimba,kazi kuonea walimu tu. Naungana na wewe huyu waziri ni kilaza!!
 
Basata wako busy na kina Roma na sio nyimbo zisizo na maadili !!

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…