FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Habari!
Marekani imetangaza rasmi [Jumatatu] kuiwekea vikwazo Uturuki baada ya Ankara kutekeleza mpango wake wa ununuzi wa mfumo wa kijeshi wa ulinzi wa anga ujulikanao kama S-400 kutoka nchini Urusi.
Takribani mwaka mmoja na nusu baada ya Uturuki kununua mfumo huo, Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi vikwazo kwa taifa hilo ambalo pia ni nchi mwanachama wa jumuiya ya NATO.
Chini ya sheria ya vikwazo iliyopitishwa na Bunge la Congress mwaka 2017 ijulikanayo kama Countering America's Adversaries Through Sanctions Act (CAATSA), vikwazo vimelilenga shirika linalohusika na masuala ya ununuzi lililo chini ya Wizara ya Ulinzi ya Uturuki pamoja na maafisa wa ngazi za juu akiwemo rais wa shirika hilo.
Vikwazo vya Jumatatu vinamaanisha kuwa, shirika hilo limefutiwa leseni za ununuzi wa bidhaa kutoka nchini Marekani likiwemo zuio la kupokea mkopo unaozidi dola milioni 10 kutoka katika benki za Marekani sanjari na zuio la mikopo kutoka katika mashirika ya fedha ya kimataifa kama vile World Bank.
Vikwazo pia vimejumuisha kuzifungia mali pamoja na viza kwa maafisa wa juu wa shirika hilo.
Mengine na zaidi ya haya yatakayokuwa yakijiri kuhusiana na sakata hili tutaendelea kuyafahamu kadri muda utakavyoturuhusu kuyafahamu!
Pia, unaweza kupitia taarifa ya awali kuhusiana na sakata hili:

Sakata la ununuzi wa S-400: Uturuki kuwekewa vikwazo
Habari! Mpango uliofikiriwa muda mrefu wa kuiwekea vikwazo nchi ya Uturuki juu ya hatua ya nchi hiyo kununua mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400 kutoka nchini Urusi umeripotiwa kukamilika. Kulingana na vyanzo mbalimbali wakiwemo maafisa kutoka nchini Marekani wameweka bayana kukamilika kwa mpango...
www.jamiiforums.com