Uturuki yatangaza kusambaratisha genge la kijasusi la Israel dhidi ya Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Uturuki yatangaza kusambaratisha genge la kijasusi la Israel dhidi ya Iran

May 24, 2023 06:35 UTC

[https://media]

Shirika la kijasusi la Uturuki limetangaza kuwa limefanikiwa kusambaratisha mtandao wa shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD uliokuwa unatumia ardhi ya Uturuki kufanya ujasusi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la Tasnim limevinukuu vyombo vya habari vya Uturuki vikiripoti taarifa ya shirika la kijasusi la nchi hiyo ikisema kwamba limefanikiwa kugundua na kusambaratisha genge la kijasusi la MOSSAD lililokuwa likifanya ujasusi dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtandao huo wa kijasusi wa Wazayuni ambao ulikuwa unafuatiliwa na maafisa usalama wa Uturuki kwa muda wa mwaka mzima na nusu, ulikuwa unafanya ujasusi dhidi ya mashirika yenye mfungamano na Iran.

Majasusi 13 wa mtandao huo wametiwa mbaroni. Mwaka jana pia, majasusi 15 wa shirika hilo la kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel walitiwa mbaroni nchini Uturuki kwa kufanya ujasusi dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS.

Wakati huo huo Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imewakamata wanachama wa mtandao wa kijasusi ambao walikuwa wanajishughulisha na mradi unaoendeshwa na shirika moja la kigeni la kijasusi kupata habari kuhusu Wairani wanaosafiri nje ya nchi.

Katika taarifa iliyotolewa jana Jumanne, wizara hiyo imesema kuwa shirika hilo la kijasusi limekuwa likiwafuatilia Wairani wenye majukumu katika nyadhifa tofauti au utaalamu maalumu katika nyanja mbalimbali na vilevile wale wanaopata taarifa muhimu za taasisi nyeti humu nchini.

Hayo yameripotiwa katika hali ambayo, siku ya Jumapili, Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran ilitangaza kwamba vikosi vyake vilivamia timu ya magaidi yenye mafungamano na shirika la kijasusi la utawala haramu wa Israel Mossad katika eneo la magharibi mwa nchi.

Aidha, mapema wiki hii, vikosi vya usalama wa taifa katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) vilisambaratisha mtandao wa kigaidi wenye mafungamano na genge la kigaidi la Daesh Khorasan (Daesh-K) katika mkoa wa kusini mwa Iran wa Fars.
 
Tangu Edogan ajifanyie mapinduzi fake ya kujipinduwa mwenyewe ili awakamate na kuwaweka jela wapinzani wake huwa siamini habari za serikali ya Uturuki, imejaa usanii sana.

Hata shule za Feza zilizopo Tanzania zinamilikiwa na mpinzani wa Edogan alitaka zifungwe ni Rais msanii msanii sana si mtu wa kuaminika.
 
Mleta uzi naye ni mdini kindakindaki
 
Chuki zako kwa Israel haziongezi wala kupunguza chochote. Wewe waite majina yote mara "mazayuni" "mayahudi" lakini hamna lolote. Kama unataka nitakupatia manati yangu nenda Gaza kapigane nao.
 
Kumbe ni wale ndugu katika imaani? Nilitaka kushangaa, Uturuki anauweza muziki wa Mossad?
Aisee hv kwa nn watu mnapenda sana kuingiza dini kwenye masuala kama haya...!!!.hv Israel ukiitenganisha na Marekani ina kipi cha zaidi kuishinda nchi kama Uturuki au Irani...???...
hv Marekani akikaa pembeni Israel anaweza kusimama peke yake kushindana na Irani ktk nyanja ipi..???...kiuchumi unafahamu Irani ni ya ngapi duniani ukiilinganisha na Israel...?...na hapo Irani yuko kwenye vikwazo miaka na miaka..!!!..
....Imani isikufanye ukajadili jambo la msingi kwa upendeleo...ww umezaliwa na kuwakuta wazazi wako wakristo ndio maana ukawa mkristo....kuna mwingine amezaliwa na kuwakuta wazazi wake islam na yy automatical akafuata huko...
Watanzania bado hatujawa kama Wazungu.... wenyewe wanafuata dini wakiwa na ufahamu nayo na wanaichanganua ndani hasa ndio wanaamua kuwa huo upande...ndio maana kwao issue ya kuabudu sio suala kubwa sana kama ss ngozi nyeusi...tunaozaliwa na kufuata dini za wazazi wetu.
Hao Israel wenyewe tunaowapigania wanampinga huyu kristo wetu hadharani kabisa...kwa nn sasa wanafanya hv???

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Kama hawataelewa hapa, basi hao ni sikio la kufa
 
Usichokijuwa Marekani na Israel ni sawa na National na Panasonic hujui ulichokiandika.

Ukienda duka la electronics kununuwa TV ya TCL basi ujuwe umenunuwa Hitachi.

Kama huna akili timamu ndio unaweza kudhani Marekani na Israel ni watu tofauti, jeuri ya Wamarekani inatoka kwa Wayahudi huu ndio ukweli ambao huujui.

Halafu ukija kwenye issue za dini, ni kwamba kwanza Hakuna dini, ni Utapeli tu wa miaka mingi ulioratibiwa kwa umakini na watu wenye akili.

Kama MNA akili timamu mnaambiwa Uislamu na Ukristo na Uyahudi ni dini za Ibrahim mpaka hapo bado hamgundui Utapeli?

Ni mtu mjinga peke yake ndio anaweza kufia dini.
 
Haahahaha daa hatar sana!!umejiita PHD ,kwa ulichokiandika hakina tofauti na na yule mtoto wa mitaani mvuta bangi aliekimbia shule. Sasa kama akili ya Phd yenyewe ndio hii bc kusoma sana hakuna maana.
 
Usichokijuwa Marekani na Israel ni sawa na National na Panasonic hujui ulichokiandika.

Ukienda duka la electronics kununuwa TV ya TCL basi ujuwe umenunuwa Hitachi.

Kama huna akili timamu ndio unaweza kudhani Marekani na Israel ni watu tofauti, jeuri ya Wamarekani inatoka kwa Wayahudi huu ndio ukweli ambao huujui.

Halafu ukija kwenye issue za dini, ni kwamba kwanza Hakuna dini, ni Utapeli tu wa miaka mingi ulioratibiwa kwa umakini na watu wenye akili.

Kama MNA akili timamu mnaambiwa Uislamu na Ukristo na Uyahudi ni dini za Ibrahim mpaka hapo bado hamgundui Utapeli?

Ni mtu mjinga peke yake ndio anaweza kufia dini.
Halafu kwa ushauri tu, usitumie akili yako ya kawaida au ulioipata kutoka kwa wazungu kujadili mambo ya dini maana hao wazungu wenyewe hawajui chochote kuhusu Ibrahim, na bado unasema dini ujinga lakin unakubali kama kulikua na nabii Ibrahim ni mambo ya ajabu .
 
Back
Top Bottom