Hatua ya serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo China haiwezi kutatua changamoto za kimsingi za kibiashara

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1704356305390.png

Hatua ya Marekani kuongeza muda wa kusamehe nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za China chini ya ‘Kifungu cha 301’ mpaka Mei 31, 2024 imepongezwa sana na jamii ya wafanyabiashara, lakini bado kuna mapungufu, kwani hatua za Marekani katika kuboresha biashara ya pande mbili bado zina vizuizi.

Tangu mwaka 2018 wakati Marekani ilipoanza vita ya kibiashara dhidi ya China, dunia nzima, mnyororo wa ugavi duniani na uhusiano kati ya China na Marekani vimepitia mabadiliko makubwa na magumu, ambayo yalipaswa Marekani kuachana na mawazo yake ya kizamani na kujenga upya sera zake za kibiashara kuhusu China.

Mwaka 2018, rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump, alichukua hatua ya kwanza katika vita ya biashara na China kwa kuweka nyongeza ya ushuru kwa baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China. Sera za kibiashara za Trump zilipingwa na jamii ya wafanyabiashara, na kuilazimisha serikali ya nchi hiyo kuondoa orodha ndefu ya bidhaa zinazotengenezwa China katika nyongeza ya ushuru kama sehemu ya vita ya kibiashara.

Busara ya kiuchumi nyuma ya kuondolewa kwa nyongeza ya ushuru inaonyesha wazi utaratibu chanya wa kiuchumi ambao umekuwa ukiunga mkono maendeleo endelevu ya nchi za China na Marekani. Idadi ya vipengele vya bidhaa za China zinazofurahia ondoleo hili inapaswa kuongezwa, na sio kupunguzwa.

Kama ambavyo Shirika la Habari la Reuters lilivyoripoti, utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump awali ulitoa punguzo la nyongeza ya ushuru kwa zaidi ya bidhaa 2,200 ili kutoa unafuu kwa baadhi ya viwanda na maduka. Muda wa punguzo hilo kwa bidhaa nyingi ulimalizika, lakini muda wa bidhaa 549 uliongezwa kwa mwaka mmoja, na kumalizika mwishoni mwa mwaka 2020. Mwezi Machi, 2022, Marekani ilirejesha tena hatua ya kuondoa nyongeza ya ushuru kwa bidhaa 352 kati ya 549 katika kipengele cha bidhaa zinazoagizwa kutoka China kutoka kwenye kile kinachoitwa “Kipengele cha 301” baada ya muda wa awali uliowekwa kumalizika.

Mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, Ofisi ya Biashara ya Marekani ilitangaza kuongeza Zaidi muda wa kuondolewa nyongeza ya ushuru kwa bidhaa 352 zinazoagizwa kutoka China na bidhaa 77 zinazohusiana na COVID-19 mpaka tarehe 31 Mei, mwaka huu wa 2024.

Ikilinganishwa na orodha ya awali ya aina 2,200 za bidhaa, hatua hii ya kuondoa ushuru wa forodha inaonekana kuwa ni ndogo sana. Kama Marekani haiwezi kuondoa nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za China haraka iwezekanavyo na kutafuta kurejesha uhusiano wa pande mbili wa uchumi na biashara katika njia ya kawaida, basi japo iongeze orodha ya bidhaa zinazoondolewa ushuru, hatua ambayo itasaidia kuboresha biashara ya pande mbili na kuchukua nafasi muhimu katika kutuliza mnyororo wa ugavi duniani.

Zaidi sana, Marekani inapaswa kufanya marekebisho sera yake kuendana na maendeleo ya sasa ya biashara duniani. Kama nchi hiyo itadumisha sera yake ya sasa ya kibiashara, inayojumuisha nyongeza ya ushuru na kufutiwa ushuru, itakuwa vigumu kwake kuendana na mahitaji ya sasa ya maendeleo, hivyo ni wazi kuwa mabadiliko ya kimsingi ni lazima yafanyike.

Mwaka 2018, wachumi wengi waliamini kuwa, hatua ya Marekani kuongeza ushuru wa ziada ungeathiri sana biashara ya nje ya China. Lakini miaka mitano imepita sasa, na ukweli ni kwamba, China imejiingiza Zaidi katika mnyororo wa ugavi duniani na inapanua mtandao wake wa biashara. Fursa ya utengenezaji nchini China haijaathirika, na badala yake, imeendelea kuimarika.

Mabadiliko mengine ni kwamba, ufanisi wa vizuizi vya kiteknolojia vya Marekani unadhoofika. Simu mpya ya kisasa ya Huawei Mate 60 Pro, ambayo baadhi ya watu wanahisi inatumia chip yenye uwezo wa teknolojia ya 5G, inafanya sekta ya semiconductor ya China kuonekana kuwa imara kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi. Sera ya kibiashara ya Marekani iliyoanza kutumika miaka mitano iliyopita haijaleta matokeo yaliyotarajiwa, na badala yake, imekuwa na athari hasi kwa biashara kati ya China na Marekani, na uchumi wa Marekani. Sasa, huu ni wakati wa kufanya mabadiliko.

Kuongeza muda wa kuondoa nyongeza ya ushuru wa forodha hadi Mei 31 mwaka huu si suluhisho la kimsingi la changamoto za pande mbili, bali hatua hiyo inachukuliwa kama kumbukumbu ya busara ya kiuchumi nyuma ya kuondolewa kwa ushuru huyo. Wanasiasa wa Marekani wanapaswa kufanya marekebisho kutokana na utegemezi wa kiuchumi kati ya China na Marekani.
 
View attachment 2861549

Mshauri wa uchumi wa USA labda atakuwa Netanyahu
 
Back
Top Bottom