Sakata la ununuzi wa S-400: Marekani yaiwekea vikwazo Uturuki

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,335
7,705
Habari!

Marekani imetangaza rasmi [Jumatatu] kuiwekea vikwazo Uturuki baada ya Ankara kutekeleza mpango wake wa ununuzi wa mfumo wa kijeshi wa ulinzi wa anga ujulikanao kama S-400 kutoka nchini Urusi.

Takribani mwaka mmoja na nusu baada ya Uturuki kununua mfumo huo, Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi vikwazo kwa taifa hilo ambalo pia ni nchi mwanachama wa jumuiya ya NATO.

Chini ya sheria ya vikwazo iliyopitishwa na Bunge la Congress mwaka 2017 ijulikanayo kama Countering America's Adversaries Through Sanctions Act (CAATSA), vikwazo vimelilenga shirika linalohusika na masuala ya ununuzi lililo chini ya Wizara ya Ulinzi ya Uturuki pamoja na maafisa wa ngazi za juu akiwemo rais wa shirika hilo.

Vikwazo vya Jumatatu vinamaanisha kuwa, shirika hilo limefutiwa leseni za ununuzi wa bidhaa kutoka nchini Marekani likiwemo zuio la kupokea mkopo unaozidi dola milioni 10 kutoka katika benki za Marekani sanjari na zuio la mikopo kutoka katika mashirika ya fedha ya kimataifa kama vile World Bank.

Vikwazo pia vimejumuisha kuzifungia mali pamoja na viza kwa maafisa wa juu wa shirika hilo.

Mengine na zaidi ya haya yatakayokuwa yakijiri kuhusiana na sakata hili tutaendelea kuyafahamu kadri muda utakavyoturuhusu kuyafahamu!

Pia, unaweza kupitia taarifa ya awali kuhusiana na sakata hili:
 
Safi Sana USA. Hili litakua funzo kwa uturuki na wengine kua unafiki haifai.

Cc:India,
. Saudi Arabia
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hivi watu mbona mnakuwa wapumbavu namna hii sasa hapo Uturuki ina kosa gani?
Uturuki atasanda, hapo bado Biden hajaapishwa. Yaani watajua kua hawajui.

Biden ata activate CAATSA, Yaani huyo sultan uchwara ataelewa Shoo maamae
 
Kwa nje, ni vikwazo sababu ya S-400, ila kwa ndani vita baridi kati ya USA against Turkey.
Hii ishu imeanzia kwenye failed coupe d'etat, ikaja ishu ya wakurd na pia kucounter influence ya turkey middle east ambayo inatishia interest za marekani
 
Kumbe unafiki ni kununua silaha unayo iyona ni bora kwa ajili ya usalama wa taifa lako?
Usalama wa taifa gani wakati yupo NATO.
akitaka uhuru huo atoke NATO aone kama Kuna mtu atamkataza kununua silaha Russia.
Huo ndo unafiki yaani upo NATO lakini unataka uwasaidie adui wa NATO.
 
Mbona nimeuliza swali rahisi sana?
Uturuki kafanya kosa gani mpaka ww ufurahie kuwekewa vikwazo?
Hizo ngonjera nyingine achana nazo.
Aache ku destabilize NATO, kwa kushirikiana na maadui wa NATO na kuwa provoke NATO members.

Hilo ndo kosa kubwa alishaonywa mara kadhaa lakini erdogan anajikuta kichwa ngumu, sasa vikwazo ndo vitampa akili, na akiendelea atachapwa.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom