Wapiga kura wa Uturuki hawataunga mkono vibaraka wa Marekani'

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Uturuki inakaribia katika awamu ya "suluhisho la mwisho", ambalo linahusisha kujitenga kabisa na "Mfumo wa Atlantiki" ambao ni wa Kimarekani na huku ikiwa inajikurubisha zaidi na madola yenye nguvu barani Asia, na uchaguzi wa rais wa Uturuki wa mwaka huu utaivuta nchi hiyo karibu na suluhisho hilo.

Haya yamedokezwa na Berke Mustafa Berkil, kiongozi mkuu wa Chama cha Wazalendo cha Uturuki.

Katika mahojiano maalumu na tovuti ya Press TV, mwanasiasa huyo mwandamizi wa Uturuki amesema ukweli kwamba muungano wa wapinzani wa Rais Recep Tayyip Erdogan unaojulikana kama "Meza ya Watu Sita" - ambao aliutaja kama "chombo cha Marekani" - haungeweza kushinda katika duru ya kwanza licha ya majigambo makubwa, unaonyesha wazi kuwa watu wa Uturuki "hawaungi mkono mipango ya Marekani".

Mwanasiasa huyo amesisitiza kuwa, "Taifa la Uturuki halitaunga mkono mipango ya Marekani na halitachagua wale ambao ni vikaragosi wa Marekani." Ameendelea kusema kuwa: "Utabiri wangu ni kwamba Bw. Erdogan atashinda uchaguzi huu. Hata hivyo, uchaguzi huu pekee hautaunda nguvu inayoweza kutatua matatizo ya Uturuki na kanda,” amesisitiza.

Kura ya urais iliyokuwa na mchuano wa karibu iliingia katika duru ya pili baada ya Erdogan kushindwa kupata asilimia 50 ya kura zinazohitajika kuunda serikali mpya na kuongeza muda wake wa miaka 20 kwenye usukani. Erdogan alipata asilimia 49.5 ya kura katika uchaguzi wa huo uliofanyika Jumapili huku mpinzani wake mkuu Kemal Kilicdaroglu akipata asilimia 44.89 – na hivyo uchaguzi umeingia duru ya pili.

Duru ya pili itafanyika Mei 28 huku Erdogan akitabiriwa na wengi kushinda ingawa Kilicdaroglu ameelezea imani kuwa chama chake kitaibuka na ushindi.

Berkil alisema serikali mpya ya Ankara lazima ikubaliane na mabadiliko ya hali halisi ya kisiasa ya duniani ambapo mfumo wa maamuzi ya upande mmoja wa Marekani "unakaribia mwisho".

Usiku wa kuamkia Jumapili, Erdogan aliwaambia wafuasi wake kwamba Rais wa Marekani Joe Biden alikuwa ametoa maagizo ya "kumpindua".

Berkil amesema utawala haramu wa Israel, kama Marekani, pia unawakilisha tishio kwa nchi zote za eneo ikiwa ni pamoja na Uturuki.

Mwanasiasa huyo amesema Kilicdaroglu yuko katika kambi ya Marekani naye Erdogan, yuko upande wa Iran, Russia, China na bara Asia.

Aidha amesema uwezekano wa Kilicdaroglu kushinda duru ya pili ni mdogo sana, na hata kama ataibuka mshindi, taifa la Uturuki halitaunga mkono mipango yake iliyo dhidi ya nchi za kikanda na kupendelea Marekani.
 
Berkil: 'Wapiga kura wa Uturuki hawataunga mkono vibaraka wa Marekani'

May 18, 2023 12:20 UTC

[https://media]

[https://media]Rais Erdogan (kushoyo) na Kilicdaroglu

Berkil amesema utawala haramu wa Israel, kama Marekani, pia unawakilisha tishio kwa nchi zote za eneo ikiwa ni pamoja na Uturuki.

Mwanasiasa huyo amesema Kilicdaroglu yuko katika kambi ya Marekani naye Erdogan, yuko upande wa Iran, Russia, China na bara Asia.

Aidha amesema uwezekano wa Kilicdaroglu kushinda duru ya pili ni mdogo sana, na hata kama ataibuka mshindi, taifa la Uturuki halitaunga mkono mipango yake iliyo dhidi ya nchi za kikanda na kupendelea Marekani.
Erdogan kafikia huku kuitegemea Usa ili kujipatia kiki ya kuchaguliwa?
 
Back
Top Bottom