Sakata la UDA: Bomu lingine lalipuliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la UDA: Bomu lingine lalipuliwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BASIASI, Aug 14, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuchunguza mazingira ya ubinafsishaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), kwa Kampuni binafsi ya Simon Group, HABARILEO Jumapili imegundua ‘madudu’ yaliyoambatana na ubinafsishaji huo.

  Kutokana na uendeshaji mbovu na hasara iliyokuwa inajitokeza kila siku, hatimaye Bodi ya Wakurugenzi ya UDA chini ya Mwenyekiti wake, Idd Simba na Katibu wake, Victor Milanzi, ambaye ndiye alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa UDA, iliamua kumtafuta mwekezaji binafsi ili aliendeshe shirika hilo kwa faida.

  Kabla ya ubinafsishaji huo, UDA ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu, kupitia Hazina, wakiwa na jumla ya hisa milioni 15, kila hisa moja ikiwa na thamani ya Sh 100.

  Kwa mchanganuo, Halmashauri ya Jiji ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa hizo, huku Hazina ikimiliki asilimia 49.

  Kwa zaidi ya wiki moja, gazeti hili lilikutana na vyanzo mbalimbali vilivyohusika kwa namna moja au nyingine katika mchakato wa ubinafsishaji wa shirika hilo, na kubaini kukiukwa kwa baadhi ya vipengele na kanuni zilizotumika kwenye mchakato huo.

  HABARILEO Jumapili ilipata nyaraka zote zilizotumiwa wakati wa ubinafsishaji wa Shirika hilo kwa Simon Group, kampuni inayomilikiwa na Mtanzania, Robert Kisena.

  Februari 11, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA, chini ya Simba, ilikutana na uongozi wa Simon Group ikiongozwa na Kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.535 ya hisa zote kwa thamani ya Sh bilioni 1.142.

  Kwa maana nyingine, mkataba huo ungeifanya Simon Group kuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa UDA kwa vile Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Hazina, wangebaki na hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.465.

  Uchunguzi huo ulibaini, kwamba kwa upande wa UDA, viongozi waliosaini uuzaji wa hisa hizo ni Simba aliyesaini kwa niaba ya Bodi na Milanzi kwa niaba ya Menejimenti wakati kwa upande wa Simon Group, aliyesaini ni Kisena.

  Baada ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka Simon Group kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za UDA (Sh bilioni 1.142) ambazo ni sawa na Sh milioni 285.669, ndani ya siku 14, tangu kusainiwa ili kuufanya mkataba utambulike kisheria, na Simon Group ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo.

  Kwa vile fedha hizo zililipwa Februari 11, baada ya siku 14, vipengele vya mkataba vilipaswa kuanza kushughulikiwa kisheria na hasa namba 4.5 ambacho kiliielekeza Bodi ya UDA, kuitisha mkutano wa wanahisa ndani ya siku 14 ili kushughulikia mambo makuu matano muhimu.

  Mambo hayo yalikuwa ni kwanza, kuitambua Simon Group kama mwekezaji mkubwa ndani ya UDA, akiwa na hisa asilimia 52.535, kuteua Bodi mpya ya uendeshaji wa UDA, ambayo kimsingi ilipaswa kuwa na wajumbe saba; wanne kutoka Simon Group, wawili Jiji na mmoja
  Hazina.

  Jambo lingine muhimu ni kumteua mkaguzi wa mahesabu na kuteua benki zitakazohusika na utunzaji wa fedha za UDA na pia kuandaa mwaka wa mpya wa mahesabu ya fedha ambao ungeanza kutumiwa na UDA mpya.

  Kuuzwa kwa UDA
  Wakati kukiwa na gumzo juu ya nani alihusika na kuuza hisa za UDA, alifanya hivyo lini na kwa gharama gani, HABARILEO Jumapili imebaini kuwa ingawa mkataba wa kuuza hisa za UDA kwa Simon Group ulisainiwa Februari 11, mazungumzo ya mauziano baina ya pande
  hizo mbili yalianza miaka miwili nyuma.

  Kutokana na mazungumzo hayo ya awali, UDA iliiandikia barua Simon Group kuitaka ilipe Sh milioni 400 kama uthibitisho wa nia yake ya kutaka kuiendesha. Barua hiyo iliitaka Simon Group kuingiza fedha hizo kwenye akaunti za Shirika la Pride tawi la Mlimani City na kwenye akaunti ya Simba katika Benki M tawi la Sea View, Upanga.

  Barua hiyo iliieleza Simon kwamba hatua hiyo ya kuitaka kuingiza fedha hizo kwenye akaunti za Pride na ile ya Simba inatokana na akaunti zinazoendeshwa na UDA kuwa na ovadrafti benki, hatua ambayo kama wangeingiza fedha hizo kwenye akaunti hizo za UDA, zingechukuliwa na benki na zisingefanya kazi iliyokusudiwa.

  Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa Simon Group waliitikia mwito huo kwa kuingiza Sh milioni 20 kwenye akaunti ya Pride namba 6033500127 Mlimani City, Februari 09, 2009 na baadaye Sh milioni 250 katika akaunti namba 0210001002 Sea View, Septemba 2, 2009
  ikionesha kumilikiwa na Simba.

  Masaburi na uuzaji UDA
  Akiwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, ambalo ni mmoja wa wanahisa wa UDA, Dk. Didas Masaburi, aliliambia gazeti hili, kwamba aliitisha mkutano wa wanahisa wa UDA ili kujadili uendeshaji wa shirika hilo.

  Alisema kuitishwa kwa mkutano huo, kulitokana na kupokea malalamiko kutoka Simon Group kuhusu kukiukwa vipengele vya mkataba wa mauziano ya hisa za UDA Februari 11.

  Alisema mkutano huo ambao ulifanyika Juni 10, uliibuka na mapendekezo yaliyofikiwa na washiriki waliohudhuria ambayo yalikuwa na lengo la kuongeza ufanisi.

  “Kikao hicho hakikuwa na nia ya kuuza hisa za UDA, UDA ilikuwa imeuzwa tayari tangu Februari 11, hivyo tusingeweza kuuza kitu ambacho tayari kimeuzwa. Sisi tulikutana kuangalia nini kifanyike ili UDA iendelee kutoa huduma za usafiri kwa ufanisi zaidi na ndiyo maana tuliibuka na mapendekezo ambayo ndiyo niliyosaini mimi, si mkataba wa mauziano,” alisema Masaburi.

  Aliongeza kuwa kilichoamuliwa na mkutano huo aliouongoza, ilikuwa ni kuiondoa Bodi ya Wakurugenzi ya UDA ili kuunda mpya, kumwondoa madarakani aliyekuwa Mtendaji Mkuu, Milanzi na kumteua CEO wa muda, Simon Bulenganija na kufunga akaunti zote za UDA, ili kufanya uchunguzi wa mahali zilikokwenda fedha za malipo ya mauzo ya hisa.

  Alisema maagizo hayo yote utekelezaji wake ulianza Juni 10.

  Simon Group na taratibu
  Kisena ni mmiliki na Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group ambaye alisema kampuni yake ilifuata taratibu zote katika ununuzi wa hisa za UDA na ilifanya hivyo ikiwa na lengo zuri la kuboresha sekta ya usafiri Dar es Salaam, ambayo imekuwa ikizorota kutokana na ufanisi duni wa UDA.

  “Tunashukuru, kwani kama unavyojua, Serikali imeagiza suala hili la UDA lichunguzwe na vyombo vya Dola, ili ukweli uweze kujulikana. Nitatoa taarifa kamili kuhusu suala zima la UDA na taarifa yangu itazingatia maeneo makuu manne nikianzia na hali ilivyokuwa kabla ndani ya UDA,” alisema Kisena.

  Kwa upande wake, Bulenganija alisema anaendelea vema na uendeshaji wa UDA tangu alipowekwa madarakani Juni 10, wakati wakisubiri maelekezo zaidi kutoka serikalini baada ya kuagiza suala la UDA lichunguzwe.

  Gazeti hili pia lilifanya juhudi ya kumtafuta Simba ili kuzungumzia sakata hili, ambapo pamoja na kumkuta nyumbani kwake Mikocheni Jumatano, jitihada hizo zilikwama baada ya Simba kupitia mwanawe, Abdul, kumtaka mwandishi kuacha mawasiliano ya simu, ili aweze kumtafuta pindi atakapokuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

  Uchunguzi zaidi wa HABARILEO Jumapili, ulibaini kuwa wakati Bodi ya Simba inavunjwa, katika hatua ya kushangaza, Menejimenti ya UDA ilikuwa imeomba mkopo wa Sh bilioni 3.8 kutoka benki ya NBC ili kununua mabasi ya Kichina, huku uamuzi huo ukifanywa bila wanahisa wa UDA kuhusishwa.

  Barua yenye kumbukumbu namba UDA/P.16/08 ya Mei 26, iliyosainiwa na Milanzi ikielekezwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NBC kupitia kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Minnie Kibuta, ilisema UDA wameamua kuomba mkopo huo, ili kuwasaidia kuboresha sekta ya usafiri Dar es Salaam, huku ikieleza kuwa mali za UDA zingewekwa kama dhamana ya mkopo huo.

   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tumeshaibiwa sana na mashirika yetu mengi yamekufa but gvnt iko kimya.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Narudia tena UDA irudishwe mikononi mwa umma tu kwanza muone watakavyoparaganyana..
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Dawa ni kuipiga chini tu serikali iliyopo na chama chao na kuweka uongozi mpya ndo hii nchi itapona. Hatuwezi kupona km nchi bado inaongozwa na genge la wezi.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi habari hizi zinavyozidi kutolewa ndivyo inavyoonyesha Ujinga mkubwa unavyoweza utumika kudanganya Umma..

  Nimesoma maelezo yote ya UDA kuuzwa lakini bado yanishinda kuelewa. Wenye hisa ni Jiji kwa asilimia 51 na hazina asilimia 49 inakuwaje Simba na UDA ndio waiuze UDA kwa Simion Group?.. Simba na UDA hawa ni watenda kazi tu hawana mamkala yoyote ya kuuza hisa za UDA wakati wao ni waajiriwa tu.. wenye mamlaka ya kuuza Hisa ni jiji au Hazina iweje hawa Simion wanunue hisa kutoka UDA ya Idd Simba!..

  jamani bado tu mnaliendeleza hili deal mfu kwa kujenga hooja ambazo haziingi akilini hata kidogo.. hakuna chochote kilichotokea zaidi ya kwamba Simion Group wameingizwa mjini na Idd Simba ama walitegemea atawasaidia kununua hisa za Jiji au Hazina, deal limejamba kila mmoja wao anatafuta pa kutokea.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,307
  Likes Received: 22,111
  Trophy Points: 280
  Hii nchi bwana, hakika hamna utaratibu wala utawala wa sheria
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Mzee jibu lao wanasema kuwa wamenunua "hisa zisizogawiwa" za UDA na wametetea hivyo kiujanja kuwa UDA iilkuwa na uwezo wa kuuza hisa hizo kwa sababu zilikuwa "zake". Hata ukikubali dhana hiyo wanajikuta wanaingia kwenye matatizo kwani kama zilikuwa ni hisa tu za UDA kwanini Simon Group ikataka kuchukua na menejimenti?

  right on.. ndio maana tunataka kuweka wazi kwanza kwamba UDA haiuziki ndio uone watakavyovurugana. taarifa ya serikali iliyotolewa wiki iliyopita ilionesha kuwa wanataka kutafuta suluhisho na mwekezaji ili kila mmoja awe safi; kwamba watakualiana jamaa alipe hela zilizobaki, bodi na serikali washirikishwe n.k and then simon anaondoka na UDA huu ndio mpango wenyewe.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,326
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mkandara, kwanza hesabu ya hisa kwenye story hii bado haijakaa vizuri. Kama jumla ya hisa ni Milioni 15 na zinamilikiwa kwa uwiano wa 49% serikali kupitia msajili wa hazina na 51% zinazomilikiwa na Halmashauri ya jiji ambaye ndiye majority shareholder, then uwezo wa jiji kuuza hisa zake una ukomo wa zile 51% tuu ambazo zinge consitute hisa milioni 7.65. Kitendo cha kuuza hisa milioni 7.8 zikiwemo hisa za serikali bila kibali cha msajili wa hazina, tayari kunaifanya hiyo sale kuwa null and void ab initio, (tangu mwanzo).

  Pia kwenye articles of association ya UDA na memorandum zake, zinaelekeza vikao halali vya bodi na mahudhurio yenye kuweza kutoa board resolution ya kuuza hisa zake, Ist priority ni kwa mbia ambaye ni serikali, baada ya serikali kuonyesha haina interest ndipo wangeuza hisa hizo kwa public kwa ushindani wa wazi with the best offer ndipo huyo Simon Group ashinde, apewe.

  Kwa vile Mmiliki wa Simon Group ni mtu mwenye good conbections, hata kama ripoti ya CAG itaonyesha madudu ya ajabu, tusishangae kama Msajili wa Hazina nae ataamua ku off load hisa zake na kumkabidhi rasmi Kisena kumiliki 100%!. Na ukifanya investigative journalism, utashanga na names behind Kisena!. Ukifuatilia sana wanaweza hata waka ku-Stan Katabalo!.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Jidulabambasi...
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa sana Iddi Simba huwa hatosheki jamani?
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  exactly pasco. uda wameuza na sehemu ya shares za hazina. na isitoshe kama mmiliki mmojawapo anataka kuuza shares zake zote na ziada ya zisizo zake inakuwaje wanahisa wengine wasitaarifiwe?
  pili, kama shirika lina overdrafts kwenye account zake na kuamua kulipia hela kwenye makampuni binafsi,huo sio wizi wa kimachomacho? yaani shirika la umma linaendeshwa kama kampuni ya mhindi na wanae au mchaga na shemeji zake?
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwanini UDA pekee ?

  je jamii inafahamu kiwanda cha mgororo kilivyobinafsishwa kwa shs mamilioni ya shs tu?
  kuna mashirika mangapi yalibinafsishwa kijinga? je tuanze kuyachambua yote au tatizo ni UDA?
   
 13. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,314
  Trophy Points: 280
  Navyojua huiwezi kuonunua kampuni eti ukanunua "assets" bila "liabilities" zake.
  Kama kile kiwanja pale kurasini ndio kimewavutia ili kukodisha kwa watu wa kuhifadhi makontena, wanapaswa kukubali pia kuchukua madeni ya hizo overdraft benki.
  Pili Idd Simba ashitakiwe kwa kudanganya hadharani kua hela walizolipa kina Kisena ni malipo ya ushauri wa kibiashara aliokua akiwapa na sio za uuzwaji wa UDA wakati Kisena mwenyewe anadai hakuna biashara nyingine yoyote ya ushauri aliofanya na Simba zaidi ya kuuziana UDA.
  Tunapenda kulalamika sana juu ya wale waliotufikisha hapa tulipo kwa mikataba mibovu, leo tushampata huyu mmoja, itasikitisha sana kama tukimuachia hivihivi.
   
 14. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />


  Yupo hai?
   
 15. Lord

  Lord Member

  #15
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyo ndo simba mla nyama atatosheka vipi???
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Yachambuliwe yote!
   
 17. n

  nchasi JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Suluhisho ni kuwaondoa na kuwashughulikia ili warudishe walivyopora. Lakini wakiendelea kutawala watatunyonya bila huruma hawa wachumia matumbo yao. Hawana huruma hata kidogo.
   
 18. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukisoma hii hbr unatamani kulia. Lini haya mambo yataisha?
   
 19. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  wakulaumiwa ni serikali na watendaji wake wasiyo waaminifu.lakini simon bado sijaona kosa lake kwa sababu alikuwa anafuata maelekezo ya uda.wamemuandikia barua pesa ziingizwe sehemu furani kwa sababu 1,2,3.akafanya hivyo.hata jana alipokuwa anahojiwa na waandishi wa habari alijibu vizuri na kuwafafanulia kila kitu lakini wa kulaumiwa ni jiji la dar es salaam na hazina kwa sababu walitakiwa wawepo lakini hawakufanya hivyo kitu ambachokimefanya tuwe na taarifa za upande mmoja.je serikali wamedanganywa wapi?
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145


  katika mashirika ya umma yaliyobinafsishwa kuna mengine walipewa bure kabisa kama kiwanda cha mgololo na sijasikia kelele za wananchi kupigwa nina hamu na harakati za UDA lakini nashindwa pa kuanzia kwani isijekuwa ni vita ya panzi tukauana wenyewe kwa wenyewe kwani kuna watu wanashambulia elimu mpaka ya mmiliki sasa sijui kama mtu akiwa na elimu ndogo anazuiwa kumiliki mali

  sipendi ufisadi daima ila nashindwa kuingia kwenye migogoro ya maslahi ya watu fulani

  ndio maana sijajiingiza katika sakata la kudai umeme unakatika katika kwani wananchi wa vijijini hatujawatetea na wamekaa gizani kwa miaka yote toka uhuru ambao ni zaidi ya asilimia 80% iweje leo tulio mijini ambao ni asilimia na tulio mijini ambao tunapata umeme ni asilimia 10% .

  tuanze kutazama ubinafsishaji wa mashirika yote , na tuanze kudai upatikanaji wa umeme nchi nzima na si mijini tu. tukifika hapo basi mtu kwa mtu na kijiji kwa kijiji kitaingia kwenye mapambano ya kudai umeme na mashirika yetu likiwemo UDA pia
   
Loading...