Sakata la UDA: Bomu lingine lalipuliwa!

<b>kwanini UDA pekee ?<br />
<br />
je jamii inafahamu kiwanda cha mgororo kilivyobinafsishwa kwa shs mamilioni ya shs tu?<br />
kuna mashirika mangapi yalibinafsishwa kijinga? je tuanze kuyachambua yote au tatizo ni UDA?<br />
</b>
<br />
<br />
Huenda sijakuelewa? Hivi unataka tusijadili UDA COZ kuna mashirika mengine yalibinafsishwa kijinga?

Hatuwezi kuendeleza "ujinga" wa namna hii. Kutokataa kuendelea kuibiwa ni upumbavu. Sisi siyo wapumbavu.

Tusiposimamia raslimali za nchi vizazi vijavyo vitafukua makaburi yetu na kuchoma mifupa na kutupa majivu baharini ili wapate maeneo ya kuendesha shughuli za uchumi. Majivu ya mifupa yetu iwe chakula cha samaki ili wawavue na kuongeza kipato.

Tupambane na ufisadi sasa kwani tukisubiri kesho tutakuwa tumechelewa.
 
huu utawala uliopo toka enzi za mzee ruksa ni mtandao wa wezi,hamna uzalendo.Wezi wanaiba na wanateteana na kukingiana vifua.Hapa dawa ni kuwa na utawala mpya usio na damu ya ccm naamini haki itatendeka.
 
sasa tutampa nani UDA hii watanzania wote hawaaminiki yani hata mwenyewe nahisi ni walewale tu, yani chozi la uzalendo linantoka, basi tuwaige wachina wala rushwa na mafisadi tukawafolenishe uwanya wa taifa pale kati afu tutandike bullet wafie mbali
 
Mzee jibu lao wanasema kuwa wamenunua "hisa zisizogawiwa" za UDA na wametetea hivyo kiujanja kuwa UDA iilkuwa na uwezo wa kuuza hisa hizo kwa sababu zilikuwa "zake". Hata ukikubali dhana hiyo wanajikuta wanaingia kwenye matatizo kwani kama zilikuwa ni hisa tu za UDA kwanini Simon Group ikataka kuchukua na menejimenti?
Nakusikia mkuu wangu halafu haiwezekani UDA kuwa na share ikiwa Ubinafsishaji wake hatujawahi kuusikia.. Na kama ilifanyika kimya kimya - Basi ndio Ufisadi wenyewe huo tunaoiupiga vita. Isichunguzwe tu huku kuuziana kwa Simion na Idd Simba bali uvunjaji wa sheria ktk ubinafsishaji wa mashirika ya Umma. Tena ingekuwa vizuri kuwa sababu ya kutazama ubinafsishaji wa mashirika yote ya Umma....

Pasco,
Mkuu wangu hakuna kinacho eleweka hata kidogo.. Na tukijaribu kuelewa mchezo ulochezwa tunachezwa sisi. Tunachofahamu sisi wananchi - UDA haijauzwa, haija binafsishwa na wala hizi habari za share inabidi zifanyiwe uchunguzi upya kabisa kwani nakumbuka vizuri sana ktk utetezi wa Idd Simba yeye alihusisha sana wizara ya Uchukuzi ktk hatua za uuzwaji wa shirika hili kupitia Kampuni hodhi ya mashirika ya Umma (CHC) hakutaja hata sehemu moja Jiji wala Hazina. Pale ilikuwa kutupeleka nje kabisa ya kuwahusisha Halmshauri ya jiji (City) na uuzwaji wa share zake, leo tumepata habari zaidi za jinsi walivyohusiak na Meya kuwa ndani ya mchezo mzima.. Haya mara tunaambiwa sijui share ambazo zilikuwa bado hazijagawiwa! wakati huo huo City wana own 51% na Hazina 49% ni zipi ambazo haizjagawiwa! Na pia CHC na wizara ya Uchukuzi wamesimama wapi ktk umiliki wa hili shirika... UChawi mtupu!
 
Narudia tena UDA irudishwe mikononi mwa umma tu kwanza muone watakavyoparaganyana..

Samahani Mkuu jana wakati naangalia Mdahalo ambapo mzee SIMON alikuwa akijibu Hoja alisema UDA haikuwa shirika la UMMA, kwa kuwa haikusajiliwa kwa sheria ya makampuni ya 2 cap 1 /2 cap 2 ( Sikumbuki vizuri) ila kuna kitu alisema UDA ilikuwa ni LTD na sio ya UMMA, Vipi Kuna ukweli wowote hapo?
 
Shaloom wana JF!

Nchi hii kwakweli ni kuzungumkuti kabisa kwani mtu kama Simba na Masaburi wametumia trick moja tu kuwa TZ hakuna serikali yaani mwenye kisu kikali ndio mla nyama wamesoma weakness za nchi na wame-take advantage kuuza shirika la UDA bila hata kuwa na aibu na kuongopa jela kwani nchi kama China ni bullet au kifo cha maisha. Enzi za nchonga meno wote waliohusika wangekuwa muda huu wako Keko wanauliza maswali imekuwaje?
 
Inasikitisha kuwa wauzaji wote ni waajiriwa tu Hazina na Jiji hawana taarifa za kuuza hisa, pesa zinawekwa kwenye ac ya mrundi mmoja, hapo kuna tatizo tena siyo dogo hawa watu wanatakiwa kutiwa magerezani haraka sana!
 
Samahani Mkuu jana wakati naangalia Mdahalo ambapo mzee SIMON alikuwa akijibu Hoja alisema UDA haikuwa shirika la UMMA, kwa kuwa haikusajiliwa kwa sheria ya makampuni ya 2 cap 1 /2 cap 2 ( Sikumbuki vizuri) ila kuna kitu alisema UDA ilikuwa ni LTD na sio ya UMMA, Vipi Kuna ukweli wowote hapo?

Mkuu kasome ujue maana na neno Ltd. The fact kuwa kampuni ni Ltd haina maana kuwa haiwezi kuwa ya Umma. A Limited company is a company in which the liability of the members or subscribers of the company is limited to what they have invested or guaranteed to the company. Kwa hiyo umma unaweza ku subscribe to the company. Mbona Tanzania Railway ni limited company na inamilikiwa na serikali 100%?
 
Mkuu kasome ujue maana na neno Ltd. The fact kuwa kampuni ni Ltd haina maana kuwa haiwezi kuwa ya Umma. A Limited company is a company in which the liability of the members or subscribers of the company is limited to what they have invested or guaranteed to the company. Kwa hiyo umma unaweza ku subscribe to the company. Mbona Tanzania Railway ni limited company na inamilikiwa na serikali 100%?

Asante ukweli ni kuwa SIJUHI KUSOMA , Vipi wewe MSOMI? unaweza kunisaidia kufafanua Tofauti ya USAJILI wa KAMPUNI kupitia SHeria hizo za 2 cap 2 na 1 cap 2 ( Sinauwakika kwani ili nililisikia na kuona jana kwenye TV)

Kuhusu LTD pia sijuhi ila nachokumbuka Simoni alitoa mfano kwa Kubenea na kumuambia kampuni yake ni LTD na ina Unallote shares kam nakumbuka vizuri.

Nasubiri majibu yako MSOMI mimi KILAZA.
 
wachina wanasema kuhusiana na maendeleo ya nchi yao kuwa,''EVERY THING STARTED FROM MAO'' Na sisi tuseme kuhusu huu uuzaji wa mashirika kifisadi kuwa''EVERY THESE STARTED FROM MKAPA''
 
hivi Mkapa ndio matokeo yake haya... kweli Baba wa Taifa katika makosa aliyoyafanya ni kumkabidhi kiti Mwinyi na Mkapa imekula kwetu
 
Yaani nchi hii sijui tuko katika sayari ipi maana mambo yake ni klichechefu kila kukicha
 
wakati waziri mkuu, mizengo pinda, ameagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (cag), kuchunguza mazingira ya ubinafsishaji wa shirika la usafiri dar es salaam (uda), kwa kampuni binafsi ya simon group, habarileo jumapili imegundua ‘madudu’ yaliyoambatana na ubinafsishaji huo.

Kutokana na uendeshaji mbovu na hasara iliyokuwa inajitokeza kila siku, hatimaye bodi ya wakurugenzi ya uda chini ya mwenyekiti wake, idd simba na katibu wake, victor milanzi, ambaye ndiye alikuwa ofisa mtendaji mkuu (ceo) wa uda, iliamua kumtafuta mwekezaji binafsi ili aliendeshe shirika hilo kwa faida.

kabla ya ubinafsishaji huo, uda ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya halmashauri ya jiji la dar es salaam na serikali kuu, kupitia hazina, wakiwa na jumla ya hisa milioni 15, kila hisa moja ikiwa na thamani ya sh 100.

Kwa mchanganuo, halmashauri ya jiji ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa hizo, huku hazina ikimiliki asilimia 49.

Kwa zaidi ya wiki moja, gazeti hili lilikutana na vyanzo mbalimbali vilivyohusika kwa namna moja au nyingine katika mchakato wa ubinafsishaji wa shirika hilo, na kubaini kukiukwa kwa baadhi ya vipengele na kanuni zilizotumika kwenye mchakato huo.

Habarileo jumapili ilipata nyaraka zote zilizotumiwa wakati wa ubinafsishaji wa shirika hilo kwa simon group, kampuni inayomilikiwa na mtanzania, robert kisena.

Februari 11, bodi ya wakurugenzi ya uda, chini ya simba, ilikutana na uongozi wa simon group ikiongozwa na kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba uda ilikuwa imeiuzia simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.535 ya hisa zote kwa thamani ya sh bilioni 1.142.

Kwa maana nyingine, mkataba huo ungeifanya simon group kuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa uda kwa vile halmashauri ya jiji la dar es salaam na hazina, wangebaki na hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.465.

Uchunguzi huo ulibaini, kwamba kwa upande wa uda, viongozi waliosaini uuzaji wa hisa hizo ni simba aliyesaini kwa niaba ya bodi na milanzi kwa niaba ya menejimenti wakati kwa upande wa simon group, aliyesaini ni kisena.

Baada ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka simon group kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za uda (sh bilioni 1.142) ambazo ni sawa na sh milioni 285.669, ndani ya siku 14, tangu kusainiwa ili kuufanya mkataba utambulike kisheria, na simon group ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo.

Kwa vile fedha hizo zililipwa februari 11, baada ya siku 14, vipengele vya mkataba vilipaswa kuanza kushughulikiwa kisheria na hasa namba 4.5 ambacho kiliielekeza bodi ya uda, kuitisha mkutano wa wanahisa ndani ya siku 14 ili kushughulikia mambo makuu matano muhimu.

Mambo hayo yalikuwa ni kwanza, kuitambua simon group kama mwekezaji mkubwa ndani ya uda, akiwa na hisa asilimia 52.535, kuteua bodi mpya ya uendeshaji wa uda, ambayo kimsingi ilipaswa kuwa na wajumbe saba; wanne kutoka simon group, wawili jiji na mmoja
hazina.

Jambo lingine muhimu ni kumteua mkaguzi wa mahesabu na kuteua benki zitakazohusika na utunzaji wa fedha za uda na pia kuandaa mwaka wa mpya wa mahesabu ya fedha ambao ungeanza kutumiwa na uda mpya.

Kuuzwa kwa uda
wakati kukiwa na gumzo juu ya nani alihusika na kuuza hisa za uda, alifanya hivyo lini na kwa gharama gani, habarileo jumapili imebaini kuwa ingawa mkataba wa kuuza hisa za uda kwa simon group ulisainiwa februari 11, mazungumzo ya mauziano baina ya pande
hizo mbili yalianza miaka miwili nyuma.

Kutokana na mazungumzo hayo ya awali, uda iliiandikia barua simon group kuitaka ilipe sh milioni 400 kama uthibitisho wa nia yake ya kutaka kuiendesha. Barua hiyo iliitaka simon group kuingiza fedha hizo kwenye akaunti za shirika la pride tawi la mlimani city na kwenye akaunti ya simba katika benki m tawi la sea view, upanga.

Barua hiyo iliieleza simon kwamba hatua hiyo ya kuitaka kuingiza fedha hizo kwenye akaunti za pride na ile ya simba inatokana na akaunti zinazoendeshwa na uda kuwa na ovadrafti benki, hatua ambayo kama wangeingiza fedha hizo kwenye akaunti hizo za uda, zingechukuliwa na benki na zisingefanya kazi iliyokusudiwa.

Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa simon group waliitikia mwito huo kwa kuingiza sh milioni 20 kwenye akaunti ya pride namba 6033500127 mlimani city, februari 09, 2009 na baadaye sh milioni 250 katika akaunti namba 0210001002 sea view, septemba 2, 2009
ikionesha kumilikiwa na simba.

Masaburi na uuzaji uda
akiwa meya wa jiji la dar es salaam, ambalo ni mmoja wa wanahisa wa uda, dk. Didas masaburi, aliliambia gazeti hili, kwamba aliitisha mkutano wa wanahisa wa uda ili kujadili uendeshaji wa shirika hilo.

Alisema kuitishwa kwa mkutano huo, kulitokana na kupokea malalamiko kutoka simon group kuhusu kukiukwa vipengele vya mkataba wa mauziano ya hisa za uda februari 11.

Alisema mkutano huo ambao ulifanyika juni 10, uliibuka na mapendekezo yaliyofikiwa na washiriki waliohudhuria ambayo yalikuwa na lengo la kuongeza ufanisi.

“kikao hicho hakikuwa na nia ya kuuza hisa za uda, uda ilikuwa imeuzwa tayari tangu februari 11, hivyo tusingeweza kuuza kitu ambacho tayari kimeuzwa. Sisi tulikutana kuangalia nini kifanyike ili uda iendelee kutoa huduma za usafiri kwa ufanisi zaidi na ndiyo maana tuliibuka na mapendekezo ambayo ndiyo niliyosaini mimi, si mkataba wa mauziano,” alisema masaburi.

Aliongeza kuwa kilichoamuliwa na mkutano huo aliouongoza, ilikuwa ni kuiondoa bodi ya wakurugenzi ya uda ili kuunda mpya, kumwondoa madarakani aliyekuwa mtendaji mkuu, milanzi na kumteua ceo wa muda, simon bulenganija na kufunga akaunti zote za uda, ili kufanya uchunguzi wa mahali zilikokwenda fedha za malipo ya mauzo ya hisa.

Alisema maagizo hayo yote utekelezaji wake ulianza juni 10.

Simon group na taratibu
kisena ni mmiliki na mwenyekiti mtendaji wa simon group ambaye alisema kampuni yake ilifuata taratibu zote katika ununuzi wa hisa za uda na ilifanya hivyo ikiwa na lengo zuri la kuboresha sekta ya usafiri dar es salaam, ambayo imekuwa ikizorota kutokana na ufanisi duni wa uda.

“tunashukuru, kwani kama unavyojua, serikali imeagiza suala hili la uda lichunguzwe na vyombo vya dola, ili ukweli uweze kujulikana. Nitatoa taarifa kamili kuhusu suala zima la uda na taarifa yangu itazingatia maeneo makuu manne nikianzia na hali ilivyokuwa kabla ndani ya uda,” alisema kisena.

Kwa upande wake, bulenganija alisema anaendelea vema na uendeshaji wa uda tangu alipowekwa madarakani juni 10, wakati wakisubiri maelekezo zaidi kutoka serikalini baada ya kuagiza suala la uda lichunguzwe.

gazeti hili pia lilifanya juhudi ya kumtafuta simba ili kuzungumzia sakata hili, ambapo pamoja na kumkuta nyumbani kwake mikocheni jumatano, jitihada hizo zilikwama baada ya simba kupitia mwanawe, abdul, kumtaka mwandishi kuacha mawasiliano ya simu, ili aweze kumtafuta pindi atakapokuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Uchunguzi zaidi wa habarileo jumapili, ulibaini kuwa wakati bodi ya simba inavunjwa, katika hatua ya kushangaza, menejimenti ya uda ilikuwa imeomba mkopo wa sh bilioni 3.8 kutoka benki ya nbc ili kununua mabasi ya kichina, huku uamuzi huo ukifanywa bila wanahisa wa uda kuhusishwa.

Barua yenye kumbukumbu namba uda/p.16/08 ya mei 26, iliyosainiwa na milanzi ikielekezwa kwa mkurugenzi mtendaji wa nbc kupitia kwa mtu aliyetajwa kwa jina la minnie kibuta, ilisema uda wameamua kuomba mkopo huo, ili kuwasaidia kuboresha sekta ya usafiri dar es salaam, huku ikieleza kuwa mali za uda zingewekwa kama dhamana ya mkopo huo.


bodi ya wakurugenzi inao uwezo wa kutafuta managing agent tu lakini sio kuuza shirika kwa kuwa bodi ya wakurugenzi ni wasimamizi t na sio wamiliki. Hawa wote ni wezi wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
hii nchi inaliwa na watu wachache lakini hawatosheki ...
 
Sijaelewa lengo la mwandishi huyu wa habari ni nini? Kuna aina ya uandishi wa habari hapa Tanzania wa ajabu sana uwa nashindwa kuelewa ni aina ya elimu ya uandishi tunayowapa watu wetu au ni kuwa kila mwandishi wa habari anapofungua milango yake ufahamu kwa ajili ya kuandika jambo mara zote wengi wao wanaendeshwa na hisia binafsi na hivyo kujikuta habari inayotolewa inakuwa si habari tena bali ni ripoti ambayo inakuwa na malengo maalum na ufafanuzi maalum.

Huyu Jamaa nadhani hayupo sawa kisawasawa; ana andika, "UDA iliuza hisa 52.5% kwa Simon na ku advocate kuwa mauzo hayo kwa mujibu wa huo mkataba zingeiacha Jiji na Hazina kubaki na hisa 47.5%" taarifa si sahihi kwa sababu hisa za UDA ni Jiji 51% na Hazina 49% sasa zikiuzwa 52.5% haoni kuwa ama hisa za Jiji ziliuzwa zote? au basi atwambie kama zilizouzwa zilizo ni nusu za hazina na kadhaa za jiji kufanya hiyo 52.5%?! mbona hakutoa ufafanuzi juu mchanganuo wa hisa zilizokubaliwa kuuzwa?

Alafu anasema "Habari leo Jumapili imebaini kuwa ingawa makatab wa kuuza hisa za UDA kwa simon .., ulisainiwa February, 2011 mazungumzo ya mauziano baina ya pande mbili hizo yalifanyika miaka miwili nyuma" ana fikisha ujumbe gani hapa? mbona hajatwambi ushahidi wa hilo? kama anajenga hisia kuwa simon ilikwisha kubaliwa kununua UDA siku nyingi mbona hasemi hayo makubaliano ya miaka miwili nyuma yalifanywa na wakina nani? na labda hapo ndipo pia angeweza kuainisha hisa zilizo uzwa ziligawanywa vipi?

Kila nikisoma hii habari sioni kama imekaa kama habari labda kama mimi ndio naisoma nikiwa nimechoka. Kuna moja niliona kwenye fb-wall ya Mwanakijiji inasema "Kapteni Lowasa apambana, kambi yake yashambulia ya kikwete Jenerali shimbo na Jairo wajeruhiwa" nilibaki kucheka maana huyu yeye aliweka wazi akili yake kuwa watu wote wanaikosoa serikali ya kikwete ni kambi ya huyo kapteni Lowasa, mwandishi na Muhariri wote bado wamelala kiasi hicho, wao hawakuona makosa aliyofanya Jairo bali waliona wanajeruhiwa na mapambano ya Lowasa! ajabu sana.

Huyu mwandishi wa habari anajiuma uma hapa ila sioni kama hii ni habari iliyosimama kama habari, hakuna taarifa yoyote ya maana aliyokuja nayo mpya hapo ambayo watanzania walikuwa hawaijui hisipo hiyo anayotaka kuyuamnisha kuwa simon ilikwisha kubaliwa kuuziwa UDA miaka miwili nyuma, ingawa hatwambii uhalali wa hayo makubaliano na walioshiriki.
 
They want us to live in a permanent state of frustration!
Likitoka hili linaingia lile huku wahusika wakiwa hawajali wala hawataki kuwajibika!
Tumelogwa au ni laana?
 
Kwa wale waliotazama Star TV jumamosi watakubaliana na nami kuwa Kisena ni tapeli wa kimataifa! Alijichanganya sana na kweli alishindwa kujibu maaswali aliyorushiwa akabaki kuzungusha maneno. Kweli UDA walihonga ili waiingie!!
 
Ikiwa kama Simon Group wanaamini kuwa mkataba wao ulikuwa safi kabisa na walikuwa makini. Iweje wakaweke pesa kwa account ya mtu binafsi na ya NGO? Hawakujua risk au impact zake? Je wanye account zao wakisema hizo pesa si za UDA, je mtathibitisha vipi? Kisheria hapo hata Simon Group hawana bao hapo. Hii ni biashara ya umma, huwezi ukaifanya kama vili ni ya Shangazi yako au Binadamu, ambayo mambo yakiharibika mtamalizana hukohuko, lakini si UDA. Huo ni ufisadi tu.
 
Back
Top Bottom