Sakata la UDA: Bomu lingine lalipuliwa!

Huyo ndo simba mla nyama atatosheka vipi???

njoo huku mbezi beach alivyojengea Nyumba ndogo gorofa moja baada ya nyingine kinachomzumbua ni kubeba mizigo inayotaka gorofa ndio maana anaiba ili aijengee awaridhishe shida tupu Mungu si jui kwa nini asiwawaishe watu kama awaondoe dunian tubaki na nyani na sio simba tena
bila aibu yaani walitaka kuipiga NBC bila aibu ila huu mchongo mnaonmwona simba kuna wakubwa zaidi ya simba nyuma yake lakini Mungu mweza yote atafichua uchafu wote..na lile soko la pale Makumbusho jamani wamemmlikisha mhuni mmoja wa BOT tumekaa kimya ati anajenga gorofa akodishe kwa manispaa laana hizi bora nikaishi JUBA
 
UDA,nyumba za bandari na TRC zote zimeuzwa bei chee na sasa ni container terminals na yadi za magari,hivi kufaidi nchi hii lazima wote wawwe watumishu wa umma? je raia wa kada nyingine hana haki?
 
Hakika watu hawana uzalendo mnakwapua kila kitu,sasa na huo mkopo wa nbc ulichukuliwa na uda kuinufaisha simon group?
Alafu mnafanya transaction za kampuni kwa kutumia account binafsi khaa
 
Haya mambo ya kuchukua mizigo zaidi ya uwezo wako ni shida ndio maana ndugu zangu fulani wakionawanazaidiwa
wanaaaga watoto wanaingia chumban wanakuta jamaa anacheza na kamba sas hili jamaa linashindwa kufikiria linaangalia pa kuliibia taifa hana adabu kabisa iddi simba
 
Kwa uzoefu wa serikali ya CCM hakuna mtu atawajibishwa,tutalalamika mwisho wa siku ishu itamalizwa ki-RICHMOND tu.Tatizo siyo Iddi Simba wala Kapuya au Kisena, ufisadi nchi hii uko kimfumo zaidi,hakuna aliye msafi hivyo lazima walindane kulinda mfumo wao. Wakisema wachimbe zaidi hakuna atakaye baki salama. Suluhisho ni moja tu, kuindoa serikali ya CCM madarakani kwa nguvu ya umma.
 
Mzee jibu lao wanasema kuwa wamenunua "hisa zisizogawiwa" za UDA na wametetea hivyo kiujanja kuwa UDA iilkuwa na uwezo wa kuuza hisa hizo kwa sababu zilikuwa "zake". Hata ukikubali dhana hiyo wanajikuta wanaingia kwenye matatizo kwani kama zilikuwa ni hisa tu za UDA kwanini Simon Group ikataka kuchukua na menejimenti?



right on.. ndio maana tunataka kuweka wazi kwanza kwamba UDA haiuziki ndio uone watakavyovurugana. taarifa ya serikali iliyotolewa wiki iliyopita ilionesha kuwa wanataka kutafuta suluhisho na mwekezaji ili kila mmoja awe safi; kwamba watakualiana jamaa alipe hela zilizobaki, bodi na serikali washirikishwe n.k and then simon anaondoka na UDA huu ndio mpango wenyewe.



Unachokisema ndicho wanachotaka kukifanya kwasababu wanagombana wenyewe maswahiba katika kuliibia taifa hili,UDA inamali kubwa hasa viwanja vikubwa ndivyo wanavyotaka kupora,isitoshe uuzaji mali ya umma ni lazima tenda itngazwe kuwe na washindani je tenda ilitangaza au ni kwasababu kisena ni swaiba wa jk?
 


katika mashirika ya umma yaliyobinafsishwa kuna mengine walipewa bure kabisa kama kiwanda cha mgololo na sijasikia kelele za wananchi kupigwa nina hamu na harakati za UDA lakini nashindwa pa kuanzia kwani isijekuwa ni vita ya panzi tukauana wenyewe kwa wenyewe kwani kuna watu wanashambulia elimu mpaka ya mmiliki sasa sijui kama mtu akiwa na elimu ndogo anazuiwa kumiliki mali

sipendi ufisadi daima ila nashindwa kuingia kwenye migogoro ya maslahi ya watu fulani

ndio maana sijajiingiza katika sakata la kudai umeme unakatika katika kwani wananchi wa vijijini hatujawatetea na wamekaa gizani kwa miaka yote toka uhuru ambao ni zaidi ya asilimia 80% iweje leo tulio mijini ambao ni asilimia na tulio mijini ambao tunapata umeme ni asilimia 10% .

tuanze kutazama ubinafsishaji wa mashirika yote , na tuanze kudai upatikanaji wa umeme nchi nzima na si mijini tu. tukifika hapo basi mtu kwa mtu na kijiji kwa kijiji kitaingia kwenye mapambano ya kudai umeme na mashirika yetu likiwemo UDA pia

Kama kweli watanzania wote tutakuwa commited na ukuwaji wa nchi hii basi tutafika mbali,tatizo kubwa ni watanzania kutoelewa nchi yetu inaibiwa na viongozi wa CCM, ili yote uliyosema yafanikiwe ni lazima watanzania wote waelewe kinachotuangusha ni viongozi wa CCM wenyewe wanajiita chama dola,hii ni hatari sana,angalia kila balaa na wizi unaohusisha nchi hii ni viongozi na maswahiba wao(wanachama mashuhuri) wanaodiriki kuingiza pesa zao za biashara zao haramu kwa kuisaidia wagombea wa CCM na malipo huwa kunyakua maliasili na miradi ya serikali kuigeza yao.
 
Navyojua huiwezi kuonunua kampuni eti ukanunua "assets" bila "liabilities" zake.
Kama kile kiwanja pale kurasini ndio kimewavutia ili kukodisha kwa watu wa kuhifadhi makontena, wanapaswa kukubali pia kuchukua madeni ya hizo overdraft benki.
Pili Idd Simba ashitakiwe kwa kudanganya hadharani kua hela walizolipa kina Kisena ni malipo ya ushauri wa kibiashara aliokua akiwapa na sio za uuzwaji wa UDA wakati Kisena mwenyewe anadai hakuna biashara nyingine yoyote ya ushauri aliofanya na Simba zaidi ya kuuziana UDA.
Tunapenda kulalamika sana juu ya wale waliotufikisha hapa tulipo kwa mikataba mibovu, leo tushampata huyu mmoja, itasikitisha sana kama tukimuachia hivihivi.
avatar21139_1.gif
Wachumia tumbo!!!
Nimeipenda hii avatar!!!!!
 
Kwa uzoefu wa serikali ya CCM hakuna mtu atawajibishwa,tutalalamika mwisho wa siku ishu itamalizwa ki-RICHMOND tu.Tatizo siyo Iddi Simba wala Kapuya au Kisena, ufisadi nchi hii uko kimfumo zaidi,hakuna aliye msafi hivyo lazima walindane kulinda mfumo wao. Wakisema wachimbe zaidi hakuna atakaye baki salama. Suluhisho ni moja tu, kuindoa serikali ya CCM madarakani kwa nguvu ya umma.
Amen to that!
 
njoo huku mbezi beach alivyojengea Nyumba ndogo gorofa moja baada ya nyingine kinachomzumbua ni kubeba mizigo inayotaka gorofa ndio maana anaiba ili aijengee awaridhishe shida tupu Mungu si jui kwa nini asiwawaishe watu kama awaondoe dunian tubaki na nyani na sio simba tena
bila aibu yaani walitaka kuipiga NBC bila aibu ila huu mchongo mnaonmwona simba kuna wakubwa zaidi ya simba nyuma yake lakini Mungu mweza yote atafichua uchafu wote..na lile soko la pale Makumbusho jamani wamemmlikisha mhuni mmoja wa BOT tumekaa kimya ati anajenga gorofa akodishe kwa manispaa laana hizi bora nikaishi JUBA

Mkuu, pamoja na kwamba Mungu anasikia vilio vya wanyonge........(well, sometimes) We need to act now!!!
Mungu atusaidie kama ataona tunafanya jambo jema.
Mwanakijiji hapendi kusikia hili, lakini if there is one thing that need to be done in this country, is" eliminate" mmoja mmoja.

Amdhuruye nduguye kwa kuwa ana uwezo kuliko yeye basi wakati wake wa kudhuriwa utakapofika, hata ardhi haitamtetea.
 
Jamani hivi Tanzania Rais yupo? au Katiba yetu rais cheo chake ni Ceremeonial kama Malikia wa UK. Some time huwa naona kuna loop hole inayochohchea uzembe na kurushiana mipira kati ya Rais na Wiri mKuu.

Kwa wiki kama mbili tatu ni ajabu sana kutosikia rais akizungumzia publicly views zake kuhusu kashfa na matatiz mbali mbali yaliytokea within hizi wiki tatu. Au rais wettu tuko naye kimwili lakini kia akili mwenzetu yuko mbali......... Hawaoni wenzake kina cameron na Obama ila siku inabidi watoe clarification ya issue mbali mbali.

Katiba mpya Tanzania inabdii ifute cheo kimoja au merekebisho makubwa yafanyike ya majukumu na mipaka ya wajibu wa Rais na waziri mkuu yajulikane wazi wazi.

Nchi haiwezi kugharimia maisha ya mtu na familia yake mpaka kifo inatokea issue bungeni anasema hawezi kufanya kitu mpaka rais. Anaishia kusema anagekuwa ana uwezo anagemfuuza kazi XYZ.

Napendekeza yafanyike mambo haya

  • Ama cheo cha waziri mkuu kiangaliwe stahkii zake zipunguzwe au kiondolewe kabisa
  • Au Madaraka ya kitendaji na kimaamuzi ya rais yapunguzwe apewe waziri mkuu. Tujue Tanzania cheo cha rais ni ceremonial.
Kuna loopholes kubwa sana kwenye struccture za uongozi nchini mwetu zinazochchea irresponsibility. na wakati huo huo hazichochei acountability ya viongozi
 
WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuchunguza mazingira ya ubinafsishaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), kwa Kampuni binafsi ya Simon Group, HABARILEO Jumapili imegundua ‘madudu’ yaliyoambatana na ubinafsishaji huo.

Kutokana na uendeshaji mbovu na hasara iliyokuwa inajitokeza kila siku, hatimaye Bodi ya Wakurugenzi ya UDA chini ya Mwenyekiti wake, Idd Simba na Katibu wake, Victor Milanzi, ambaye ndiye alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa UDA, iliamua kumtafuta mwekezaji binafsi ili aliendeshe shirika hilo kwa faida.

Kabla ya ubinafsishaji huo, UDA ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu, kupitia Hazina, wakiwa na jumla ya hisa milioni 15, kila hisa moja ikiwa na thamani ya Sh 100.

Kwa mchanganuo, Halmashauri ya Jiji ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa hizo, huku Hazina ikimiliki asilimia 49.

Kwa zaidi ya wiki moja, gazeti hili lilikutana na vyanzo mbalimbali vilivyohusika kwa namna moja au nyingine katika mchakato wa ubinafsishaji wa shirika hilo, na kubaini kukiukwa kwa baadhi ya vipengele na kanuni zilizotumika kwenye mchakato huo.

HABARILEO Jumapili ilipata nyaraka zote zilizotumiwa wakati wa ubinafsishaji wa Shirika hilo kwa Simon Group, kampuni inayomilikiwa na Mtanzania, Robert Kisena.

Februari 11, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA, chini ya Simba, ilikutana na uongozi wa Simon Group ikiongozwa na Kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.535 ya hisa zote kwa thamani ya Sh bilioni 1.142.

Kwa maana nyingine, mkataba huo ungeifanya Simon Group kuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa UDA kwa vile Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Hazina, wangebaki na hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.465.

Uchunguzi huo ulibaini, kwamba kwa upande wa UDA, viongozi waliosaini uuzaji wa hisa hizo ni Simba aliyesaini kwa niaba ya Bodi na Milanzi kwa niaba ya Menejimenti wakati kwa upande wa Simon Group, aliyesaini ni Kisena.

Baada ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka Simon Group kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za UDA (Sh bilioni 1.142) ambazo ni sawa na Sh milioni 285.669, ndani ya siku 14, tangu kusainiwa ili kuufanya mkataba utambulike kisheria, na Simon Group ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo.

Kwa vile fedha hizo zililipwa Februari 11, baada ya siku 14, vipengele vya mkataba vilipaswa kuanza kushughulikiwa kisheria na hasa namba 4.5 ambacho kiliielekeza Bodi ya UDA, kuitisha mkutano wa wanahisa ndani ya siku 14 ili kushughulikia mambo makuu matano muhimu.

Mambo hayo yalikuwa ni kwanza, kuitambua Simon Group kama mwekezaji mkubwa ndani ya UDA, akiwa na hisa asilimia 52.535, kuteua Bodi mpya ya uendeshaji wa UDA, ambayo kimsingi ilipaswa kuwa na wajumbe saba; wanne kutoka Simon Group, wawili Jiji na mmoja
Hazina.

Jambo lingine muhimu ni kumteua mkaguzi wa mahesabu na kuteua benki zitakazohusika na utunzaji wa fedha za UDA na pia kuandaa mwaka wa mpya wa mahesabu ya fedha ambao ungeanza kutumiwa na UDA mpya.

Kuuzwa kwa UDA
Wakati kukiwa na gumzo juu ya nani alihusika na kuuza hisa za UDA, alifanya hivyo lini na kwa gharama gani, HABARILEO Jumapili imebaini kuwa ingawa mkataba wa kuuza hisa za UDA kwa Simon Group ulisainiwa Februari 11, mazungumzo ya mauziano baina ya pande
hizo mbili yalianza miaka miwili nyuma.

Kutokana na mazungumzo hayo ya awali, UDA iliiandikia barua Simon Group kuitaka ilipe Sh milioni 400 kama uthibitisho wa nia yake ya kutaka kuiendesha. Barua hiyo iliitaka Simon Group kuingiza fedha hizo kwenye akaunti za Shirika la Pride tawi la Mlimani City na kwenye akaunti ya Simba katika Benki M tawi la Sea View, Upanga.

Barua hiyo iliieleza Simon kwamba hatua hiyo ya kuitaka kuingiza fedha hizo kwenye akaunti za Pride na ile ya Simba inatokana na akaunti zinazoendeshwa na UDA kuwa na ovadrafti benki, hatua ambayo kama wangeingiza fedha hizo kwenye akaunti hizo za UDA, zingechukuliwa na benki na zisingefanya kazi iliyokusudiwa.

Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa Simon Group waliitikia mwito huo kwa kuingiza Sh milioni 20 kwenye akaunti ya Pride namba 6033500127 Mlimani City, Februari 09, 2009 na baadaye Sh milioni 250 katika akaunti namba 0210001002 Sea View, Septemba 2, 2009
ikionesha kumilikiwa na Simba.


Masaburi na uuzaji UDA
Akiwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, ambalo ni mmoja wa wanahisa wa UDA, Dk. Didas Masaburi, aliliambia gazeti hili, kwamba aliitisha mkutano wa wanahisa wa UDA ili kujadili uendeshaji wa shirika hilo.

Alisema kuitishwa kwa mkutano huo, kulitokana na kupokea malalamiko kutoka Simon Group kuhusu kukiukwa vipengele vya mkataba wa mauziano ya hisa za UDA Februari 11.

Alisema mkutano huo ambao ulifanyika Juni 10, uliibuka na mapendekezo yaliyofikiwa na washiriki waliohudhuria ambayo yalikuwa na lengo la kuongeza ufanisi.

“Kikao hicho hakikuwa na nia ya kuuza hisa za UDA, UDA ilikuwa imeuzwa tayari tangu Februari 11, hivyo tusingeweza kuuza kitu ambacho tayari kimeuzwa. Sisi tulikutana kuangalia nini kifanyike ili UDA iendelee kutoa huduma za usafiri kwa ufanisi zaidi na ndiyo maana tuliibuka na mapendekezo ambayo ndiyo niliyosaini mimi, si mkataba wa mauziano,” alisema Masaburi.

Aliongeza kuwa kilichoamuliwa na mkutano huo aliouongoza, ilikuwa ni kuiondoa Bodi ya Wakurugenzi ya UDA ili kuunda mpya, kumwondoa madarakani aliyekuwa Mtendaji Mkuu, Milanzi na kumteua CEO wa muda, Simon Bulenganija na kufunga akaunti zote za UDA, ili kufanya uchunguzi wa mahali zilikokwenda fedha za malipo ya mauzo ya hisa.

Alisema maagizo hayo yote utekelezaji wake ulianza Juni 10.

Simon Group na taratibu
Kisena ni mmiliki na Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group ambaye alisema kampuni yake ilifuata taratibu zote katika ununuzi wa hisa za UDA na ilifanya hivyo ikiwa na lengo zuri la kuboresha sekta ya usafiri Dar es Salaam, ambayo imekuwa ikizorota kutokana na ufanisi duni wa UDA.

“Tunashukuru, kwani kama unavyojua, Serikali imeagiza suala hili la UDA lichunguzwe na vyombo vya Dola, ili ukweli uweze kujulikana. Nitatoa taarifa kamili kuhusu suala zima la UDA na taarifa yangu itazingatia maeneo makuu manne nikianzia na hali ilivyokuwa kabla ndani ya UDA,” alisema Kisena.

Kwa upande wake, Bulenganija alisema anaendelea vema na uendeshaji wa UDA tangu alipowekwa madarakani Juni 10, wakati wakisubiri maelekezo zaidi kutoka serikalini baada ya kuagiza suala la UDA lichunguzwe.

Gazeti hili pia lilifanya juhudi ya kumtafuta Simba ili kuzungumzia sakata hili, ambapo pamoja na kumkuta nyumbani kwake Mikocheni Jumatano, jitihada hizo zilikwama baada ya Simba kupitia mwanawe, Abdul, kumtaka mwandishi kuacha mawasiliano ya simu, ili aweze kumtafuta pindi atakapokuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Uchunguzi zaidi wa HABARILEO Jumapili, ulibaini kuwa wakati Bodi ya Simba inavunjwa, katika hatua ya kushangaza, Menejimenti ya UDA ilikuwa imeomba mkopo wa Sh bilioni 3.8 kutoka benki ya NBC ili kununua mabasi ya Kichina, huku uamuzi huo ukifanywa bila wanahisa wa UDA kuhusishwa.

Barua yenye kumbukumbu namba UDA/P.16/08 ya Mei 26, iliyosainiwa na Milanzi ikielekezwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NBC kupitia kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Minnie Kibuta, ilisema UDA wameamua kuomba mkopo huo, ili kuwasaidia kuboresha sekta ya usafiri Dar es Salaam, huku ikieleza kuwa mali za UDA zingewekwa kama dhamana ya mkopo huo.
Kwenye red hapo, Inamaana fedha zote zilizolipwa kwenye account ya Idd Simba na Pride (ya Idd Simba) ilikua ni kwaajili ya kuthibitisha nia ya kununua hisa tu wala si malipo ya hisa!, Ingekua ni nchi ya kuwajibishana, sasahivi tungekua tuna story nyingine kabisa!


Kwenye blue hapo, Mwandishi naona tayari una upande unaoutetea!, wote hawa ni mafisadi kweli kweli waliodhamilia kuila UDA!, Kama kuna mwenye fursa ya kupata details za account za Victor Milanzi aangalie hapatakosa mamilioni yalioingia baada ya transaction hizo, itakua ni mgao wa fedha hizo alizoingiziwa Idd Simba!
 
Wana JF,

Wapi Azimio la Arusha??? liliwashikisha adabu viongozi hawa na ndio maana walilikataa ili ulaji wao uwepo waliona mbali lakini yakija ya kitaifa hawaoni mbali hapo ndipo wanapo nishangaza!!! kwenye deal zao wanaona mbali kweli ila kutekeleza ya wananchi hawaoni mbali wala hawana future plan ya maendeleo ya nchi hii wao wana future plan zao na familia zao.

Mwl.Nyerere alijitahidi sana kutetea mashirika ya UMMA yasiuzwe ila hawa viongozi wetu jamani wakala vyote eg general Tyre ya Arusha huko nadhani lishakuwa dangulo pia sasa wamehamia UDA. ukirudi nyuma ukichunguza walimo wote ni CCM, vyama vingine vikilalama ooooh vinaleta fujo sasa fujo gani wewe CCM mtawala unahujumu mali ya UMMA na hao unao wasema wanaleta fujo ndio unawanyonya kwanini wasi lalame na ni UMMA huo.

Alafu ukiludi huku Lukuvi anatuambia nchi inandeshwa kwa sheria na haki na utawala bora!!!! its pathetic
 
Huduma ya UDA ni muhimu iwe inaendeshwa na umma au na makampuni binafsi,Tunachotaka kutoka kwa UDA ni huduma bora na nafuu.
 
kwanini UDA pekee ?

je jamii inafahamu kiwanda cha mgororo kilivyobinafsishwa kwa shs mamilioni ya shs tu?
kuna mashirika mangapi yalibinafsishwa kijinga? je tuanze kuyachambua yote au tatizo ni UDA?
well said mkuu.
 
Ukisoma hii hbr unatamani kulia. Lini haya mambo yataisha?

Kila siku wanazalisha jambo lakini mie wameniacha na donda ndugu moyoni mwangu.....watake wasitake kuna siku ya siku NYUMBA ZA SERIKALI WALIZOUZIANA zitarudi Serikalini pamoja na hiyo UDA
 
Back
Top Bottom