Sakata la Plea Bargain limenikumbusha Kisa hiki cha Wezi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
SAKATA LA PLEA BARGAIN LIMENIKUMBUSHA KISA HIKI CHA WEZI

Anaandika, Robert Heriel

Nyakati nasoma, nakumbuka shuleni kulikuwa na magenge ya Wezi. Kila shule inamagenge ya aina hizo. Yapo magenge ya Siri na yale ambayo yapo waziwazi. Ingawaje wapo Wezi binafsi WA kujitegemea ambao hufanya shughuli zao Kwa Siri kubwa pengine wala usingewadhania kabisa kama wanahusika na matukio hayo.

Magenge ambayo ninayakumbuka yalikuwa kama ifuatavyo;
1. Genge la Wezi wa vifaa vya shule kama Chokaa, cement, makopo ya rangi n.k.

2. Genge la Wezi wa Vitabu, madaftari, mabegi, kalamu na zana zote za Wanafunzi na waalimu za kujifunzia.

3. Genge la Wezi wa Chakula, iwe cha waalimu au cha Wanafunzi.

4. Alafu Wezi WA kujitegemea wao matukio Yao yalikuwa kama kuiba Simu za Wanafunzi na waalimu, kuiba Pesa kwenye mapochi ya waalimu n.k.

Rafiki zangu baadhi walikuwa Wezi, hivyo kimsingi nazijua Akili na tabia za Wezi Kwa kiwango Fulani. Najua Timing Yao, namna wanavyopanga mipango na mikakati Yao, na namna wanavyofuta ushahidi.
Kimsingi katika wahalifu wenye Akili basi wezi Akili zao kidogo zimechangamka,

Yaani Taikon nikiambiwa nitaje wahalifu wenye Upeo wa kufikiri, basi wezi nitawaweka nafasi ya Kwanza.
Tofauti na Wanzinzi, wauaji, Wabakaji, Na wahalifu wengine. Ili uwe mwizi itakupasa uwe mjanja Sana.

Taikon Kutokana na kuchoshwa na Chakula cha shule nikajiingiza kwenye Genge moja la Wezi wa vyakula, hasa vyakula vizuri vitakavyopikwa kwaajili ya Wanafunzi au kwaajili ya Waalimu.

Nilichoka Kula makande na ugali. Sasa tamaa yangu ilitapika nikawa nataka Kula nyama, pilau na mapochopocho ya waalimu.

Ingekuwa nadra Sana kunishuku😂😂 Kutokana na haiba na Sifa za nje nilizonazo, uwezo wa darasani, nidhamu ya mavazi, Makosa Makosa ya kipuuzi huwezi kunikuta, hivyo Mimi ndio nilitumiwa kama msoma Ramani, Jamani! Jamani! Nitaenda ofisini kukagua waalimu waliopo, ukiniita kunituma sitokataa😂, pia nitakuuliza maswali ya masomo kukuzuga, kisha nitakagua Maeneo ya jikoni, na njia zote muhimu. Tayari tutakuwa tume-master ratiba za kila Siku za mwalimu Kwa masaa ya kuanzia saa 6:30 mpaka saa 8:00 Mchana.

Kisha ningerudisha ripoti, kama Hali sio nzuri, lakini kama ningerudi Kwa dakika 20 basi tulipatana kuwa wakiona hivyo Hali ni shwari hivyo waje mmoja mmoja.

Kila mmoja alipewa kitengo chake, na kila mmoja alifanya Kwa ufanisi mkubwa na hiyo ilitufanya tukadumu katika Fani hiyo Kwa Mwaka mzima bila kushtukiwa, ingawaje kuna Wakati iliibuka mizozo ndani ya staff ya waalimu kuwa chakula ni kidogo.

Sisi hiyo taarifa tuliichukilia kama Mafanikio makubwa katika kazi yetu 😀😀, hasa wale wenzangu watukutu ndio walikuwa wakifurahia mizozo hiyo huku lawama zikipelekwa Kwa wapishi kuwa wanapika chakula kidogo au wanaondoka na Chakula, hatukuwa na sababu ya kuwaonea huruma kwani kila MTU alijali ubinafsi wake. Kila walivyoboresha mbinu za kutaka kuwashika Wezi ndivyo nasi tulivyoboresha mipango kabambe ya kuiba chakula.

Kwa bahati nzuri genge letu lilikuwa na wanafunzi sita, mwanafunzi mmoja alikuwa yupo karibu na moja ya waalimu hivyo taarifa nyingi za yaliyokuwa yanaendelea Staffs tulikuwa tunazipata, Hii ilitusaidia kubuni bwinu😊 za kudumu kwenye Fani ya Majizi.

Kumbuka magenge ya Wezi shuleni mara nyingi yanajuana Kwa kiasi kikubwa, tukio linapofanyika baadhi ya Wanafunzi hujua wafanyaji wa tukio Hilo. Ingawaje Wezi WA kujitegemea Wakati mwingine huweza kusababisha tukio lisijulikana Kwa mara moja limefanywa na nani.

Mwaka uliofuata, Uchaguzi wa viongozi wa Wanafunzi ulifanyika, sijui niiite bahati nzuri au Mbaya, utajua namna ya kuiweka.

Mshindi wa Kiti cha U-headboy alikuwa moja ya Jizi la Siri Kutoka katika genge la Wezi wa vifaa vya shule kama Mifumo ya sementi, sijui chaki, chokaa, mabati n.k.

Headboy huyu Mpya ambaye waalimu hawakujua Tabia zake za ndani kwani alikuwa MTU wa kujionyesha mwenye Tabia njema alibeba matumaini makubwa Kwa waalimu katika kuwasaidia kuwaongoza Wanafunzi.

Hii kwa Sisi magenge ya Wezi ilikuwa ni sherehe kubwa. Tukajua utawala wa Majizi upo madarakani hivyo mambo mengi yataende mswano.
Lakini haikuwa hivyo.

Headboy alianza mambo ya u- Snitch, mara ajifanye mchapakazi, mara mtoa adhabu, mara muwahiji wa Asubuhi.

Mmmh! Tukasema labda ni nguvu za soda, danganya toto ili ionekane anachapa kazi. Lakini haikuwa hivyo tukashangaa mwezi mzima mwendo ni mpera mpera.

Ingawaje hakugusa maslahi yetu lakini tayari tulishaanza kuona hatari hiyo, tulijuaje? unauliza, nilishakuambia huwezi kuwa mwizi pasipo Akili.

Sasa ilibidi ili kumdhibiti huyu Mhusika Mpya ilitupasa kumpa kazi Moja ya mwizi mmoja awe karibu yake ili Wakati wizi ukifanyika awe anamzubaisha Huko darasani.

Lakini Jizi ni Jizi tuu, lile jizi lililopewa kofia ya U-headboy lilishtukia Mpango wetu, siku moja likatushika red-handed, lilivyokuwa jinga sasa likajitia uzalendo, acha bhana wee! Likatupelekea Ofisini ingawaje wengine walikimbia.

Tulitandikwa viboko Mbele ya shule, alafu mshikaji akawa anatutumia Sisi kujisafisha na kujifanya yeye ni mtakatifu na Kiongozi mzalendo.

Baada ya kuchezea bakora za kutosha Kutoka Kwa waalimu sita waliokuwa wamejipanga Mstari Kila mmoja akidondosha Viboko viwili matakoni, tukapewa adhabu ya kufyatua matofali kila mmoja hamsini hamsini.

Kwa kweli hiyo kwangu ilikuwa aibu, nilitukanwa na kusemwa na waalimu Kwa kutokutegemea kuwa Nina Tabia za kijizi. Nilikuwa mkimya nisiyetaka macho yangu yaangaliane na yeyote pale Assemble.

Tukio likaisha, Maisha ya shule yakaendelea,
Tukadhani labda Headboy ameokoka na kubadilika ndio maana anatuchoma wadhalimu na wenye dhambi😂😂, Majizi na wasio na nidhamu.

Tulianza kumsifu Sana ingawaje mikakati yetu ya kufufua chama chetu cha Wezi WA chakula ulikuwa haujafa licha ya kuwa tulikuwa tupo likizo kusoma nyendo za huyu Kiongozi headboy mnoko.

Kwa kweli tulianza kuona mabadiliko ya nje Kwa headboy tukaanza kumsifu tukiwa vijiweni na kwenye magenge yetu ya wahalifu.

Lakini kumbe tulichotwa tuu na maneno yake zaidi, alikuwa mwingi wa nyimbo Bora za uzalendo, kutetea HAKI na wanyonge, kusimamia nidhamu za Wanafunzi na kutoa adhabu, kuna Wakati alikuwa anatutisha Kwa maneno makali na hata vipigo Kwa baadhi ya Wanafunzi.

Magenge ya uhalifu ya wapiganaji na masenari shuleni pia yapo. Kama uliwahi kusikia wanaopiga na kutupia mayai viza waalimu wapo katika kategori hii.

Tulijaribu kukaa nao kuona wanamchukuliaje huyu headboy ambaye alikuwa mhalifu mwenzetu katika genge la Wezi wa vifaa vya shule, wakasema jamaa kabadilika, Ila genge moja la wahalifu la Wazinzi na mabishoo lilitutonya kuwa Headboy mbona Hana Wema wowote.

Akaanza kutumwagia maovu yake, akasema, headboy alizuia genge la Wezi wa vyakula na hiyo kazi anaifanya yeye Kwa kushirikiana na kiranja WA chakula tena wanaiba sukari na Unga na Michele wanaenda kuuza maduka ya mjini Huko. Tukafuatilia, tukabaini ni kweli mpaka duka analopeleka hizo bidhaa,

Taarifa hiyo ilitukasirisha Sana.
"Jamaa mbinafsi,
Iweje aibe pekeake,
Sisi wote Majizi,
Iweje aibe pekeake
Alafu mnafiki Sana,
Mbele za Watu anajifanya mtakatifu,
Jamaa mbinafsi, iweje aibe pekeake"
Tulilalama ungedhani ni wimbo huo. Lakini tulikasirishwa Mno.

Ukishakuwa mhalifu jitahidi usiwe mbinafsi, wahalifu hawapendi Watu wabinafsi. Unaiba iweje uibe mwenyewe?
"Huyo sio wako,
Nami sio wangu, wivu WA nini Kati yangu Mimi na wewe"
Magenge ya uhalifu shuleni yakaungana, headboy tutamtoaje, atatokaje, tukaazimia atoke kivyovyote, Kwa kheri au Kwa Shari.

Kukatisha Stori Hii ya kweli, Yale magenge ya wahalifu wote tulihitimu shule, tupo mtaani huku, sijajua Nani anafanya nini, lakini picha niliyoiona Huko shuleni haiko mbali na picha halisi iliyopo mtaani. Kwa sababu wahusika ni walewale Ila wamebadilishiwa Mandhari.

Hii ishu ya Plea Bargain imenikumbuka miaka Kumi na mbili iliyopita Enzi nasoma.
"Ukitaka kuiba usizibe wezi wengine hiyo ni kanuni"
Mwizi hawezi kumzuia mwizi mwenzake.
Kumzuia mwizi mwenzako ni Unethical.
Na Matokeo huwaga sio mazuri.

Taikon Mimi ngoja nipumzike Kwanza, alafu tutaendelea na stori.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwaiyo Magufuli alikuwa anaiba then anakula peke yake au na Mama Samia alikuwa hampi kitu chochote?
 
Kwaiyo Magufuli alikuwa anaiba then anakula peke yake au na Mama Samia alikuwa hampi kitu chochote?

Mimi sijui Mkuu.
Mimi nimesimulia kisa cha shuleni Huko kwetu niliposomaga miaka Ile.
Kanuni ya uhalifu ni kutokuwa mnafiki, unafiki hana rafiki
 
Happy jibu ni kuwa magu alikuwa anaiba na kula peke yake.

Nasisitiza,
Ukitaka ueleweke mahali popote pale, Ukiamua kuwa mhalifu kuwa mhalifu kiukweli kweli, hata wenye Haki watakuelewa na kukupenda na kukuamini.

Ukitaka kuwa mtenda Haki kuwa mwenye Haki. Hata wahalifu watakuelewa na kukupenda na kukuamini

Lakini sio kuwa vuguvugu na kujivalisha ngozi ya Mbuzi kumbe ndani Mbwa mwitu.
Vita hiyo utapasuka mapema Sana.

Kwa Mungu haupo Kwa Shetani haupo.
Chahua upande

Yule headboy wetu alikuwa mjinga Sana. Anatuzuia tusiibe tukadhani anatufundisha Wema tumrudie Mungu na tuwe na Maadili Mema, kumbe mwenzetu ni ili aibe pekeake, come on!
 
Nasisitiza,
Ukitaka ueleweke mahali popote pale, Ukiamua kuwa mhalifu kuwa mhalifu kiukweli kweli, hata wenye Haki watakuelewa na kukupenda na kukuamini...
Bandiko lako kuu na ulichoandika hapo yawezekana una hoja ila umeshindwa kuiweka wazi kwa sababu unasukumwa na mtizamo wako kisiasa na chuki kwa sababu uliguswa kwenye maslahi yako binafsi
 
Bandiko lako kuu na ulichoandika hapo yawezekana una hoja ila umeshindwa kuiweka wazi kwa sababu unasukumwa na mtizamo wako kisiasa na chuki kwa sababu uliguswa kwenye maslahi yako binafsi

Sikuwa na tatizo pale headboy alivyotudhibiti Kwa Tabia zetu za wizi, nilijua anataka niwe Mwema na mwenye Maadili.

Tatizo lilianza pale Headboy aliponizuia nisiibe Mimi ili aibe yeye. Hapo ndipo chuki unayoizungumzia ilipoanzia,
Wewe ukiangalia ni Haki hiyo?
 
bro izo ni siasa tuu he kama magufuli angekuwa hai angesema hivo ........ hii yuiweke kwenye mabano

Tatizo la wengi hawawajui wahalifu na wadhambi jinsi wanavyofanya Kazi.
Siku mkijua wahalifu na wadhambi wanavyo-operate ndipo utaelewa ni Kwa nini sasa hivi Kelele zimepungua,😊

Huwezi Kula pekeako kwenye uhalifu, uliza popote pale
Utamhusisha Mganga WA kienyeji, utahusisha, mastermind, utahusisha Wasoma ramani, utahusisha wanapropaganda,
 
Ndani ya CCM hakun rais ambaye hakuna au ambaye haibi isipokuwa Nyerere japo naye alifanya ufisadi wa uchaguzi hasa kule zenj na kumpora ushindi Augustino Mrema
 
Mmh! Ndugu Taikon hii ni hadithi ya kweli? Au ni kazi ya sanaa inayotumia maneno kufikisha fikra za mwanadamu kwa hadhira iliyokusudiwa??
 
Mmh! Ndugu Taikon hii ni hadithi ya kweli? Au ni kazi ya sanaa inayotumia maneno kufikisha fikra za mwanadamu kwa hadhira iliyokusudiwa??

Vyovyote Mkuu.

Ukiamua kuiona kama Sanaa ni Sawa.

Ukiamua kuiona kama tukio halisi pia ni Sawa.

Ila kisa hiki kimetokea Wakati nasoma
 
Back
Top Bottom